Huyu Babu wa Loliondo mnamwonaje?

Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:22 Shija Felician, Igunga
WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.

Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... "Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?"

Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.

Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.

Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.

Comments

0 #4 elibariki yerald 2011-03-16 05:34 Quoting Singala-Ch- Vietnam:
Ni vigumu kupinga au kuunga mkono. Masuala ya kiimani mtu anapona kama ana amini. Hata pale hospitali wapo watu wanapata dawa lakini wale ambao hawamwamini daktari hupona wadudu lakini hubakiwa na magonjwa yao. "Nimetibiwa lakini yule daktari sijui kama ameniandikia dawa sahihi, si unajua wanataka hela" wagonjwa wa aina hii hubakiwa na magonjwa yao ya saikolojia.
Vipofu wawili walimwendea Yesu: "Tadhali Bwana tuonee huruma,utuponye " akawauliza: "Je mnaamini naweza kufanya hilo?" wakajibu "ndiyo Bwana tunaamini" Yesu akawaponya. Wapo wasiokuwa na imani walibaki na ukoma wao, kisukari chao nk...​

pia si hvyo tu hata wale 10 wenye ukoma aliowaponya mmoja wao alirudi kushukuru akaponywa je, hao anaosema huyu fidadi walishukuru au walikwenda pale kudhihaki tuu ile dawaaaaaaaaaaaa aa?
Quote

0 #3 elibariki yerald 2011-03-16 05:32 suala ni imani na si kufanya mzaha kama hauamini hwezi pona na babua alishasema kama ulikuwa unafanya matendo machafu uyaache,,ukiend elea nayo hutapona maana Mungu hapendi wenye kiburi bali watiifu wa moyo ....wewe fisadi mkubwaaaaaaaaaa aaaaaa.
Quote

0 #2 Mhifadhi 2011-03-16 05:09 Asante baba kwa laki tano tano naona tutakupa tena kura next time
Quote

+1 #1 Singala-Ch- Vietnam 2011-03-16 02:47 Ni vigumu kupinga au kuunga mkono. Masuala ya kiimani mtu anapona kama ana amini. Hata pale hospitali wapo watu wanapata dawa lakini wale ambao hawamwamini daktari hupona wadudu lakini hubakiwa na magonjwa yao. "Nimetibiwa lakini yule daktari sijui kama ameniandikia dawa sahihi, si unajua wanataka hela" wagonjwa wa aina hii hubakiwa na magonjwa yao ya saikolojia.
Vipofu wawili walimwendea Yesu: "Tadhali Bwana tuonee huruma,utuponye " akawauliza: "Je mnaamini naweza kufanya hilo?" wakajibu "ndiyo Bwana tunaamini" Yesu akawaponya. Wapo wasiokuwa na imani walibaki na ukoma wao, kisukari chao nk...
Quote
 
PHP:
My dia hiki ni  kitendawili kikubwa sana, mie naamini kweli babu anaponya!!! ngoja  nijikusanye nami nikamuone ila tatizo langu ni low pressure hope  nitapona!

My love unapoona Lowassa na swahiba wake mkuu wanatofautiana kwenye hili huyu Rostam Aziz ujue hili sasa ni fumbo kubwa........................
 
kweli ni fumbo, ngoja nasi tukikusanye tukapate kikombe
 
Mchungaji Loliondo amnusuru Kikwete
• Askofu Laizer atangaza kumrejesha kwenye uchungaji

