Nimemsikia asubuhi,
Kweli ni masikitiko makubwa juu huyu mpotoshaji!sijui kazaliwa wapi na haya maneno anayasema akijiamini nini.
Labda nianze kwa kusema, tanzania na hasa katika bunge, hakuna hoja kwa miaka ya hivi karibuni, imepitishwa kwa vigezo vya hoja zilizotolewa na wabunge badala la kelele za kishabiki na kukidhi matakwa yao! Utamaduni upi wa mtanzania anaoueleza, nani hajui utamaduni wa sasa uliojengwa na watawala na kuasi utamaduni wa viongozi wetu waasisi wa nchi! Alienda mbali na kugusia suala la wananchi kuamua juu ya hili, na kweli sisi tutaamua kwani wanachokifanya chadema ni kitenda cha kiungwana kuwasilisha dukuduku lao kwa wananchi, sisi ndo kimbilio lao kwani vyombo husika kama kamati za bunge zimekuwa zikiegamia upande mmoja na hili liko wazi, aliwataka wafanye nini?
Kaenda mbali zaidi kaongelea suala la hoja kama zinakataliwa au hawapewi nafasi inabidi wamfate speaker na kumueleza hivi huyu jamaa vip? Wamfate mara ngapi na kanuni na taratibu za bunge zinasemaje kuhusu hili, mara ngapi amewapuuza juu ya haya maswala, bunge linaamua mambo kwa hoja, bunge hili nilijualo mimi?sio kelele za ndiyoo!je kama watu ni wachache inakaaje hii?tuna vigezo vya kuamua jambo ndani ya bunge kwa kupima uzito wa hoja hapa??? Mbona usomi unaupaka matope bwana benso bana, mbona unajipunguzia credit zako na uwered wako juu ya kutetea uozo na ushenzi unaofanywa na ccm na speaker wao,
umeulizwa swali juu ya upendeleo wa speaker na sikuona jambo la msingi ulililo liongea juu ya hili badala yake umekwepa na kuongelea mambo ya ajabu, je ni wangapi wapo kijiweni na hawana elimu hata ya std 7 lakini huu upendeleo wanauona, kama kweli wewe ni mtaalam wa sayansi ya siasa mbona umeshindwa kulisemea hili??
Wewe ni kada pamoja na unafiki wako kujifanya unatoa maoni na kushauri mambo ya kisiasa nchi, msomi ninayemwamini aliyetukuka na heshima yake itakuwa palepale ni profesa issa shivji, siku zote huyu mzee hamung'unyi jambo na ndo maana serikali hawamtumiii, yeye ndo mtaalam wa sheria na katiba tangu enzi za sokoine na baba wa taifa, je usomi wake umeteteleka wapi hadi nchi ishindwe kumtumia katika kipindi hiki?wanaogopa na kuwatumia watu kama bana wenye mtazamo wa karibu na utetezi wa walanguzi wa nchi yetu.
Matatizo ya hii nchi yanapigiliwa msumari na wasomi kama hawa, mbona hakuongelea utovu wa nidham wa wabunge wa ssm waliotumia muda wa walipa kodi kuzungumza kukashifu na kuwatukana chadema huku speaker wao akiweka mikono yote miwili kwenye kidevu?hilo hakuliona kuwa na utovu wa nidhamu?tumewatuma waende kufanya mipasho ndani ya jengo wanaliliita tukufu?utukufu wa jengo ni upi hai waliomo ni makafiri, hakuna dhambi mbaya kama kuwadhurum wananchi, kuwatapeli na kuwasaliti wapiga kura!hayo hayaoni anaona la chadema tu. Huyu mtu anatakiwa kutangazwa kuwa moja ya watu hatari wa kisisa za nchi yetu!