kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
Wakuu amani iwe kwenu!
Lengo la uzi huu ni kuwapa kwa ufupi yaliyonipata jana na mrembo fulani mkali. Ilikuwa hivi, jana nilitembelea chuo chetu kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa shida zangu binafsi. Nilipomaliza kilichonipeleka nikawa naondoka kurudi kupitia hii njie ya kuelekea ardhi . Mbele yangu alikuwepo mlimbwende mkali hatari, basi nikatembea faster kumuelekea. Nilipofika nikampa salama, akageuka kuniangalia alivyoniona hakuitikia hata salama yangu. Nikarudia tena kumsalimia hakuitikia kabisa nikaona isiwe shida.
Sasa kumbe dada wa watu alikuwa na mafua halafu hakutembea na leo au labda aliisahau anakojua yeye. Ile napiga hatua mbili tatu baada ya salama yangu ya pili kutokujibiwa , dada akapiga chafya ya nguvu. Aisee makamasi yalimtoka yule dada puani kwa wingi utadhani kondoo mwenye mafua makali. Kwa nguvu ya ile chafya nikajikuta nimegeuka kumcheki na kumpa pole akawa hawezi kunijibu halafu hana cha kujifutia huku akiwa ameinama utadhani mtu anayejifunza kukwepa bomu la machozi linalotegemewa kwa wale wa 26/4. Basi nikaona isiwe shida na wala nisilipize kisasi nikaamua kumpa leso langu nililolitumia kutwa nzima. Nadhani mnajua hali ya hiyo leso ilikuwaje maana joto la dsm si haba hasa kwa wiki hizi mbili . Basi yule dada kwa aibu kubwa aliniona kama mkombozi wake, aliipokea ile leso kama mtu aliyetekelezwa jangwani na magaidi wa boko haramu anavyofakamia maji japo machafu kwenye oasisi jangwani. Alipomaliza nikamwambia naomba utembee nayo tu maana unaweza kupiga chafya tena kabla ya kufika kwa wauzaji wa leso nzuri.
Kwa hakika yule dada alinishukuru japo kwa aibu kwanza kutokana na kutokuitikia salamu zangu tena kwa makusudi, pili kwa aibu ya kupiga chafya na kutokwa na makamasi kama kondoo mwenye mafua lakini tatu kwa kupokea leso langu ambalo tayari lilishatumika toka asubuhi. Pamoja na hayo sikutaka kuwa na gubu au kusema chochote kumsuta bali niliamua kuongeza mwendo na kumuacha naye akiwa anaendelea na safari yake.
USHAURI
Dada zetu hasa wale warembo na wasomi (maana hawa walioko vyuoni ndiyo wanajiona wamesoma kuliko watu wengine ) kuweni na nidhamu kwa kila mtu. Huwezi kudharau wanaume kwasababu labda ni wasumbufu, au kwa vile wanatumia magari bila kuwa na funguo za magari hayo (daladala). Heshima ni muhimu kwa kila mtu na dharau hazifai, sasa ona leso langu chafu lilivyomuokoa huyu mrembo, Badilike jamani .
Kindikwili