na David Frank na Chalila Kibuda

amka2.gif
KUIBUKA kwa tiba ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwaisapile wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kumeleta ahueni kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Ahueni hiyo imetokana na vyombo vingi vya habari, masikio na macho ya Watanzania kuelekezwa kwa Mchungaji Mwaisapile anayetoa tiba ya maajabu kutibu maradhi sugu ya ukimwi, kisukari, shinikizo la damu, saratani na mengine; na kuacha kujadili mambo ya msingi yanayolikabili taifa kwa sasa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wiki moja sasa, umebaini kuwa tangu kuanza kwa tiba hiyo ya maajabu, maelfu ya wananchi wamekuwa wakijadili tiba hiyo na kuweka kando mambo ya siasa na hivyo kuipa ahueni serikali ya CCM, inayoongozwa na Rais Kikwete iliyokuwa ikiandamwa kwa kashfa mbalimbali za ufisadi, kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi na kusababisha kupanda mara dufu kwa gharama za maisha.
Mambo yaliyowekwa kando tangu kuibuka kwa tiba hiyo ni pamoja na suala la malipo ya kampuni ya kufua umeme wa dharula ya Dowans ambalo limekuwa mwiba mkali kwa serikali ya Kikwete tangu Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC), ilipotoa hukumu ya kulitaka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuilipa Dowans fidia ya sh bilioni 94 kwa madai ya kuvunja mkataba.
Mambo mengine yaliyofunikwa na tiba ya Loliondo ni sakata la umeya na mauaji ya watu watatu mkoani Arusha, milipuko ya mabomu iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 20, kupanda kwa gharama za bidhaa na huduma mbalimbali kama umeme, nauli za mabasi ya mikoani na daladala jijini Dar es Salaam.
Presha ya Rais Kikwete na viongozi wake juu ya matatizo yanayolikabili taifa, ilizidi kuongezeka baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuamua kufanya maandamano na mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuelimisha jamii juu ya matatizo yanayolikabili taifa.
Katika hotuba yake ya mwezi uliopita, Rais Kikwete katika utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kila mwezi, alitumia muda mwingi kukilaumu CHADEMA kwamba kinatumia matatizo yanayolikabili taifa kufanya uchochezi.
Mawaziri kadhaa pamoja na makada mbalimbali nao walijitokeza kuunga mkono hutuba ya Rais Kikwete na kuvitaka vyombo vya dola vitumike kuwathibiti viongozi wa CHADEMA.
Wakizungumzia kunusurika kwa serikali, wanaharakati na mwanasiasa maarufu, Seneta Misellya, alisema hakuna ubishi kwamba tiba ya Mchungaji wa Loliondo imepunguza presha kwa Rais Kikwete na serikali yake.
"Lakini binafsi nawabebesha lawama waandishi wa habari kwamba wanapaswa kujua matatizo ya msingi ya taifa hili na mchango mkubwa wa kulisaidia taifa. Tatizo letu sio Loliondo, tunajua umuhimu wa tiba ya Loliondo, lakini kamwe msisahau matatizo yetu ya msingi," alisema Misellya.
Katika hatua nyingine, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini limemrejesha kundini Mchungaji Mwasapila kwa kumpa ajira mpya licha ya kustaafu miaka minne iliyopita.
Uamuzi wa kumwajiri upya mchungaji huyo ambapo atapata mshahara sawa na wachungaji wengine pamoja na stahili mbalimbali za kichungaji ulifikiwa hivi karibuni na kutangazwa rasmi na Baba Askofu wa Kanisa hilo, Thomas Laizer, huko kijijini Samunge alipokwenda kumtembelea.
Awali Mchungaji Mwaisapila alifikia umri wa kustaafu baada ya kulitumikia kanisa hilo katika maeneo tofauti.
Amepata kufanyakazi ya utumishi katika Ushariki wa mjini Babati, mkoani Manyara, kwa miaka saba kabla ya kuhamia Usharika wa Sonjo alikofanya kazi kwa miaka 12 kabla ya kustaafu rasmi.
Habari toka ndani ya dayosisi hiyo zilizothibitishwa na Askofu Laizer, zilisema kuwa uamuzi wa kumwajiri upya ulifikiwa na kutangazwa kijijini hapo hivi karibuni baada ya mchungaji huyo kudai kuoteshwa kutoa tiba hiyo.
Akithibitisha hatua hiyo, Askofu Laizer alisema baada ya kutafakari kwa makini, kanisa limeona busara kumrejesha mchungaji huyo kwani kazi aliyopewa na Mungu ya kuwatumikia watu ni kubwa kuliko uchungaji.
Alisema Mchungaji Mwaisapile ambaye amepata umaarufu kutokana na kutoa tiba hiyo, atafanya kazi zake katika kituo cha Usharika cha Sonjo, mahala alipo sasa.
"Ni kweli tumefikia uamuzi wa kumwajiri upya mchungaji Ambilikile na atalipwa mshahara na kupata stahili wanazopata wachungaji wengine na tayari nimeshamwagiza Katibu Mkuu wa KKKT Israel Kariyongi kushughulikia masuala ya ajira yake yafanyike mapema iwezekanavyo," alisema Askofu Laizer.
"Na zaidi atakuwa katika kituo cha Usharika wa Sonjo na pale anaendelea na ujenzi wa nyumba yake na sisi kama kanisa tutatoa msaada wa hali na mali ili ujenzi huo umalizike haraka," alisisitiza Askofu.
Alisema mchungaji huyo ameridhia uamuzi wa kanisa na kuahidi kutoa ushirikiano katika kulijenga kanisa na kumtumikia Mungu.
Habari zaidi kutoka Loliondo zinasema mchungaji huyo aliyezaliwa Rungwe, mkoani Mbeya, hivi sasa anatoa huduma kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa tatu usiku kila siku na wagonjwa wanapewa tiba wakiwa ndani ya magari yao na kuondoka, hali ambayo imepunguza msongamano kwa kiasi kikubwa.
Lakini pia kupatikana kwa huduma mbalimbali muhimu katika eneo hilo kama chakula, vinywaji, sehemu ya malazi na vyoo, kumechangia kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaokwenda kupata dawa kwa mchungaji huyo, maarufu kwa jina la Babu.
Pamoja na uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kutoa agizo la kuzuia magari yasiingie ili kuwaruhusu waliotanguliwa watoke, agizo hilo limepuuzwa na badala yake ulinzi umeimarishwa.
Baadhi ya watu walizungumza katika kijiji hicho chenye kaya zinazokadiriwa kufikia 500, wametoa wito kwa kampuni za simu za mkononi kupeleka minara ya mawasiliano japo ya muda ili kuondoa tatizo la mawasiliano.
Kwa nauli ya kwenda na kurudia katika kijiji cha Samunge kwa magari aina mbalimbali imeshuka kutoka sh 150,000 na 180,000 kwa Land Cruiser na kufikia sh 100,000 hadi 120,000, huku mabasi yakitoza sh 70,000 na 80,000.
Wakati huo huo, watu 80 waliokuwa wakisafiri kutoka Arusha kwenda Loliondo kwa Babu, wametelekezwa wakati tayari walishalipa nauli ya 55,000 kila mmoja.
Kutokana na utapeli hiyo, wananchi wameonywa kuwa makini na wasafirishaji wa aina hiyo ya utapeli.
Loliondo yapandisha nauli Dar, Arusha
Nauli ya usafiri wa mabasi kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Arusha, imeongezeka kutoka sh 20,000 hadi sh 40,000.
Baadhi ya abiria waliliambia gazeti hili jana kuwa kupanda kwa gharama hizo kumesababisha baadhi ya wagonjwa kushindwa kusafiri kwenda kupata tiba Loliondo.
Mmoja wa abiria hao, Zainabu Alli alisema hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri wanaokwenda Loliondo.
 
Mwingira amlaani mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:32

Elizabeth Suleyman
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. "Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.

"Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,"alisema Mwingira.

Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. "Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.
Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka," alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.
"Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,"alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

"Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira. Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion' na baade ikaleta madhara."

Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

Pengo alisema: "Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion' na baadae watu wakapata madhara makubwa.

"Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,"alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.

Comments

123

0 #44 jojas brand 2011-03-16 10:01 Nabi na Mtume.Ninaomba sana kwa maana hujuwi ulitendalo.Hiyo ni hofu yako,je?hizo of Money unazozipata na kuzila hizo hela unamhubiria shetani?Ni heri aliekubali kuchukua mia kuliko wewe.
Hifi ni hofu ya kukimbiwa na waumini wako baada ya kupona
Quote

0 #43 Neema Linke 2011-03-16 10:00 Mimi ninamuunga mkono Mwingira kuhusu huyo Babu ninapinga tiba zake na nunabii wake mungu ajamwelekeza wala hajamuotesha
lolote kuhusu kutibu watu,kinacho fanyika
kwa Baba ni Shetani ana mtumia anamutumia
Baba kuteka roho za watu ktk ulimwengu roho.ktkt Bibulia imeandikwa yakwamba Shetani ujigeuza anakujifanya kuwa kama malaika wa Nuru,mimi ninamkemea Baba kwa
jina la Yesu Kristo wa Anazaret ashindwe
Baba kadanganywa na Shetani.Hapo ktk dawa
zake hakuna nguvu za Mungu.Mtu akitaka kuponywa magonjwa yake ansome Bibulia
kuna ahadi ya uponyaji Isaya 53:3-5
Quote

0 #42 Mhifadhi 2011-03-16 09:58 Quoting Jesus is Lord God:
simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?

