Uchaguzi 2020 Huyu bwana michoro yake imepinda!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,214
56,855
Wala haitaji kutumia akili kubwa sana kumjua mchoraji mahili na mchoraji asie mahili.

Kama utakuwa ni mtu mwenye fikra pana na uonaji sahihi hakika utaona mchoro wake UMEPINDA!

Anataka aonekane yeye ni mchoraji makini kushinda waliopita huko ni kujitakia sifa ambazo hana na ni sifa hizohizo ndizo zinazomuangusha na kuzidi kupindisha mchoro wake dhahiri! Hakuanza leo wala jana tena alianza kwa maigizo yaliyovuta hisia watu,hakuishia hapo kwenye maigizo bali akaanza pia kufuta walipochora wengine akidai palikosewa kumbe yeye ndo anakosea na wala hajui.

Anachokifanya anazidisha yale makosa machache kuwa mengi! Na katika uchoraji wake anaiamini miwani yake ambayo hajui kuwa inamtoa nje ya mchoro.

Mchoraji anataka kuaminisha wacholewa kuwa mchoro anaouchora hivi sasa ndio mchoro unaotakiwa na ati wengi wamerudisha imani zaidi katika mchoro huo!

Hivi ni mchoro upi makini wenye kuchorwa kwa nguvu pasipo kutumia akili,na mchoro huo ukawa mchoro mzuri na halali?

Isitoshe hata zana za mchoro hazitumii ipasavyo! Panapotakiwa penseli yeye anachorea pen! Panapotakiwa rangi nyeusi ye anaweka njano!, kwenye blue anaweka kijani na alivyo mpenda sifa kaweka na rangi nyekundu ambapo ktk mchoro huo hapakutakiwa rangi hiyo!

Kaamua kuwafata wanaomshangilia na kuwaumiza ambao wanalia! Tena kawapa na jina wanaolia kawaita "wachoraji wa nje" mchoraji huyu anajikosesha Kisha anafuta halafu anasema Kuna mchoraji alichora vibaya Kisha anachora yeye tena!.. lkn haachi hivihivi ktk kurudia michoro yake huwatoa kafara wajakazi wake wadogowadogo.

Mchoraji huyu asipokanywa basi mchoro wake atauharibu zaidi maana mpk sahivi kauharibu nusu! Na kwajinsi asivyoelewa nusu iliyobaki ataizongorota si kifani! Na mumuambia walikuwepo wachoraji wazuri zaidi yake nao wamepita. Walikuwepo wachapa rangi wazuri zaidi yake nao wamepita! Kila anachokiona kitapita na ataviacha Sasa ni jukumu lake kuache vyema kuliko kuacha vibaya maana siku zote mwisho wa ubaya ni ubaya.
 
IMG_5791.png
 
Mtakuwa waimba taarabu, mipasho na mafumbo mpaka mtakapo jipanga vzr kwa ajili ya uchaguzi wa 2025
 
Japo mataga hawapendi kabisa kusikia mambo yao ...ila kwa kiasi fulani nimekusoma between the lines nikang'amua jambo fulani the hidden meaning
 
Mtakuwa waimba taarabu, mipasho na mafumbo mpaka mtakapo jipanga vzr kwa ajili ya uchaguzi wa 2025
Tume huru,mtaikubali?,wajipange Vipi tena wakati walishaenda mpaka mahakamani kupinga wakurugenzi kuwa wasimamizi Wa uchaguzi na wakashinda kesi,srrikari kwa kupitia Wakili wake wakapinga mahakama ya rufaa,maagizo yakatoka juu wakarudishwa.
CCM chama cha mafisi.
 
karatasi aliyotumia kuchora nayo si yenyewe haiewezi kuakisi mchoro vizuri.Picha kaipaka rangi zisozo muafaka,picha imekuwa kama zombi hata mtoto mdogo akiona itamtisha na kumuwekea kumbukumbu mbaya maishani,picha inaonekana ni jinamizi baya sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom