zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,628
- 3,155
Mimi nashangaa sana kwa nini vyombo vya habari vinapenda sana kusikia kauli za huyu Dr. Banna inapotokea issue yoyote ya kisiasa? Si magazet, si television, utamwona tu Dr. Banna pale na maoni yake. Na siku zote maoni yake ni pro-ccm na anti-chadema. Lakini hayo yote yanachangiwa na wanataaluma wetu wa vyuo vikuu vyetu vikongwe kuendelea kuitegemea serikali kwa mishahara yao na kwa karibu kila kitu. UDSM kwa umri ulio nao ilipaswa kuwa inajitegemea sana kifedha na kujigharamia project kubwa muhimu za utafiti. Lakini ilivyo sasa vyanzo vya mapato pale hasa kule kwenye department za political, social sciences na sheria wanategemea fedha ya serikali kupitia kwenye consultancies fulani fulani za kiserikali. Na serikali si ya ccm? Sasa hapo ndo unawaona akina Banna wanakuja upfront kwenye vyombo vya habari na matokeo yake tunayaona. Yaani kuisifia CCM kwa kwenda mbele na kuikandia chadema kisawasawa.
Department zisizojihusisha na masuala ya kisiasa pale UDSM masikini zimetelekezwa kweli kweli pale. Kila project kubwa zinazohitajika kufanyiwa kazi hazipati hela yoyote serikalini maana hawana chochote cha kurudisha serikalini kwa mfumo wa kuisifia ccm. Hivyo huwezi kumwona professa yeyote wa biology, physics, chemistry au medicine akikaribishwa kujimwaga mwaga mbele ya vyombo vya habari kuelezea matokeo ya utafiti fulani wa science yake na impact yake kwa jamii ya watanzania. Upande wa serikali wana makosa kutothamini michango ya wanasayansi hapa nchini lakini pia na vyombo vya habari vinakosea kuwaalika hawa madokta vibaraka vya wanasiasa. Tumechoka siasa za ccm sisi .