Huyu Babu wa Loliondo mnamwonaje?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Nimepitia taarifa nyingi juu ya tiba zitolewazo a huyu Babu wa Loliondo....................mlionyeshewa mvua zake hebu mtupashe habari...................zaidi ..................................hivi kweli yupo Mwenyezi Mungu kwenye tiba tajwa?????????????????

Daktari: Mgonjwa Loliondo amepona Ukimwi Send to a friend Monday, 14 March 2011 21:40

atibiwaukimwi.jpg
Mussa Juma, Loliondo na Deusdedit Moshi, Dodoma
DAKTARI Joachiam Mbosha wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Ngorongoro ya Wasso, amethibitisha kuwa mmoja wa wagonjwa wa Ukimwi aliyekwenda kutibiwa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile, maarufu kwa jina la 'Babu', huko Samunge, Loliondo amepona Ukimwi.
Wilia John Lengume (30), juzi alikuwa kivutio kwa mamia ya watu baada ya kutangazwa na Mchungaji Mwasapile kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Usharika wa Sonjo iliyoshirikisha mamia ya watu. Akizungumza katika ibada hiyo, Mchungaji Mwasapile alisema Lengume ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza kumtibu.

Akizungumza na Mwananchi kanisani hapo, Lengume alisema baada ya mumewe, John Meneyi Lengume kufariki dunia mwaka 2002, aliamua kwenda kupima na kuonekana kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) lakini baada ya kutumia dawa hiyo alisema sasa hana tena virusi vya Ukimwi. Alisema kwa muda mrefu mama huyo alikuwa akitumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo (ARV) katika Kituo cha Afya Didodigo wilayani Ngorongoro.
Akizungumza na Mwananchi jana kuhusu kupona kwa mama huyo, Dk Mbosha alisema: "Hiki kitu kilituchanganya sana, nakumbuka mimi ndiye nilimpima mwaka jana... ikabidi niwaeleze watu wa maabara Hospitali ya Wasso ili wafuatilie aliyempima awali huyu mama na nilimweleza aache kutumia dawa kwani hana HIV," alisema Dk Mbosha.
Dk Mbosha alisema alihamishiwa katika kituo hicho cha Afya cha Digodigo zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alimkuta mama huyo akiendelea kuhudhuria kliniki na kupata ARV pamoja na ushauri wa kulinda afya yake lakini alianza kuona mabadiliko makubwa ya afya yake na ndipo alipoamua kumpima tena.

Aliamua kumpima mwaka jana baada ya kuona 'CD4' (kinga za mwili) zake zinaimarika kiasi cha kutohitaji kuendelea kutumia dawa hizo za kupunguza makali.Aliamua kumhoji kujua siri iliyokuwa imejificha katika mabadiliko hayo ambayo alisema yalikuwa ya haraka haraka mno na ndipo alipomweleza kwamba alipata tiba kutoka kwa Mchungaji Mwasapile.
Lengume alisema licha ya mumewe kufariki, mtoto wao mmoja pia alifariki dunia lakini baada ya kutumia dawa ya Mchungaji Mwasapile, maisha yake ni mazuri na ana mtoto mwingine mchanga anayeitwa Evelyn ... "Namshukuru Mungu na Mchungaji Mwasapile sasa nimepona na ninaishi maisha mazuri tu."Alisema baada ya kuanza kuugua, mchungaji huyo, ndiye aliyemfuata na kumuomba amtibu akimthibitishia kwamba atapona maradhi yaliyokuwa yakimsibu.Hata hivyo, kitalaamu bado haijathibitika kupatikana kwa tiba wala chanjo ya Ukimwi.

Ushuhuda wa Mzee Mtaki
Mwingine aliyejitangaza kupata ahueni kubwa kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsibu baada ya kupata tiba ya mchungaji huyo ni aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mzee Ali Said Mtaki.Mzee Mtaki (81) ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mpwapwa katika miaka ya 1980, Mkuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida kwa nyakati tofauti, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mbunge wa Afrika Mashariki na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Usharika Mkoa wa Dodoma, alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kutetemeka kiasi cha kushindwa kutembea na kuzungumza vizuri.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Mtaa wa Nyerere Mjini Dodoma, Mzee Mtaki alisema tangu anywe dawa ya mchungaji huyo Jumanne ya wiki iliyopita huko Loliondo, sasa anaendelea kupata nafuu siku hadi siku.
Akiongea kwa kujiamini alisema sasa anajiona kama amepona na anaweza kuendelea na shughuli zake ikiwamo ya uwakala wa bima... "Si unaona nilikuwa natembea kwa shida, kuzungumza kwa taabu, sasa hali yangu ni nzuri nafanya kila kitu bila kusaidiwa."Akielezea safari yake ya siku mbili ambayo ilimfikisha kijijini Samunge, Loliondo anasema alifuatana na mkewe, Amina Mtaki ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na mgongo. Anasema naye pia amepona.