Please hata kama Mwingira ana mapungufu (kitu ambacho sio suala la msingi hapa), tujadili alichosema. Hata mlevi akikuonya, utakuwa makini kuchambua anachosema na si aliyesema, kwa kuwa main issue hapa ni kama Mungu wa Biblia ndiye anayetenda kazi na Babu Mwasapile.
Shalom!​

Kili[NENO BAYA] mezani ni lile lililo zito. Swala la mtumishi mkuu mwema nabii mtume kuanza kuro po ka na kumwaga laana ni kubwa zaidi ya unayotetea ya kutokuwepo biblia n.k. Swala la hivyo vingine hakutupa uthibitisho ila ktk laana tumeona akituthibitishi a anavyojua kulaanai. Katika vitabu vitukufu watu hawa wamekuwepo tangu hapo kale na walikuwa wakijipendekeza kwa wafalme ili waonekane wao ndio basi. Wafalme wa siku hizi ni watu walio na hela na utaona manabii hawa wa uongo wakijipendekeza kwao. Mwache babu atumie anachotaka kutumia ili mradi waendao kule wanaimani wanaponywa. Mbona hatumsikii huyu nabii akiwalaani waganga? kama angekuwa anakemea ya ukweli miaka yote anapowalaghai watu basi leo kungekuwa hakuna uchawi wala mganga bongo na kila mtu anagekuwa akiishi maisha safi. THis is actually a downfall of mr. nabii mkuu mtumishi mtume na ukishaanza kuelekea kwenye downfall huwa hakuna turning back. Umewaonea sana waumini wako na kusababisha vifo bila sababu kwa kuwadanganyia maombezi bila dawa
Quote

0 #41 Ankali 2011-03-16 09:52 Kama unabii ni kutoa mapepo sielewi. Kakobe amelaani,laana haijafika, Kama Mwingira ni nabii wa kweli mbona hakuliona suala la mchungaji kabla halijatokea? Paulo (Saulo) alipoi[NENO BAYA] utume hakuwa mfuasi bali mtesi wa mitume wakati huo. Wasifikiri tunategemea uponyaji utoke kwa hao manabii uchwara. Mungu ana njia yake ya ajabu kuteua watu wake.
Quote

0 #40 The Matokeoism 2011-03-16 09:50 NGASTUKAA! KUMBE DINI NI SIASAA?
lol.gif

wengine wanabariki, wengine wanalaani,
jamani mbona mwatuchanganya, au kuna nini?
jamani viongoz w Mungu kaeni chini mtafakari ukweli kisha muangalie namna ya kumtangaza Kristu la mtaganyika, wakatoliki kwa waliteri, wpentekoste kw waaswmbly.
JAMANI MAMBO YA DINI ME SIMOOOOOOOOOOOO !
Quote

0 #39 Bernard 2011-03-16 09:47 Mwingira hacha unafiki wewe ukihubiri hautaji sadaka?kwanini unauza neno la Bwana?huyu babu kasimamisha shuguli zake zote ambazo zingemuingizia mapato kwa ajili ya kutibu watu.Nini mia tano anayotoza!!!
Quote

0 #38 Ruakia 2011-03-16 09:39 Huyu mtuu anaye jiita nabii anawaza nini? huyu mzee anayetoa tiba ni kama bure kulinganisha na bei yenyewe, na pia watu wanao kwenda kuchimba dawa na bili ya maji na kuni vyote hivyo anapewa bureeeeee! tuwaze kabla yakusema
Quote

0 #37 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:32 Jamani NGIWIRA asifuatwe ni mshenzi tu huyo sio nabii
Quote

0 #36 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:30 Mitume yote na Manabii wote wametajwa katika Vitabu vitukufu.
Hivi hawa mitume na manabii Josephat Mwingira anatokea wapi.
Huyu ni muongo na watu wasimsikilize bali waende kutafuta tiba.
Quote

+1 #35 paulsen shijah 2011-03-16 09:30 Haya sasa ni Majungu, Wewe mwingira kama kweli we ni mtumishi wa Mungu huwez kumuombea mabaya babu wa loliondo, kinachokusumbua wewe ni hiyo sh. 500 anayotoza? Au ni wasiwasi wa kukimbiwa na wumin!, hayo unayoyaomba yampate babu sio mazuri na hayana tofauti na arbadri, Wkristo tumeagizwa kuwapenda adui zetu na kuwaombea wale wote wa
naotuudhi, wewe umefanya lipi?, na ndio unajiita Mtume na Nabii, je!?, Kazi ya Mtume na Nabii ni Kulaani na Kuombea mabaya?, huduma zenu wenyewe haziaminiki, zimekuwa za kinafiki, kwenu mtu akipata uponyaji nilazima abaki kanisani kwenu lakin hatujasikia babu akilazimisha mtu abaki KKKT, unaponywa unaenda zako, sasa tatizo liko wapi?, lakin kwenu mnaponya na kuwaomba Pesa nyingi tu!, eti kwa Kisingizio cha Kumtolea Bwana Shukrani, mie nawomba kabla hamjatoa maoni au kupinga kitu ni vyema kuchunguza kwanza kuliko kuropoka ukaonekana kituko mbele ya jamii, kauli hiyo ya kulaani iko tofauti sana na Mafundisho ya Kiongozi wa Ukristo, YESU KRISTO mwenyewe, ni bora ungemuomba mungu akakufunulia kujua kama huduma hiyo inatoka kwake na sio kutoa maneno ya kukashifu na kulaan.
Kaka Mwingira wewe unaejiita Mtume na Nabii, Toa Kwanza Boriti lilomo ndani ya Jicho lako kabla hujatoa kibanzi ndani ya Jicho la Mwenzako.

Tuache unafiki tuseme kweli nayo kweli itatuweka huru,
Am Out.
Quote

0 #34 Jesus is Lord God 2011-03-16 09:25 simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?

Shalom!
Quote

+1 #33 miriam 2011-03-16 09:21 wewe mtumishi nasikitisikitik a sana kwani mbona huduma yako pia inasikika haitoki kwa mungu unakwenda kupokea kwa mfalme wa giza mnapigana vikumbo na watu wa ulimwengu wa giza unafikiri ni kila mtu anakuamini?????? WEWE WATU WANAJUA VITU UNAVYOTUMIA KUVUTA WATU HUNA CHA INJILI ILA BIASHARA TU HAPO.
Quote

+1 #32 Kabigi 2011-03-16 09:18 Mwingira, Hivi wewe ni mtume kweli???Umepewa wapi mamlaka ya kulaani?Anayelaani ni Mungu si wewe.Ninamashaka na unabii wako.Mungu amesema tuombeane mema mbona wewe unayejiita nabii humuombei mema mtumishi mwenzako?Au kwasababu anatoa tiba sawa na bure?Au kwasababu Mungu amemuinue yeye na si wewe?Acha wivu bwana.Acha Mungu aliyemuumba amtumie kama apendavyo yeye na si wewe.Au ulitaka aje kanisani kwako ndo uamini Mungu amempa maono?Umetuboa na Si kuamini tena kama mtume kweli
Quote

0 #31 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:16 Jamani MWINGIRA anaonekana kama mtu asiye na busara hata kidogo na anaonekana kama mtu mwenye choyo kikubwa kwa sababu anaona kwa nini miujiza hii amepewa Mchungaji Mwasapile na hakupewa yeye.
Hivyo jamani Mwingire ni mtu mbaya na hafai katika jamii yetu kufuatwa kwani watu wanaonekana kupona.
Quote

0 #30 JOHN 2011-03-16 09:14 Jamani ninawaomba katu msipotoshe na matapeli wanaojiita ati ni Manabii, huo ni u[NENO BAYA]. Kwani yeye na familia yake anakula nini kama si kuwatapeli waumini wenye IMANI na dini yao. [NENO BAYA]IIIIIII.
Quote

123
 
Mwingira amlaani mchungaji Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 21:32

Elizabeth Suleyman
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. “Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.

“Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,”alisema Mwingira.

Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. “Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.
Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka,” alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.
“Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,”alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

“Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira. Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara."

Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

Pengo alisema: “Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion’ na baadae watu wakapata madhara makubwa.

“Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,”alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.

Comments

123

0 #44 jojas brand 2011-03-16 10:01 Nabi na Mtume.Ninaomba sana kwa maana hujuwi ulitendalo.Hiyo ni hofu yako,je?hizo of Money unazozipata na kuzila hizo hela unamhubiria shetani?Ni heri aliekubali kuchukua mia kuliko wewe.
Hifi ni hofu ya kukimbiwa na waumini wako baada ya kupona
Quote

0 #43 Neema Linke 2011-03-16 10:00 Mimi ninamuunga mkono Mwingira kuhusu huyo Babu ninapinga tiba zake na nunabii wake mungu ajamwelekeza wala hajamuotesha
lolote kuhusu kutibu watu,kinacho fanyika
kwa Baba ni Shetani ana mtumia anamutumia
Baba kuteka roho za watu ktk ulimwengu roho.ktkt Bibulia imeandikwa yakwamba Shetani ujigeuza anakujifanya kuwa kama malaika wa Nuru,mimi ninamkemea Baba kwa
jina la Yesu Kristo wa Anazaret ashindwe
Baba kadanganywa na Shetani.Hapo ktk dawa
zake hakuna nguvu za Mungu.Mtu akitaka kuponywa magonjwa yake ansome Bibulia
kuna ahadi ya uponyaji Isaya 53:3-5
Quote

0 #42 Mhifadhi 2011-03-16 09:58 Quoting Jesus is Lord God:
simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?

Please hata kama Mwingira ana mapungufu (kitu ambacho sio suala la msingi hapa), tujadili alichosema. Hata mlevi akikuonya, utakuwa makini kuchambua anachosema na si aliyesema, kwa kuwa main issue hapa ni kama Mungu wa Biblia ndiye anayetenda kazi na Babu Mwasapile.
Shalom!​
Kili[NENO BAYA] mezani ni lile lililo zito. Swala la mtumishi mkuu mwema nabii mtume kuanza kuro po ka na kumwaga laana ni kubwa zaidi ya unayotetea ya kutokuwepo biblia n.k. Swala la hivyo vingine hakutupa uthibitisho ila ktk laana tumeona akituthibitishi a anavyojua kulaanai. Katika vitabu vitukufu watu hawa wamekuwepo tangu hapo kale na walikuwa wakijipendekeza kwa wafalme ili waonekane wao ndio basi. Wafalme wa siku hizi ni watu walio na hela na utaona manabii hawa wa uongo wakijipendekeza kwao. Mwache babu atumie anachotaka kutumia ili mradi waendao kule wanaimani wanaponywa. Mbona hatumsikii huyu nabii akiwalaani waganga? kama angekuwa anakemea ya ukweli miaka yote anapowalaghai watu basi leo kungekuwa hakuna uchawi wala mganga bongo na kila mtu anagekuwa akiishi maisha safi. THis is actually a downfall of mr. nabii mkuu mtumishi mtume na ukishaanza kuelekea kwenye downfall huwa hakuna turning back. Umewaonea sana waumini wako na kusababisha vifo bila sababu kwa kuwadanganyia maombezi bila dawa
Quote

0 #41 Ankali 2011-03-16 09:52 Kama unabii ni kutoa mapepo sielewi. Kakobe amelaani,laana haijafika, Kama Mwingira ni nabii wa kweli mbona hakuliona suala la mchungaji kabla halijatokea? Paulo (Saulo) alipoi[NENO BAYA] utume hakuwa mfuasi bali mtesi wa mitume wakati huo. Wasifikiri tunategemea uponyaji utoke kwa hao manabii uchwara. Mungu ana njia yake ya ajabu kuteua watu wake.
Quote

0 #40 The Matokeoism 2011-03-16 09:50 NGASTUKAA! KUMBE DINI NI SIASAA?
lol.gif

wengine wanabariki, wengine wanalaani,
jamani mbona mwatuchanganya, au kuna nini?
jamani viongoz w Mungu kaeni chini mtafakari ukweli kisha muangalie namna ya kumtangaza Kristu la mtaganyika, wakatoliki kwa waliteri, wpentekoste kw waaswmbly.
JAMANI MAMBO YA DINI ME SIMOOOOOOOOOOOO !
Quote

0 #39 Bernard 2011-03-16 09:47 Mwingira hacha unafiki wewe ukihubiri hautaji sadaka?kwanini unauza neno la Bwana?huyu babu kasimamisha shuguli zake zote ambazo zingemuingizia mapato kwa ajili ya kutibu watu.Nini mia tano anayotoza!!!
Quote

0 #38 Ruakia 2011-03-16 09:39 Huyu mtuu anaye jiita nabii anawaza nini? huyu mzee anayetoa tiba ni kama bure kulinganisha na bei yenyewe, na pia watu wanao kwenda kuchimba dawa na bili ya maji na kuni vyote hivyo anapewa bureeeeee! tuwaze kabla yakusema
Quote

0 #37 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:32 Jamani NGIWIRA asifuatwe ni mshenzi tu huyo sio nabii
Quote

0 #36 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:30 Mitume yote na Manabii wote wametajwa katika Vitabu vitukufu.
Hivi hawa mitume na manabii Josephat Mwingira anatokea wapi.
Huyu ni muongo na watu wasimsikilize bali waende kutafuta tiba.
Quote

+1 #35 paulsen shijah 2011-03-16 09:30 Haya sasa ni Majungu, Wewe mwingira kama kweli we ni mtumishi wa Mungu huwez kumuombea mabaya babu wa loliondo, kinachokusumbua wewe ni hiyo sh. 500 anayotoza? Au ni wasiwasi wa kukimbiwa na wumin!, hayo unayoyaomba yampate babu sio mazuri na hayana tofauti na arbadri, Wkristo tumeagizwa kuwapenda adui zetu na kuwaombea wale wote wa
naotuudhi, wewe umefanya lipi?, na ndio unajiita Mtume na Nabii, je!?, Kazi ya Mtume na Nabii ni Kulaani na Kuombea mabaya?, huduma zenu wenyewe haziaminiki, zimekuwa za kinafiki, kwenu mtu akipata uponyaji nilazima abaki kanisani kwenu lakin hatujasikia babu akilazimisha mtu abaki KKKT, unaponywa unaenda zako, sasa tatizo liko wapi?, lakin kwenu mnaponya na kuwaomba Pesa nyingi tu!, eti kwa Kisingizio cha Kumtolea Bwana Shukrani, mie nawomba kabla hamjatoa maoni au kupinga kitu ni vyema kuchunguza kwanza kuliko kuropoka ukaonekana kituko mbele ya jamii, kauli hiyo ya kulaani iko tofauti sana na Mafundisho ya Kiongozi wa Ukristo, YESU KRISTO mwenyewe, ni bora ungemuomba mungu akakufunulia kujua kama huduma hiyo inatoka kwake na sio kutoa maneno ya kukashifu na kulaan.
Kaka Mwingira wewe unaejiita Mtume na Nabii, Toa Kwanza Boriti lilomo ndani ya Jicho lako kabla hujatoa kibanzi ndani ya Jicho la Mwenzako.

