Huyu dada anaroho ngumu sana

NATA

JF-Expert Member
May 10, 2007
4,492
1,311
Anabwana kazaa naye.
Amelazimisha kuhamia kwa bwana, anakaa chumba cha wageni. Bwana hamhusishi kwa lolote ndani ya nyumba na sasa bwana katembea na house girl wa huyo dada kampa mimba.

Bado huyu mdada ameng`ang`ania huko ndani. Sijui asaidiwe vipi maana huyo bwana ni mwisho wa matatizo.

Na dada nimrembo na anakazi bomba kabisa!
 
amefungwa pingu huko ndani? Au ndo kutaka ushahidi/sifa kuwa anaishi na mwanaume!
 
Mrembo ila hajiamini....

Hivi haya maisha ni ya kujing'ang'aniza kwa mwanaume baradhuli kama huyo? Huyo mdada ana lake jambo sina hakika ni kupenda.
 
Mrembo ila hajiamini....

hivi haya maisha ni ya kujing'ang'aniza kwa mwanaume baradhuli kama huyo? Huyo mdada ana lake jambo sina hakika ni kupenda.

Tatizo liko hapo kwenye bold. Kajifunga mwenyewe na bado hajaona vituko vya huyo bwana. Atajutaje?!
 
amefungwa pingu huko ndani? Au ndo kutaka ushahidi/sifa kuwa anaishi na mwanaume!
Lol, hivi kuishi na mwanaume kumbe nayo ni sifa eeh? Subiri anyongwe huko ndani ndio atajua kuwa sifa zina faida na hasara.
 
Lol, hivi kuishi na mwanaume kumbe nayo ni sifa eeh? Subiri anyongwe huko ndani ndio atajua kuwa sifa zina faida na hasara.

Si ndo hapo! Inawezekana yeye anaona sifa! Kumezuka tabia ya wadada wengi kung'ang'ania wanaume ilhal hawana ndoa! Wanavumilia weee wakija kushtuka mambo yameharibika
 
Ana shida ya kichwa,je uliwahi kuongea nae ujue kinachomshikilia humo ndani ni nini?

Nalisha ongea naye sana,rafiki zake walishaongea naye sana, tena kwa mapana na marefu .Lakini wamechemsha ameng`nga`na huyu mrembo...
 
Mke mwenza,huyo dada anajiamini sana kuliko mimi na wewe. Sema anajiamini kwenye sekta tafauti.
Kupanga ni kuchagua. Labda ana strategy yake, wanasema anaecheka wa mwisho kuna mawili, haelewi haraka ama ndo atacheka kwa muda zaidi!

Mtoa mada,nifikishie pongezi kwa huyo dada

Mrembo ila hajiamini....

hivi haya maisha ni ya kujing'ang'aniza kwa mwanaume baradhuli kama huyo? Huyo mdada ana lake jambo sina hakika ni kupenda.
 
Mke mwenza,huyo dada anajiamini sana kuliko mimi na wewe. Sema anajiamini kwenye sekta tafauti.
Kupanga ni kuchagua. Labda ana strategy yake, wanasema anaecheka wa mwisho kuna mawili, haelewi haraka ama ndo atacheka kwa muda zaidi!
Mtoa mada,nifikishie pongezi kwa huyo dada
Hahaha! Sante mke mwenza, mie hapa sina cha kuongeza!..lol.

Kumbe ndio mana na wewe umejing'ang'aniza kwa kakake ashadii eeh? Unipe hiyo siri mwenzio manake mie nna moyo mwepesi kupita maelezo.
 
mke mwenza,huyo dada anajiamini sana kuliko mimi na wewe. Sema anajiamini kwenye sekta tafauti.
Kupanga ni kuchagua. Labda ana strategy yake, wanasema anaecheka wa mwisho kuna mawili, haelewi haraka ama ndo atacheka kwa muda zaidi!
Mtoa mada,nifikishie pongezi kwa huyo dada

zimefika kaka
 
anaonyesha ana maamuzi mazito na anaelewa nini afanyalo
 
Yaani hapa kuna mawili nshasema, either nitacheka for the rest of my life, or kichwa yangu haifikirii haraka na kuna siku ntazinduka. Tuombe Mungu isiwe hilo la kwanza. Manake unajua hakuna gumu zaidi ya wakati ww umemaliza kucheka, unaanza kulia mwenzio ndo anacheka.

Hivi unajua kuna mambo huwezi kumshauri mtu? Unashauri the obvious?

Hahaha! Sante mke mwenza, mie hapa sina cha kuongeza!..lol.
Kumbe ndio mana na wewe umejing'ang'aniza kwa kakake ashadii eeh? Unipe hiyo siri mwenzio manake mie nna moyo mwepesi kupita maelezo.
 
elimu na kazi yake hazijamkomboa anaona huyo jamaa ndo mkomboazi wake
 
Anabwana kazaa naye.
Amelazimisha kuhamia kwa bwana,
Anakaa chumba cha wageni,
Bwana hamhusishi kwa lolote ndani ya nyumba na sasa bwana katembea na house girl wa huyo dada kampa mimba.
Bado huyu mdada ameng`ang`ania huko ndani.
Sijui asaidiwe vipi maana huyo bwana ni mwisho wa matatizo.

Na dada nimrembo na anakazi bomba kabisa!

kweli ana roho ya kipekee...ngumu imepitiliza iyooo.....atasaidiwaje kama hajataka kuanza kujisaidia.....ni kumpa pole afu unamwambia wanaume ndo walivogo we vumilia tuu ipo siku atabadilika...sababu wanawake wengi tunajipaga matumaini ambayo hayapogo...
 
Back
Top Bottom