Anasema safari ya kutoka Dodoma hadi Samunge iliwagharimu Sh60,000 kila mmoja na baada ya kufika huko walikuta umati mkubwa wa watu ukisubiri kupata tiba hiyo. Anasema aliwakuta watu wa mataifa mbalimbali, Waafrika, Wahindi, Wazungu na Waarabu... "Watu walikuwa wengi na kila mtu na matatizo yake lakini Mchungaji alikuwa akiwasisitizia kwamba habagui watu na haangalii dini au uwezo wa mtu."
"Katika mkusanyiko huo nilibahatika kukutana na Askofu Thomas Laizer wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati akiwa amefuatana na mama wa kizungu. Nilikaa karibu na mama yule wa kizungu ambaye sikumbuki jina lake. Nilimshika Askofu Laizer mkono tukasalimiana na kuongozana naye kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile."

"Tulipofika kwa Mchungaji, Askofu Laizer akamwambia mchungaji kwamba ana wageni wake, hivyo mama yule wa kizungu akapewa dawa na mimi pia nikapewa na mke wangu akapewa pamoja na kijana wangu japo yeye hakuwa na tatizo lolote la kiafya."

Last Updated on Tuesday, 15 March 2011 08:54 Comments

123456

0 #80 Brighton Mbowe 2011-03-15 20:19 JUMBE UNASEMA "Jana niliongea na watu wawili ambao jamaa zao walienda kwa Babu. Mmoja dada yake alikua na ukimwi na ni mkazi wa Karatu baada ya kunywa dawa ya babu akaacha tiba na ameshafariki. Yeye alikua wale wa mwanzo kwenda kwa babu. Mwingine jamaa yake ana pressure amekunywa maji na ameacha tiba hivi yuko taabani amelazwa hospitali. hapa tunasemaje?" Mimi mwenzio rafiki yangu yupo mahututi tangu jana. aliacha ARV zaidi ya wiki kwa kuamini dawa ya babu
Quote

0 #79 Malaika wa Duniani 2011-03-15 20:15 Hiyo yote ni PROPAGANDA tu. Mnajua huko WEST AFRICA mambo haya ni COMMON sana.
imefikia hadi RAISi wa GAMBIA anadai kuwa anatibu AIDS/ aondoa virusi HIV.
Loooh Jamani hizi ni CAMPAIGNi na propaganda nasi hapa tunaiga za Africa Magharibi. HAMUONI kuwa kuna mikakati maalumu na mchezo mkubwa wa kuwatafuna waliyo DESPERATE people. Kunafungu la wajanja wemesuka network hii na hatimaye kunufaika na kufaidisha mradi wao huu ili kujiandaa na UCHAGUZI ujao 2011. " mutaniambia ya kweli baadaye...tusubiri mtaona!!
Quote

0 #78 hezron Lus 2011-03-15 20:10 YES @Tunaishi nyakati za mwisho. Neno la Mungu linasema waziwazi kuwa nyakati za mwisho zitakuwa ni siku za hatari, hatari kubwa inayomaanishwa hapa ni watu kujitenga na imani na kufuata roho zidanganyazo – 1Tim. 4:1.
Biblia pia inasema, nyakati hizi za mwisho watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama inawezekana, hata walio wateule – Mt.24:23-24. Ibilisi anahangaika kuwapeleka watumishi wake wengi kwa lengo na kuwavuta na kuwapoteza watu wasikae katika mapenzi ya Mungu, ili hatimaye wakataliwe na Mungu. Kwa sababu hiyo basi, tunapaswa kuwa makini sana na mambo yote yanayotokea nyakati hizi.
Kwa sasa hivi, kwa sababu kanisa bado halijanyakuliwa , mpinga kristo bado hajafunuliwa. Lakini roho yake tayari inatenda kazi. Neno la Mungu linasema kuwa kutenda kazi kwa roho ya mpinga kristo kunaambatana na ishara na ajabu za uongo ili kuwavuta na kuwapoteza wanadamu – 2Thes. 2:7-12, Uf.13:11-14.
Kwa hiyo ndugu zangu, tunapaswa kuwa makini sana katika kila jambo, tusiwe wepesi wa kuchulikwa na kila upepo unaovuma. Hata kama mtu atasema kuwa anatumiwa na Mungu, bado hatupaswi kuwa wepesi wa kukubaliana naye.GOOD!!!!!!!!!!! !!
Quote

0 #77 hezron Lus 2011-03-15 20:02 HII SAFI SAANA"kama waandishi wahabari mnawajibu wa kutoa habari zenye ukweli na mantiki ya hali ya juu kwa jamii na si kupotosha jamii, naamini mlikuwa na wajibu wakufuatilia uhakika wa hii habari yenu kwa kina sana, mfano je wilaya ya ngorongoro ina wagonjwa wangapi wa HIV? je wangapi wanatumia ARV? Je wangapi wameacha ARV na kwenda kwa mchungaji kunywa hiyo dawa? na Je wangapi kati hao waliokunywa wamepona? na wangapi wamekufa baada ya kuacha ARV?
Quote