Tuache unafiki tuseme kweli nayo kweli itatuweka huru,
Am Out.
Quote

0 #34 Jesus is Lord God 2011-03-16 09:25 simtetei yeyote lakini mbona mnajibu mkiwa mmejaa emotionalism? Has someone shot sacred cow somehwere, mh? Kuna maswali mwingira ameuliza nilitarajia wachangiaji wayajadili lakini yamekuwa totally ignored, badala yake wanamshambulia yeye binafsi na si hoja alizoweka. Kwa nini kwa Babu Jina la Yesu halitajwi, Biblia haitumiki, watu hawahubiriwi?

Please hata kama Mwingira ana mapungufu (kitu ambacho sio suala la msingi hapa), tujadili alichosema. Hata mlevi akikuonya, utakuwa makini kuchambua anachosema na si aliyesema, kwa kuwa main issue hapa ni kama Mungu wa Biblia ndiye anayetenda kazi na Babu Mwasapile.
Shalom!
Quote

+1 #33 miriam 2011-03-16 09:21 wewe mtumishi nasikitisikitik a sana kwani mbona huduma yako pia inasikika haitoki kwa mungu unakwenda kupokea kwa mfalme wa giza mnapigana vikumbo na watu wa ulimwengu wa giza unafikiri ni kila mtu anakuamini?????? WEWE WATU WANAJUA VITU UNAVYOTUMIA KUVUTA WATU HUNA CHA INJILI ILA BIASHARA TU HAPO.
Quote

+1 #32 Kabigi 2011-03-16 09:18 Mwingira, Hivi wewe ni mtume kweli???Umepewa wapi mamlaka ya kulaani?Anayelaani ni Mungu si wewe.Ninamashaka na unabii wako.Mungu amesema tuombeane mema mbona wewe unayejiita nabii humuombei mema mtumishi mwenzako?Au kwasababu anatoa tiba sawa na bure?Au kwasababu Mungu amemuinue yeye na si wewe?Acha wivu bwana.Acha Mungu aliyemuumba amtumie kama apendavyo yeye na si wewe.Au ulitaka aje kanisani kwako ndo uamini Mungu amempa maono?Umetuboa na Si kuamini tena kama mtume kweli
Quote

0 #31 Mohamed H. Mohamed 2011-03-16 09:16 Jamani MWINGIRA anaonekana kama mtu asiye na busara hata kidogo na anaonekana kama mtu mwenye choyo kikubwa kwa sababu anaona kwa nini miujiza hii amepewa Mchungaji Mwasapile na hakupewa yeye.
Hivyo jamani Mwingire ni mtu mbaya na hafai katika jamii yetu kufuatwa kwani watu wanaonekana kupona.
Quote

0 #30 JOHN 2011-03-16 09:14 Jamani ninawaomba katu msipotoshe na matapeli wanaojiita ati ni Manabii, huo ni u[NENO BAYA]. Kwani yeye na familia yake anakula nini kama si kuwatapeli waumini wenye IMANI na dini yao. [NENO BAYA]IIIIIII.
Quote

123
 
Lowassa apeleka watu kunywa dawa

*Akodi gari kila kata kwenda Loliondo
*Babu Mwaisapile arejeshwa kazini KKKT

Na Waandishi Wetu

WAKATI maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya Tanzania wakizidi kumiminika kupata dawa kwa Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwaisapile, Mbunge wa
Monduli, Bw. Edward Lowassa naye ametangaza kujitolea usafiri kupeleka watu jimbo lake Loliondo kupata tiba kwa mchungaji huyo.

Hatua hiyo imekuja wakati taarifa za karibuni zikianza kutoa ushuhuda wa watu mashuhuri na wale wa kawaida kuwa wamepona maradhi sugu yaliyokuwa yakiwasumbua, ukiwamo ukimwi, kisukari, saratani, shinikizo la damu na upungufu wa nguvu za kiume.

Bw. Lowassa aliyewahi kuwa Maziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, anakuwa mbunge wa pili kufanya hivyo baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Bw. Phillemon Ndesamburo kujitolea kufanya hivyo.

Taarifa zilizopatikana wilayani Monduli na kuthibitishwa na Bw. Lowassa, zinaeleza kuwa mbunge huyo alijitolea kuwapeleka watu hao kuanzia juzi, kwa kugharamia usafiri na mambo mengine kama maji ya kunywa.

Mmoja ya watu walipiga simu katika chumba cha habari cha Majira kwa masharti ya kutotajwa jina lake gazetini alisema ameamua kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe wa shukrani kwa Bw. Lowassa kwa kitendo hicho.

Alisema Bw. Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo aliamua kufanya hivyo baada ya watu wa jimbo hilo kuwa na nia ya kufika huko lakini hawakuwa na uwezo wa kufanya hivyo kutokana na gharama za usafiri kuwa juu.

Alisema watu wote wamekuwa wakijiandikisha katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na huduma hiyo imekuwa ikitolewa bila kuangalia itikadi za kichama katika kata 10 za Monduli, ingawa hata watu kutoka mjini Arusha walionekana kujiandisha ili kusafiri kwenda kwa 'Babu'.

"Ametoa gari moja kwa kila kata litakalowapeleka wakazi hao kupata dawa, hivi mimi nipo hapa nasubiri zamu yangu," alisema.

Akizungumzia suala hilo, Bw. Lowassa alikiri kufanya hivyo kwa lengo la kuwasadia watakaohitaji kwenda kunywa dawa hiyo.

"Ni kweli nimefanya hivyo kutokana kuwepo kwa vuguvugu la habari za kuwepo kwa mchungaji katika Kijiji cha Samunge kuwa anatoa dawa ya kutibu watu wa maradhi mbalimbali.

