Shenkalwa, Dr. Bana ni dr wa ukweli na Ph.D yake ni ya halali, huyu ndie mkuu wa Redet, yeye na Prof. Mkandara, baada ya kuifayia CCM kazi nzuri kwenye tafiti zao, Mkandara kesha kuwa rewarded u VC bado Bana.
Pia Dr. Bana namfahamu vizuri kwenye siasa za pale chuo, ni kama Mkandara, Kabudi na Mwakyembe, wamejimbambanua wako upande gani. Wengine wanashabikia CCM kwa uzalendo wa dhati kwa ajili ya kuutunza utaifa (nationalism), kwa vile wapinzani hawajaonyesha ukomavu wa siasa wa kuweza kukabidhiwa dola!.
Nawaombeni sana wana JF wenzangu, tusiwabeze wenzetu kwa sababu ya misimamo na mitazamo yao ya kisiasa, tuzibeze hoja zao kwa hoja mbadala. Kwangu mimi hata baadhi ya hoja za kina Malaria Sugu, Faiza Fox na Rejao, zina mashiko kama utazisoma ukiwa outside the box.
Tatizo letu kubwa humu jukwaani, wengi wetu tuko ndani ya mabox tuliomo huku tukiyatazama yale mabox mengine wengine waliomo, hivyo hoja yoyote toka nje ya box tuliomo tunaiona kama sio hoja. Ili kupata view nzuri, tokeni kwanza nje ya hayo mabox ilijifungia na mtazame hoja kama hoja regardless imeleta hoja, ameegemea wapi!