0 #76 Kalumanzila 2011-03-15 20:01 Quoting mie:
Quoting from loliondo mkazi:
Ama kweli nimeamin habari yenye nia mbaya inasambaa sana kuliko habari yenye nia nzuri,nyinyi gazeti mwananchi nyinyi kama wanahabari mbona mfuatiliii habari za watu wenye ukimwi hapohapo samunge na digodigo na karatu amabao wamekufa kwa baada ya kunywa hiyo dawa ya babu(mchungaji) kwa ufahamu wangu mimi kuna wagonjwa 13 wa ukimwi wamefaliki.
kama waandishi wahabari mnawajibu wa kutoa habari zenye ukweli na mantiki ya hali ya juu kwa jamii na si kupotosha jamii, naamini mlikuwa na wajibu wakufuatilia uhakika wa hii habari yenu kwa kina sana, mfano je wilaya ya ngorongoro ina wagonjwa wangapi wa HIV? je wangapi wanatumia ARV? Je wangapi wameacha ARV na kwenda kwa mchungaji kunywa hiyo dawa? na Je wangapi kati hao waliokunywa wamepona? na wangapi wamekufa baada ya kuacha ARV? WHAT YOU GUYS (MWANANCHI)HAVE DONE TO OUR COUNTRY ITS IRRESPONSIBLE JOURNALISM, SIO UNAMPIGIA MTU SIMU SAA TATU USIKU UNAJITAMBULISHA KAMA JAMAA YA MGONJWA AFU UNAMWUULIZA SWALA NYETI KAMA HILI AFU KESHO ASUBHUHI UMECHAPISHA HABARI KWENYE FRONT PAGE
NAOMBA TUWE MAKINI SANA HAPA ILE NI IMANI JE WASIOAMINI TUWAACHE WAFE? KWAN WAPO WENGI TU AMBAO WENYE HIV​

sawasawa kabisa​
Hivi hamuelewi? Sio wote watapona,ni wenye imani tu. Mimi nilikuwa naumwa vidonda(Nilipim a Amana Hospital)vya tumbo nikaenda kwa Dr Rahabu alinipa dawa kwa Tsh 250,000 kisha akaniambia utapona kwa nguvu za mungu. Kwa kuwa niliamini nimepona,Ila kwa taarifa yako kunawtu wanatumia hata 1,000,000 na hawaponi na dawa ni ile ile.
Quote

-1 #75 Kalumanzila 2011-03-15 19:51 We unaonekana ni mdini sana. Kichwa cha habari kinaelezea uthibitisho wa Dr juu ya habari za huyo mama.Sasa mwananchi swala la udini wameandika wapi? Mi nafikiri uwe unachangia vitu vya msingi sio kila ukichangia unataka kuhusisha dini.Kuhusu Maabara kwa taarifa yako hata hao madocta wa hospital wanaenda kama hujui.Quoting 2pak hitem all:
Yaleyale ushuhuda kanisani usanni mtupu.
Leteni ngoma maabara mzee apate tuzo ya ukweli.
Nanyie mwananchi kama mmeamua kuchukua kazi ya gazeti la kiongozi na nyakati bora mkae pembeni week nzima all most asilimia 75 habari ni za kanisa tu!​
Quote

+1 #74 zubeda 2011-03-15 19:43 Binadamu lazima atakufa, hivyo swali kuu ni je dawa inaponyesha magonjwa sugu yaliyotajwa?

Tukumbuke mgonjwa wa UKIMWI au AIDS hali zao huwa mbaya kama pia wanasumbuliwa na majonjwa nyemelezi mfano nimoniya,ini kuharibika kwa hepatatis B na C,kaswende ya ubongo n.k

Babu kataja magonjwa sugu yanayoweza kutibiwa hapo Loliondo, lakini kuna mtu anaweza kuwa na HIV pamoja na magonjwa mengine kibao ambayo hayatibiwi na Babu.

Hivyo hao waliokufa ama siku zao zimefika au wagonjwa wa UKIMWI walikuwa pia na magonjwa nyemelezi ambayo hayatibiki kwa dawa ya Babu.

Suala hapa ni kuwa kama una virusi vya HIV na hauna magonjwa hatari nyemelezi Babu anasema virusi vya HIV zitapotea na wewe kuwa HIV Negative.
Quote

0 #73 wamjinia 2011-03-15 19:34 si chuki binafsi bali shetwani anafanya kazi ndani yao, maana shetwani halali analandalanda masaa 24 akitafuta watu wake wamfanyie kazi. mungu ameamua kuleta huruma yake ni kama alivyomtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali apate uzima wa milele.
Quote

0 #72 wamjinia 2011-03-15 19:27 asante mungu kwa kutuletea tiba yako ya ajabu!
Quote

+1 #71 sadiky Bota 2011-03-15 18:55 Hizi niporojo, je hukusikia babu anaombea dawa kabla ya kunywesha watu! nadhani wewe bado una ugonjwa wa kidhehebu, unadhani unaposali tu ndiko kuliko sahihi, na siyo ajabu kwani Kakobe naye anadhani hivyo, baada ya kuhiji eti babu kaokoka!Hamuami ni madhehebu yote isipokuwa mlipo. Nikukumbushe kitu!hayo madhehebu mliyopo ndani yamekuja juzi tu. sidhani kama ni zaidi ya miaka 100. sasa wote waliokufa kabala hawataona mbinu kwa sababu eti hwakuokoka!?[