"Hivyo nimeamua kuwasadia lakini si pekee yangu, bali nasaidiana na wengine wanachangishana na kukodi magari ili kwenda huko kwa kuwa ni mbali. Jana (juzi) walikwenda watu 100 katika kijiji hicho leo tena (jana) wanandelea kujitokeza kujiandikisha," alisema.

Bw. Lowassa alisema ataendelea kutoa msaada huo kulingana na uwezo wake wa kifedha iwapo utahurusu katika siku zijazo.

Mwaisapile arudishwa kazini

Wakati Babu Mwasapile akizidi kuvuta watu, Kanisa lake la KKKT limemrudisha kazini kwa kumwongezea mkataba wa ajira usiyo na kikomo, ikiwa ni miaka minne baada ya kustaafu, hivyo kumwezesha kuendelea kupata mshahara na stahili zingine.

Ajira hiyo isiyo rasmi imetokea kwa mchungaji huyo mara baada ya kudaiwa kupata karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuanza kutibu magonjwa sugu yakiwemo kisukari, saratani na UKIMWI kwa kile kinachoelezwa kuwa tiba hiyo inafanyika kwa njia ya imani na kimaombi.

Kuajiriwa upya kwa mchungaji huyo kutamwezesha kupata mshahara kama kawaida na kusitisha pensheni aliyokuwa akiipata kama mchungaji mstaafu.

Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Thomas Laiser alithibitisha kurudi kazini rasmi kwa mchungaji huyo jana, akisema kanisa hilo limetafakari na kubaini umuhimu wa mchungaji huyo katika dayosisi hiyo na taifa kwa ujumla, na kumrudisha ili atumikie umma akiwa ndani ya kanisa hilo.

Alisema mchungaji huyo alipewa kazi hiyo na Mwenyezi Mungu tena kazi kubwa kuliko hata ile aliyokuwa akiifanya kabla ya kustaafu, hivyo iwapo ametukuzwa na Mungu kiasi hicho vipi wao wasimjali na kumweka katika himaya ya kanisa.

Mchungaji Mwaisapile ambaye atabakwa katika Usharika cha Sonjo alipokuwa akitumikia awali, alistaafu baada ya kulitumikia kanisa hilo katika maeneo mbalimbali, ukiwamo Ushariki wa Babati Mjini, Mkoa wa Manyara kwa miaka saba kabla ya kuhamia Sonjo alikotumikia kwa miaka 12 hadi kustaafu.

Tumeaona tumweka vizuri ili aweze kutenda kazi aliyotumwa na Mwenyezi Mungu kwa ufanisi zaidi akiwa anajitosheleza kimapato na kwamba mpango huo hauna kikomo…lakini lugha rahisi ndiyo hiyo kwamba ameajiriwa upya,� alisema Askofu Laiser.

Alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa KKKT, Bw. Israel Kariyongi
kutekeleza maamuzi hayo yaliyofikiwa na Kanisa Machi 3, mwaka huu wakati timu ya viongozi wa kanisa hilo ilipomtembelea kijijini Samunge na kufikia maamuzi hayo kwa pamoja.

Alisema baada ya mchungaji huyo kuelezwa uamuzi huo aliridhika na maamuzi ya kanisa ukizingatia kuwa hana makuu na kwamba kanisa linaamini kwa kumweka katika mazingira mazuri ya kiuchumi anaweza kufanya kazi hiyo ya Mungu kwa ufanisi mkubwa.

Taarifa zaidi kutoka Samunge zimeeleza kuwa huduma inaendelea kama kawaida lakini usafi hasa wa chupa za maji bado ni tatizo linalohitaji kufanyiwa kazi kikamilifu.

Mkono wa Babu sasa umekuwa mwepesi kweli kweli, anaweza kufuta gari zaidi ya 20 kwa muda mfupi tu na hiyo naamini inasaidiwa na wagonjwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali kwamba huduma itatolewa katika magari pekee…lakini bado tatizo kubwa lipo
kwenye usafi, hali ni mbaya sana,� alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kampuni mmoja ya uzalishaji soda na maji kupeleka bidha hizo kwa kiasi kikubwa na kuuza kwa bei ya kawaida tayari matumizi ya maji yameongezeka na kusababisha idadi kubwa ya chupa tupu na maji kuzagaa ovyo.

Basi latelekeza wateja wa babu

Basi la Kampuni ya Air Msae jana lilitelekeza abiria 80 waliokuwa wanakwenda kupata tiba kwa babu baada ya kuharibikia eneo la Ngerenaro, kilomita moja kutoka mjini Arusha.

Baada ya tukio hilo, dereva wa gari hilo alitokomea kusikojulikana na baadaye kukamatwa na polisi wakishirikiana na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) na kulitoza sh. 250,000 kwa kuendesha gari bovu.

Wakati huo huo, Mzee Piniel King’ori (65) aliyedaiwa kwenye gazeti hili jana kupotea baada ya kunywa dawa Loliondo amegundulika amekufa ikiwa ni siku 11 tangu alipoochana na wenzake.

Mwili wa mzee huyo umepatikana baada ya kufukuliwa baada ya kuzikwa na wenyeji Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro baada ya
kutotambulika.

Wenzetu waliokwenda Loliondo wametutaarifu kuwa ndugu yetu amefariki na kuzikwa baada ya kutotambulika, hivi tunaendelea na taratibu za msiba huku tukisubiru mwili wake urejeshwa kwa mazishi ya heshima itakavyoamuliwa na vikao vya familia,� alisema Bw. King’ori nyumbani kwa marehemu eneo la Sekei wilayani Arumeru.

1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Ngastukaaa! Kumbe Dini ni siasa?
watu wanatoa matamko, wengine wanalaani.
wengine wanabariki, machale kundesa chunga imani yako, ngastukaa watu hawana Imani?
March 15, 2011 11:41 PM
 
PHP:
kweli ni fumbo, ngoja nasi tukikusanye tukapate kikombe

Maria Roza usiwe na haraka na hii tiba mbadala.....subiri uwaone wafu wakiwazika wafu wenzao...............................vute subira ya miezi sita usije ukashanga kumbe hata yule mama naye kakata roho......................na huyu mchungaji bomu naye kaishia kwa Bwana kwenda kuhukumiwa kwa ghiliba zake hizi zisizo na kikomo.....................................ninakupenda sana nisinependa ukapatikana na majanga kibao.........................kama figo na maini kufa kutokana na sumu ya miti ambao huyu mzee anachakachua nao...............
 
