Huyu dada ni muuaji

SN.BARRY

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
4,051
Reaction score
9,004
Ilibidi harusi ifanyike leo ila kutokana na bibi harusi kushinikiza vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa bwana harusi sherehe na ndoa vimeahirishwa. Bibi harusi amekataa Ukumbi (hauna hadhi), Keki ya bei ndogo, Wasimamizi sijui amewaona walugaluga, Gari pamoja na salon ya kumpamba vyote amesema vipo chini ya kiwango.

Tangu Jumatano wanafanya vikao vya kumbembeleza ila haelewi kitu wala hajibu kitu hadi atimiziwe haja zake. Ndugu wa bwana harusi wameshauri kijana aachane na binti na mahari asahau ila kijana hajatoa msimamo zaidi ya kuahirisha harusi.

Kijana ni mwalimu shule ya private na binti ana degree ya ualimu ila hana kazi. Wamesoma darasa moja na bwana harusi wakamaliza 2017.

Nimeongea na kaka wa bwana harusi nikamwambia "HUYO BINTI NI MUUAJI".
 
Binti analaumiwa bure
Ina maana Hadi mnachagua ukumbi hamkumwambia?..

Keki siku hizi si zinaletwa picha mnachagua?
Hakutumiwa picha watsaap?

Harusi ni tukio sensitive Kwa baadhi ya watu..

Ushamba uko Kwa hao kamati
 
Binti analaumiwa bure
Ina maana Hadi mnachagua ukumbi hamkumwambia?..

Keki siku hizi si zinaletwa picha mnachagua?
Hakutumiwa picha watsaap?

Harusi ni tukio sensitive Kwa baadhi ya watu..

Ushamba uko Kwa hao kamati
Kwani harusi ni ya huyo binti? Kamati ya harusi upande wa mwanaume ndio yenye shughuli. Yeye anatakiwa aridhike na alichokikuta. Kama alitaka hayo yenye hadhi yake angeaandaa kamati ya harusi yake ajioe mwenyewe
 
Binti analaumiwa bure
Ina maana Hadi mnachagua ukumbi hamkumwambia?..

Keki siku hizi si zinaletwa picha mnachagua?
Hakutumiwa picha watsaap?

Harusi ni tukio sensitive Kwa baadhi ya watu..

Ushamba uko Kwa hao kamati
harusi inaandaliwa na upande wa bwana harusi,
bwana harusi anaanda shuhuli kulingana na uwezo wake na familia yake.
 
Harusi ni jambo linalotokea (ukiacha Waislamu) mara moja katika maisha! Kwa nini lisisherehekewe katika mazingira ambayo kila mmoja aridhike?

Ataonekana mbaya, ila ana haki kulikataa hilo! Inawezekana alishatoa maelekezo wakapuuzia thus why kasusa.

NB: Mpate na bibi harusi umuhoji ili story iweze kubalance, inawezekana kuna jingine zaidi!
 
harusi inaandaliwa na upande wa bwana harusi,
bwana harusi anaanda shuhuli kulingana na uwezo wake na familia yake.

Kuna ndoa na kuna Sherehe ya harusi..
Binti anaweza kabisa kukubali kuolewa
Ila asikubali Sherehe ..
Binti kugomea sherehe sio lazima hataki kuolewa..
Pengine Yuko ready sherehe ifanyike baadae hali ikiruhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…