@Senior E na wengine wenye imani haba.Mungu hana kanuni ya kuponya, je kwani yaesu hakuwahi kuchanganya mate yake na udongo na kisha kumpaka kipofu na baadae kupona!?na je hapakuwahi kuwa na jemadari wa jeshi la israeli nyakati zile aliye amriwa na nabii akajichovye mara saba kwenye maji ya mto jordan na akapona ukoma wake!Je hiyo siyo hiyo biblia. Tafadhali tusitumie ushawishi kupotosha watu na kupoteza imani za watu kwa kudai ni siku za mwisho.
Pili kwa wale wanasayansi wanaosema it has to be proven in the lab"as far as I know, science has never proven anything". Kama una imani nenda kwa babu kapate dawa. Lipi bora!kuwa na imani na kupona au na hata kutokupona , au kutokuwa na imani na hatimaye kufaaa!Wasio wagonjwa ndio wanao mkandia babu. Laiti kama mngekuwa kwenye hali ya ugonjwa....je mngendelea kusema...nyakati za mwisho...huo mwisho umeuona wewe.....????
Quote

+1 #70 Thobias 2011-03-15 18:45 Tuna mshukuru Muumba aliyekufumbulia karama hiyo na tunakutakia kheri na fanaka katika kuwahudumia watu hao ambao wamekuwa wakitaabika katika maisha yao kwa siku nyingi. Mwenyezi Mungu akuongoze vema " BABU."
Quote

+1 #69 Kibandula 2011-03-15 18:42 #65 2pak hitem all-Imani na mahabara? Are you ok up there?
#65 2pak hitem all-You have ADD (Attention Defiency Disorder). Kanisa halihusiki ili walioppona ndio wanajitangazia.
#63 jah man-Huna mungu ila shetani na malaika zake ni majini.
Quote

+1 #68 Jumbe 2011-03-15 18:30 Jana niliongea na watu wawili ambao jamaa zao walienda kwa Babu. Mmoja dada yake alikua na ukimwi na ni mkazi wa Karatu baada ya kunywa dawa ya babu akaacha tiba na ameshafariki. Yeye alikua wale wa mwanzo kwenda kwa babu. Mwingine jamaa yake ana pressure amekunywa maji na ameacha tiba hivi yuko taabani amelazwa hospitali. hapa tunasemaje?
Quote

0 #67 sadiky Bota 2011-03-15 18:30 Hizi niporojo, je hukusikia babu anaombea dawa kabla ya kunywesha watu! nadhani wewe bado una ugonjwa wa kidhehebu, unadhani unaposali tu ndiko kuliko sahihi, na siyo ajabu kwani Kakobe naye anadhani hivyo, baada ya kuhiji eti babu kaokoka!Hamuami ni madhehebu yote isipokuwa mlipo. Nikukumbushe kitu!hayo madhehebu mliyopo ndani yamekuja juzi tu. sidhani kama ni zaidi ya miaka 100. sasa wote waliokufa kabala hawataona mbinu kwa sababu eti hwakuokoka!?[
Quote

0 #66 sadiky Bota 2011-03-15 18:20 @Senior E na wengine wenye imani haba.Mungu hana kanuni ya kuponya, je kwani yaesu hakuwahi kuchanganya mate yake na udongo na kisha kumpaka kipofu na baadae kupona!?na je hapakuwahi kuwa na jemadari wa jeshi la israeli nyakati zile aliye amriwa na nabii akajichovye mara saba kwenye maji ya mto jordan na akapona ukoma wake!Je hiyo siyo hiyo biblia. Tafadhali tusitumie ushawishi kupotosha watu na kupoteza imani za watu kwa kudai ni siku za mwisho.
Pili kwa wale wanasayansi wanaosema it has to be proven in the lab"as far as I know, science has never proven anything". Kama una imani nenda kwa babu kapate dawa. Lipi bora!kuwa na imani na kupona au na hata kutokupona , au kutokuwa na imani na hatimaye kufaaa!Wasio wagonjwa ndio wanao mkandia babu. Laiti kama mngekuwa kwenye hali ya ugonjwa....je mngendelea kusema...nyakati za mwisho...huo mwisho umeuona wewe.....????
Quote

123456
Refresh comments list
 
Nimepitia taarifa nyingi juu ya tiba zitolewazo a huyu Babu wa Loliondo....................mlionyeshewa mvua zake hebu mtupashe habari...................zaidi ..................................hivi kweli yupo Mwenyezi Mungu kwenye tiba tajwa?????????????????

Ingawaje sijapata dawa zake, lakin nina imani kubwa na kutibu kwake kwa sababu anakutibu kwa imani na dawa anakupatia pia.
So anakutibu kwa nguvu mbili wakati mmoja, lazima shetani akimbie hapo
 
hii nayo ni mahusiano na mapenzi? hapa nafikiri sio sehemu yake? peleka kwenye chit chat
 
atibiwaukimwi.jpg
Kwa aliyepona na VVU ungelimtarajia awe na ahueni zaidi ya hii..........................hii afya haitii matumaini...........................
 