Barua ya wazi kwa Babu Loliondo
ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

amka2.gif
Wanaokunywa kikombe hiki ndilo somo la barua yangu hii kwako ambayo ni barua ya wazi. Ninakuandikia barua hii mzee mwenzangu nikiwa na heshima kubwa na taadhima isiyo kifani.
Hasa nikiangalia msururu wa watu wanaokuja kwenye mji wako hapo. Hapa kwangu ukiondoa watoto wanaopita kunisumbuasumbua na kuku wa jirani ambao wamefanya uwanja wangu kuwa uwanja wao wa taifa hakuna msururu wowote ule.
Babu Mchungaji, wewe ni mtu mwenye nguvu kuliko wote Tanzania sasa hivi. Una nguvu kuliko rais, una nguvu kuliko mkuu wa polisi, una nguvu kuliko mkuu wa jeshi au Jaji Mkuu, na Spika wa Bunge haifui dafu mbele yako.
Kwa hakika naweza kusema una nguvu kuliko hata viongozi wengine wa dini. Hakuna shehe au padre, mchungaji au mpiga tambiko yeyote anayefua dafu mbele yako. Siyo Pengo, Malasusa wala Mufti Simba ambaye ana nguvu ulizonazo wewe.
Sisemi hivi ili kuwafanya wote hawa waonekane duni; bali kuonyesha kuwa kuna mtu ambaye ameweza kufanya kile ambacho viongozi wengi wa Tanzania wameshindwa kukifanya kwa miaka mingi sasa.
Baba Mchungaji, kuwafanya maelfu ya watu waje kunywa kikombe kimoja cha dawa ya maji ya mitishamba wakiwa na imani ya uwezo wa Mungu kuwaponya kimiujiza magonjwa yaliyoshindikana si jambo dogo.
Kuwafanya wasomi na wasio wasomi, wazee wengine na vijana, matajiri na maskini kuja na kunyenyekea mbele ya kikombe chako cha maji ya dawa si jambo la mchezo hata kidogo.
Kwa hakika kuwafanya hata watu wetu wenye nguvu kubwa kuja na kusimama mstari ili wapate kikombe hiki kwa kweli si utani.
Naamini bila ya shaka kwanza ni kwa sababu ya unyenyekevu unaoonyesha. Lakini zaidi vile vile ni kutokana na jumbe ambao unatokana na huduma hii nzima. Kwamba, watu wasikate tamaa ya maisha kwa sababu wameambiwa "haiwezekani".
Mzee mwenzangu kuna mambo mengi ya kukatisha tamaa katika jamii yetu. Watu wetu wamepindika migongo yao kwa hali ngumu ya maisha na wapo ambao kutokana na masahibu mbalimbali ya maisha wamejikuta katika kona ya kukata tamaa na wengine wamesimama daima bila kujua waende wapi katika njia panda ya kutokujua.
Lakini wewe na kikombe chako cha maji ya dawa umeweza kuwarudishia watu tumaini. Binafsi sijui na wala sijali kama kweli kikombe hicho kinatibu inavyodaiwa. Ninachojua ni kuwa siwezi kubishana na mtu ambaye atasema alikuwa ana kisukari na baada ya kunywa kikombe hicho akakutwa hana kisukari tena.
Nitaweza vipi kubishana na mtu ambaye anasema alikuwa na mgonjwa mahututi na sasa anatembea.
Chochote kinachotokea hapo mjini kwako mzee mwenzangu ni imani ambayo imepotea kwa muda mrefu. Kwamba watu wamepewa sababu ya kuamini zaidi ya nguvu zao wenyewe.
Ni wazi kama wengine walivyokwisha kosoa kuwa hakuna msingi wa kisayansi wa kile kinachotokea hapo. Angalau kwa sasa hakuna uthibitisho wa kisayansi.
Mzee mwenzangu hata hivyo mimi si muumini wa sayansi kuwa ndicho kipimo pekee cha ukweli wa kitu. Mfumo wetu wa sayansi ya kimagharibi umejengwa kutokana na vipimo.
Kile ambacho hatuwezi kukipima na kukithibitisha basi hakipo. Siyo kwamba kinaweza kuwepo ila hatuna kipimo cha kupimia bali ni rahisi kujiaminisha kuwa hakipo.
Babu Mchungaji ninaamini kabisa ya kuwa yawezekana dawa na maji yake yana sifa fulani za kimaabara ambazo labda zitakuja kuthibitishwa na sayansi hiyo.
Lakini wananchi wanaokuja hapo ni wazi hawaji kwa sababu wamevutiwa na bailojia au kemia ya miti shamba na maji ya kunywa. Wanakuja kwa sababu wanaamini kuwa kuna nguvu ya pekee ambayo inatenda kazi katika mazingira hayo na ni wazi wanaihusisha nguvu hiyo na neema ya Mungu.
Hili linanikumbusha simulizi la kwenye maandiko ambapo mtu aliyezaliwa kipofu alimwendea Bwana Yesu na kumuomba amponye. Tunasimuliwa kuwa Yesu alitema mate udongoni akaufikisha na kumpaka yule bwana machoni na kumwambia aende akinawe uso wake kwenye kisima cha Siloamu (Yohana 9).
Wakati wasomi wengi wa Biblia na waamini wanaweza kuwa wamevutiwa na imani ya yule kipofu na maneno ya Yesu pale, kitu kimoja ambacho hakijaelezewa vizuri ni kuwa kwanini Yesu alitumia mate na udongo kutengeneza tope na kumpaka yule kipofu na kumwambia aende na mbele ya safari atakuwa mzima? Bila ya shaka watu waliokuwa karibu hawakuelewa na isingekuwa rahisi kuelewa ni kitu gani kimefanyika pale.
Tunachosimuliwa katika simulizi lile ni kuwa hata wasomi wa kidini wa wakati ule walishindwa kutolea ufafanuzi uponyaji wa mtu yule kiasi cha kumfisha kwa wakuu wa dini kutaka maelezo kwani alikuwa amezaliwa akiwa ni kipofu. Kwa kadiri ninavyofahamu ni muujiza ule peke yake ambapo mtu aliyeponywa aliletwa kushitakiwa na kuhojiwa juu ya uponyaji wake.
Hata leo ninapofikiria hili nashindwa kutolea maelezo mazuri; ni kwanini Yesu alitumia mate na udongo wakati sehemu nyingine aliamuru tu na ikawa?
Wanatheolojia wengine wamewahi kudai kuwa kimsingi Yesu alifanya uumbaji mpya kabisa kwa sababu yawezekana yule jamaa hakuwa hata na gololi za macho.
Binafsi ninaamini ilikuwa ni suala la imani na chombo cha kupitishia uponyaji huo. Yesu angeweza kuamuru ikawa tu au angeweza kumwambia kama alivyowaambia wale wakoma kumi waende kutakasika.