PHP:
[B] [IMG]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon1.png[/IMG] Re: Huyu Babu wa Loliondo mnamwonaje? [/B]

    hii nayo ni mahusiano na mapenzi? hapa nafikiri sio sehemu yake? peleka kwenye chit chat

Tatizo lako naona ni upeo.............mahusiano huzaa hata haya...................................ambayo Babu anadai kuyatibu.................
 
PHP:
Ingawaje sijapata dawa zake, lakin nina imani kubwa na kutibu kwake kwa sababu anakutibu kwa imani na dawa anakupatia pia.
So anakutibu kwa nguvu mbili wakati mmoja, lazima shetani akimbie hapo

Ninasikia baadhi ya masharti yake ni kuwa tuache ngono zembe sijui ni kweli kasema hayo au anapakaziwa...............
 
PHP:
   	  0 	  #80  Brighton Mbowe 2011-03-15 20:19 JUMBE UNASEMA "Jana  niliongea na watu  wawili ambao jamaa zao walienda kwa Babu. Mmoja dada  yake alikua na  ukimwi na ni mkazi wa Karatu baada ya kunywa dawa ya babu  akaacha tiba  na ameshafariki. Yeye alikua wale wa mwanzo kwenda kwa  babu. Mwingine  jamaa yake ana pressure amekunywa maji na ameacha tiba  hivi yuko  taabani amelazwa hospitali. hapa tunasemaje?" Mimi mwenzio  rafiki yangu  yupo mahututi tangu jana. aliacha ARV zaidi ya wiki kwa  kuamini dawa  ya babu
  Quote

Kama hizi taarifa ni za kweli yawezekana kabisa huyu Babu hatofautiani na yule Kibwetere wa uganda aliyeua wengi kwa imani potofu za kidini....................
 
PHP:
Niliogopa kusema maana Ruta mmmhh namuheshimu nikaogopa nisije vunja sheria ya kwao

refresh na utafurahi kuwa mahusiano yamejaa tele hapo....................
 
PHP:
Ingawaje sijapata dawa zake, lakin nina imani kubwa na kutibu kwake kwa sababu anakutibu kwa imani na dawa anakupatia pia.
So anakutibu kwa nguvu mbili wakati mmoja, lazima shetani akimbie hapo

Ninasikia baadhi ya masharti yake ni kuwa tuache ngono zembe sijui ni kweli kasema hayo au anapakaziwa...............

Yah

Ni kweli mkuu, amesema wazi wazi kwamba akikuponya kwa dawa yake mtu sharti asirudie kufanya uzinzi, la sivyo fasta unawahi namba ahera
 
hii nayo ni mahusiano na mapenzi? hapa nafikiri sio sehemu yake? peleka kwenye chit chat

Kaka

Sio kwa vile hii sredi haihusishi mwanamke na mwanaume basi ndio tuseme haistahili hapa au haina mahusiano, hapana.
Mahusiano yapo kwa uponyaji wa Babu na Watu wanaoenda kwake.
So kitendo cha watu kukutana na kubadilishana mawazo, au kusaidiana tayari ni uhusiano
Nimejitahidi kuelezea jaman
 
Serikali, Ndesamburo watimiza ahadi Loliondo Send to a friend Monday, 14 March 2011 21:37

ndesaahadi.jpg
Wananchi mbalimbali wa mji wa Moshi na vitongoji vyake wakijiandikisha katika ofisi za Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo kwa ajili ya kwenda Loliondo kupata tiba ya dawa kwa mchungaji Ambilikile Mwasapile. Picha na Dionis Nyato

Waandishi Wetu
SERIKALI imeanza kutimiza ahadi yake ya kumsaidia Mchungaji Ambilikile Mwasapile (76) anayedaiwa kutoa tiba ya magonjwa sugu katika Kijiji cha Samunge, Loliondo, mkoani Arusha baada ya kutoa mashine ndogo ya kufua umeme (jenereta) na kupeleka wauguzi na askari wa kutosha.Wiki iliyopita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema Serikali ilikuwa inaandaa utaratibu wa kutuma idadi ndogo ya wauguzi ambao wangesaidia kutoa huduma kwa watu watakaohitaji ambazo zingekuwa nje ya zile zinazotolewa na Mchungaji Mwasapile. Aliahidi kupeleka gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kijijini humo ili kutoa msaada wa haraka kwa watu watakaohitaji huduma hiyo.

Kutokana na mchango huo, kazi ya ugawaji wa dawa hiyo kuanzia juzi ilikuwa ikienda kwa haraka zaidi tofauti na awali. Pia sasa wagonjwa mahututi wanafikishwa kwanza kwa wauguzi kabla ya kupelekwa kwa mchungaji huyo Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).Pia Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wameweka kambi jirani na nyumba za Mchungaji Mwasapile na wamekuwa wakisimamia magari na hata kusaidia kusambaza vikombe vya dawa kwenye magari hayo ili kuondoa msongamano.
Aidha, kupatikana kwa huduma hiyo ya umeme, hivi sasa Mchungaji Mwasapile ameanza kufanya kazi hadi usiku, kutokana na Serikali kupitia Halmashauri ya Ngorongoro, kumkabidhi jenereta hiyo. Sasa inasaidia kupatikana kwa mwanga wa kutosha katika eneo analotoa tiba na nyumbani kwake.

"Naishukuru sana Serikali kwa kuleta umeme hapa na kuna wauguzi wamekuwa wakisaidia watu wanaokuwa mahututi, ila bado kuna tatizo la vyombo vya kuchemshia na kutolea dawa kutokana na ongezeko kubwa la watu," alisema Mchungaji Mwasapile.Mwenyekiti wa Kijiji cha Samunge, Michael Lengume alisema tayari Serikali ya Kijiji hicho kwa kushirikiana na viongozi wengine wameunda kamati mbalimbali za kukabiliana na wingi wa watu.

"Kijiji chetu kina kaya 500, sasa. Wingi wa watu ambao unafikia hadi 30,000 kwa siku ni janga na ndiyo sababu tumejipanga kuhakikisha hakuna madhara ambayo yanatokea," alisema Lengume na kutaja moja ya kamati hiyo kuwa ni ya afya, usafi na mazingira."Pia tumehamamisha watu kuleta vyakula hapa na huduma nyingine na sasa chakula kipo. Hakuna sababu mtu kutoka Dar es Salaam kuja na chakula chake," alisema Lengume.
Alitoa wito kwa kampuni za simu kupeleka minara ya mawasiliano japo ya muda ili kuondoa adha ya watu kukosa mawasiliano na ndugu zao wakiwa kijijini hapo.Mwandishi wa habari hizi juzi aliwashuhudia wauguzi wakiwabeba wagonjwa kwenye machela na kuwapeleka kunywa dawa kwa mchungaji Mwasapile na baadaye kuwabeba na kuwarejesha katika Zahanati ya Samunge kupumzika.
Tatizo kubwa sasa ni jinsi ya kufika kwa mchungaji huyo na kuna wasiwasi kwamba kama mvua zikiendelea kunyesha itakuwa vigumu kwa wananchi kufika huko kupata huduma. Tatizo ni kubwa hasa kwa wananchi wanaotumia Barabara ya Kigongoni, Engaruka, pembezoni mwa Mlima Oldonyolengai, Digodigo hadi kufika Samunge.

Akizungumza kwa simu kutoka Arusha baada ya kutoka Semunge kupata matibabu, mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Stella Ludovick alisema pamoja na misaada mingine ya kibinadamu, ujenzi wa barabara ya kuelekea katika kijiji hicho ni muhimu zaidi."Ndiyo, misaada hiyo mingine ni muhimu lakini, barabara ni tatizo la msingi kabisa. Serikali inapaswa kulishughulikia haraka tatizo la barabara kama kweli ina nia ya kusaidia huduma ya babu huyo," alisema Stella.

Alisema ilimchukua saa tisa kutoka Arusha hadi kijijini Semunge... "Barabara ni mbaya sana na kimsingi hili ndilo tatizo kubwa. Sisi tuliondoka Arusha saa 4:00 usiku na kufika kijijini huko saa 3:00 asubuhi ya siku iliyofuata. Saa tisa mtu uko njiani."Magari yanayotumika ni magari ya watalii ambayo mvua ikinyesha, hayawezi tena kwenda.
Nauli yake kutoka Arusha hadi Loliondo ni Sh150,000 kwa abiria. Zamani magari hayo yalikuwa yakisubiri abiria lakini kutokana na msongamano wa wagonjwa hili limekuwa haliwezekani tena. Mfanyabiashara gani atasubiri juma moja kupata tiba?"

Alisema maeneo mengi ya barabara hiyo ni mabaya kutokana na kujaa vumbi na mashimo, huku wingi wa magari yanayosafirisha wagonjwa kuelekea katika kijiji hicho yakiongeza tatizo hilo.

Ndesamburo atimiza ahadi
Mbunge wa Moshi Mjini, Phillemon Ndesamburo ametimiza ahadi ya kutoa usafiri bure kwa wakazi wa jimbo hilo kwenda Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile.Ndesamburo aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tangu kuanza kwa huduma hiyo amegundua kuwa wananchi ndiyo wanaopata shida zaidi kufika Loliondo.

Alisema baada ya kuguswa na tatizo hilo, ametoa magari mawili aina ya Bedford na Youmork yenye uwezo wa kubeba wagonjwa 73 ambayo yataanza kutoa huduma kesho. Hata hivyo, Ndesamburo alikuwa ameahidi kuwapeleka wananchi wa jimbo lake huko Loliondo kwa helikopta yake kabla ya kubadili uamuzi huo na kutumia magari hayo makubwa.
Alisema msaada huo hauhusiani na itikadi za chama cha siasa. Usafiri huo ni kwa ajili ya wakazi wa Moshi Mjini na vinatumika vitambulisho vya kupigia kura kuwabaini.Ndesamburo alifafanua kuwa wakazi hao watatakiwa kujitegemea chakula, maji na Sh500 ya kumlipa mchungaji huyo.
Mbunge huyo alisisitiza kuwa huduma hiyo si ya muda mfupi hivyo kuwatoa wasiwasi wakazi ambao wamekuwa wakigombea kwenda katika awamu ya kwanza kwa hofu kuwa inaweza iwe ndiyo mwisho.
Habari hii imeandikwa na Kizitto Noya, Dar; Mussa Juma, Loliondo na Fina Lyimo, Moshi.