Hivyo Babu Mchungaji, wakati tunabakia na maswali ya kisayansi na kitheolojia na mengine ambayo yako mbele yetu hakuna shaka kuwa umeweza kuwavuta watu wengi na nguvu kama nilivyosema awali ni nguvu kubwa sana. Inahitaji hekima kutumiwa na inahitaji utulivu na busara ya hali ya juu kutoitumia. Najua mzee mwenzangu wakati utakapofika kwamba yakupasa kuacha huduma hiyo au kwamba Mungu akikuongoza na kusema "inatosha" basi hautalazimisha kuendelea. Kwani kila kipawa kinapimwa kwa kipimo chake.
Lakini Babu Mchungaji nilipokaa na kufikiria zaidi nguvu hii ilivyo kubwa nimejikuta nikikumbushwa juu ya gonjwa kubwa ambalo limetukabili kama taifa na imebidi nijiulize kama kikombe chako hiki cha Loliondo chaweza kutusaidia kutibu ugonjwa ambao umewaathiri watu wetu mbalimbali hasa wale wenye madaraka na uwezo mkubwa wa kifedha, hadhi na vyeo.
Ni ugonjwa mbao hadi hivi sasa haujapatiwa tiba yake kama vile ulivyo ukimwi na saratani za aina mbalimbali. Ni ugonjwa ambao umetusababisha na unaendelea kuligharimu maisha ya Watanzania. Huu ni ufisadi.
Baba Mchungaji, laiti kikombe chako kingeweza kututibia watu walioathiriwa na ugonjwa mbaya sana. Wale wenye kutumia madaraka yao vibaya kana kwamba nchi hii ni ya kwao peke yao na wengine ni wapangaji; wale wenye kuliingiza taifa katika mikataba mibovu na wanapoambiwa wawajibike wanatushangaa; wale ambao wanafikiri kuwa kila anayewakosoa basi anawachukia na hivyo wanakesha kwenye runinga wakihubiri vitisho dhidi ya Watanzania! Laiti kikombe chako hiki kingekuwa tiba kwa gonjwa hili la ulevi wa madaraka!
Sijui ni watu wangapi ambao wangeendelea kuja hapo kijijini kwako kama wangejua kuwa ukinywa kikombe hiki nawe umetoka kudhulumu watu, umekula rushwa, umeiba fedha za umma, umetumia madaraka yako vibaya kujinufaisha au kuwaonea maskini basi una siku saba tu za kuishi! Nina uhakika mkubwa kwamba yawezekana watu ambao wangekuja kupata kikombe hicho wangekuwa kweli wenye kuhitaji si watu ambao wamekuja ili wapate kupona na wakirudi kwenye maofisi yao waendelee kuwanyanyasa na kuwaonea Watanzania.
Labda mzee mwenzangu unaweza kuzungumza na "yule Aliye Juu" kuona kama kuna uwezekanao wa kupata maelekezo ya ziada ya jinsi ya kutumia dawa hasa kwa watu ambao ni mafisadi au wenye mrengo wa ufisadi.
Hata kama haiwezi kuwadhuru unaweza kumuomba "Bwana Mkubwa" kama watu hawa wakinywa basi mioyo yao itageuzwa na wataanza kuwatumia Watanzania kwa uadilifu. Kwani ina maana kupona halafu urudi na kuwaumiza wengine? Nina uhakika hata mbinguni wanaweza kusikiliza rufaa yangu hii.
Ukiondoa hilo hapo Babu Mchungaji ni matumaini yangu kuwa wale wote "wanaokunywa kikombe hiki" watapata muda wa kutafakari maana ya kile wanachokipata. Hata kama si wote watapona ni wazi kila mmoja kwa namna yake amepata tumaini jipya la kuishi.
Kwamba wananchi wetu wameonyeshwa kuwa yupo mtu anayejali matatizo ya watu wetu na ya kwamba usiku na mchana tena pasipo kudai makubwa yuko tayari kuwahudumia wananchi.
Kiongozi ambaye ameonyesha kujali utu wa mtu na si sura za watu au kuonyesha upendeleo wa pekee pasipo sababu yoyote ile. Ndani yako babu mchungaji maelfu ya watu wetu wameona kile walichokikosa kwa viongozi wao.
Leo wanaoitwa "viongozi" wetu wanapoenda kupanda miti wanatandikiwa mikeka! Leo viongozi wetu hata kushika sululu kuonesha mfano, au kubeba matofali kama alivyofanya Mwalimu wanaona wameshushwa sana. Ndani yako Watanzania hata wale wasioamini dawa unayowapatia wananchi wanajikuta wanakubali kwa jinsi gani uko kati ya watu na kweli ni mtu wa watu. Na nina uhakika hata utakaposema kuwa sasa imetosha Watanzania wala hawatakulalamikia sana watakuelewa kwa sababu umesikizana nao na kukaa nao na kuyaelewa matatizo yao.
Kwani zawadi kubwa unayowapatia watu siyo dawa ya mwili bali dawa ya mioyo. Kwani katika kuja kwao watu wetu wamekaa pamoja na kuzungumza. Wanapofika hapo urafiki unajengwa na mwingine ni ududu wa ndani kabisa.
Umeweza kufanya kile kilichowashinda watawala wetu kwani hapo ulipo hakuna udini, ukabila, chama, au umahali. Na ndio maana viongozi wa dini waliojaribu kujiingiza na kukupuuzia wananchi wamewapuuza wao.
Katika mji wako hapo japo watu wanajua wewe ni Mkristu tena mchungaji hakuna anayelishikilia jambo hilo kama silaha dhidi yako.
Katika taifa ambalo udini unasukumizwa na watawala wetu mzee mwenzangu unatumia dini ile ile kutuonesha kuwa sisi ni watu wamoja, ni taifa moja, na ya kuwa matatizo yetu yanatuhusu sis sote. Hakuna kansa inayomsibu Mwislamu peke yake; hakuna kisukari kinachochagua Mlutheri na Mkatoliki.
Ndiyo maana wakati na saa hii tiba kubwa ambayo inatokana na kikombe hiki siyo ile ya mwilini bali ya mioyo ya Watanzania.
Laiti watawala wetu wangetambua jambo hili na laiti Watanzania ambao wanaelewa somo hili watawakataa viongozi wa kisiasa na kidini wanaojitahidi kutubagua na kututababishia vurugu. Laiti Watanzania wenye ujasiri hawataacha radio zenye sumu ya udini na ukabila zikiendelea kumwaga sumu hizo katika mioyo ya Watanzania.
Ni hapo tutakapotambua kuwa sote tunahitaji tiba ya mioyo yetu iliyojaa chuki, uonevu, kisasi, hasira na ukandamizaji ndipo tutaweza kweli kusimama kujenga taifa letu sote kwa pamoja kama wale wanaokutana kule Loliondo kwako mzee mwenzangu.
Nakutakia maisha mema na marefu na huduma nzuri!
Ubarikiwe pamoja na wote wenye kukusaidia!
Mzee mwenzako,
MM Mwanakijiji
 
Ruth sijajua,wewe kama ww point yako ni ipi.kwamba anaponya au Haponyi angalia watu wanavyo kutolea Macho juu ya swali lako mi sitii neno.
 
Back
Top Bottom