Comments

0 #11 Emaculata Mlwale 2011-03-15 18:48 Nashangaa watu wanaleta mashara wakati Mungu kanuletea uponyaji kupitia mchungaji huyo mstaafu. Masuala ya dini na hili wapi na wapi. Acheni ufukara wa kufikiri, watu mmsoma lakini uwezo wenu wa kufikiri sifuri. Au mliandikiwa pepa zenu
?
Quote

0 #10 Mmao Josephat 2011-03-15 16:47 Ni viziri sana serikali kutoa gari wagonjwa huko Samunge Loliondo.
ila Ndesamburo ametisha kwa kutoa gari mbili kwa wakati moja,
Hongera baba Ndesa pesa una kura 2015 kama kawa.
Asante sana.
Quote

0 #9 ismail 2011-03-15 15:57 Baba ndesamburo wewe ndio mtu,unayejua utu,
lukuvi hana shida mponda hana elimu,
BABU WA LOLIONDO NI BABU WA WANADUNIA NZIMA KWANI ANATIBU DUNIA, HIVYO TUMWOMBEE MUNGU AMPE MAISHA MAREFU NA AENDELEE KUTIBU WATU WA MUNGU.BABU UBARIKIWE SANAAAAAAAAAAAA A
Quote

+1 #8 MPERAMPERA 2011-03-15 14:21 NATIONAL INSTITUTE OF MEDICAL RESEARCH mnasema je? na wakemeaji mbona kimya? Ndodi vipi inahitajika gharama kiasi gani kutibu kisukari? Mchungaji Kakobe kama unavyofahamika maombi bila dawa ni usanii au? Mch.lwakatere vipi mbona hatukusikii
Quote

-1 #7 albert 2011-03-15 12:37 lUKUVI HANA NENO MWENYWE KUULIZWA NI YULE WAZIRI WA AFYA ALIYETAKA KUMKATIZA BABU ASITOE HUDUMA WATU WAENDELEE KISA NI KUONA WIZARA YAKE ITAHAMISHIWA KWA BABU,AMA KUTAKA BABU ATOE KIDOGO AMA ALIPIEE [TRA]HAWAJUI HUYO NI MTUMSHI WA MUNGU HAMNAGA CHAKACHUA NI UKAPATE KIKOMBE KUTOKA KWA MKONO WAKE MWENYEWE SIYO UKAJARIBU KUCHAKACHUA KUPITIA MLANGO WA NYUMA,HAKUNA KABISAAAA UFIJARIBU TU MAMBO YANAKUENDEA VIBAYA KUNA WATU WAMESHAZOEA VITU VYA MLANGO WA NYUMA,PIA NAPENDA KUWAONYA KWA WALE WATAKAOKWENDA KUTOA MSAADA KWA BABU WAJUE NAO SIYO KWENDA KUJITAFUTIA MAISHA KUTOKANA NA MKONO WA BABU WASIJARIBU,NI VEMA USIJARIBI YATAKUTOKEA PUANIPALE NI NGUVU NA MIUJIZA YA MUNGU.ANGALI JAPAN MAMBO GANI YAMETOKEA?HIYO YOTE NI MIUJIZA YA MUNGU,NA HII DAWA NI MIUJIZA YA MUNGU YA KUONA VILE WATU WANAPATA SHIDA NA KUFA,AKAMCHAGUA MTUMSHI WAKE MMOJA NA KUWEZA KUWALISHA MAMILIONI YA WATU BILA KUCHOKA BILA KULIPISHA MALIPO MENGI ILA NI ILE SADAKA YAKE YA KANISA.WEWE UNAYE TAKA KUKATIZA HUDUMA YAKE BABU SHINDWA KWA JINA LA YESU NA HUENDE KUTUBU,NA KUMWOMBA MSAMAHA BABU KWANI NI MADHARAU KUMDHARAU MTUMISHI WA MUNGU.PIA NAPENDA UKAPATE HUDUMA KWA BABU KWANI WEWE INAONEKANA HALI YAKO SIYO MZIMA NI KATI YA WATU WALISHAKATA TAMAA NA MAISHA.WIZARA YA AFYA PAMOJA NA WAZIRI WA AFYA WANAPOSEMA WANATAKA KUIFANYIA UTAFITI WA HIYO DAWA TOKA HAPO MWANZONI WALIKUWA WAPI?KAMA ILIKUWA NI MBAYA NI WANGAPI UNGEKUTA WAMEUWAWA NA HIYO DAWA,MAWAZIRI WANGAPI WAMESHAPATA HIYP HUDUMA.NAOMBA BUNGE LIKIANZA HII WIZARA ISIMAMISHWE BABU APEWE KIPA UMBELE KWANZA,PIA MATOKEO YATAKUWA NA NA NAMBA KUBWA KWA WALE WOTE WAMEPONA,TUNAWE ZA KUPATA NAMBA YA WATU KUTOKANA NA USHUHUDA WAO NA KWA MADAKTARI WA MAHOSPITALI MBALI MBALI. WANANCHI MUWE NA IMANI WAKATI WA KUNYWA ILE DAWA NA UTAPONA KWANI NGUVU ZA MUNGU ZINAFANYA KAZI HAKUNA USHIRINA NDANI YAKE,HATA YESU ALIWALISHA WATU WAPATAO WANGAPI NA WOTE WAKAPATA UPONYAJI?NI IMANI YAKO NDIYO ITAKUPONYA TU KUWA NA IMANI NA MTUMISHI WA MUNGU NA SIKU ZAKO ZA KUISHI ZIONGEZEKE KAMA UMESHAKATA TAMAA NENDA UKAMWONE HUYO MTUMISHI WA MUNGU HATAKI MALI ZAKO WALA CHOCHOTE KWAKO NI ILE SADAKA YAKO MIA TANO TUUUUUUUUU NA HAPO UNAPATA UPONYAJI.MUNGU APEWE SIFA......AMEN....
Quote

0 #6 NOEL MARUNDA 2011-03-15 11:16 Ninaomba serikali itoe mchango mkubwa ili kumsaidia Babu wetu wa Loliondo kwani anasaidia wengi,
vitu vyenyewe ni:-
- Choo- kwani watu wanajisaidia kwenye makorongo
- Ulinzi uongezwe
- Wasitokee watu wataotumia uwepo wa Babu kujinufaisha wenyewe.
Quote

+1 #5 valuvalu 2011-03-15 09:31 sasa tulinganishe Lukuvi na Mponda nani ana vision ya kusolve mambo kistaarabu. Tunahitaji akina lukuvi wengine.
Quote

+1 #4 TongoTongo 2011-03-15 09:12 Sasa hivi kuna improvement kubwa sana ktk utoaji huduma. Watu wanaondoka leo wanarudi kesho yake mchana au jioni. hii ni ishara ya kwamba serikali ikiamua inaweza, sijui kwanini kwenye Umeme kuna GUGUMIZI...
Quote

+1 #3 lupogo 2011-03-15 08:27 HONGERA MCHUNGAJI! Hongera pia kwa serikali kwa kumpa sapoti!
Quote

+2 #2 MWAYA 2011-03-15 07:57 Tunampenda Ndesamburo kwa sababu anatusaidia shida zetu. Ni Ndesamburo tu, 2015. Asante Baba!
Quote

+1 #1 Mangi Lelo 2011-03-15 07:24 Mzee fanya kazi ya kujenga Barabara za Bondeni ndio muhimu wachana hiyo hila za CCM ya ku divite mambo..
Quote
 
PHP:
Kaka 
 
Sio kwa vile hii sredi haihusishi mwanamke na mwanaume basi ndio tuseme haistahili hapa au haina mahusiano, hapana.
Mahusiano yapo kwa uponyaji wa Babu na Watu wanaoenda kwake.
So kitendo cha watu kukutana na kubadilishana mawazo, au kusaidiana tayari ni uhusiano
Nimejitahidi kuelezea jaman
Ninashukuru kwa mchango huu wa busara.......................sijui kwa nini baadhi ya wenzetu ukianza kugusa masuala ya vvu ambayo yanatokana na mahusiano wanatafuta hoja nyepesi za kufunga mjadala........................

vvu ni matunda ya mahusiano na tiba zake zipo kwenye mkondo huo huo wa kuimarisha au kudhoofisha mahusiano..............
 
Hapo umenena mkuu hasa hapo kwenye bluu
 
Lisemwalo lipo na kama halipo ipo siku litatokea. Yawezekana kweli babu anaponya mie bado najiuliza kama haponyi mbona kuna msululu kibao wa watu!!!
Mungu azidi mbariki Babu na wagonjwa wote
 
Lisemwali lipo na kama halipo ipo siku litatokea. Yawezekana kweli babu anaponya mie bado ajiuiza kama haponyi mbona kuna msululu kibao wa watu!!!
Mungu azidi mbariki Babu na wagonjwa wote

Hapo sasa my dia
Yaani watu wazima na nyazifa zao wakiwemo mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, viongozi wa dini na vyama vya siasa bila kusahau mabalozi na wengine kibao kutoka South Afrika na Europe wanamimikika Loliondo kupoteza muda tu????
Yaani sio tu kwamba haiingii akilini, pia hata haieleweki
 
My dia hiki ni kitendawili kikubwa sana, mie naamini kweli babu anaponya!!! ngoja nijikusanye nami nikamuone ila tatizo langu ni low pressure hope nitapona!
 
My dia hiki ni kitendawili kikubwa sana, mie naamini kweli babu anaponya!!! ngoja nijikusanye nami nikamuone ila tatizo langu ni low pressure hope nitapona!

Kwanini usipone my dia!??

Nenda kapate kikombe halafu uje uniambie,
Tena kwa jina lako lilivyokaa ki-utakatifu takatifu yaani ndo kabisaaaaaaaaa
Fasta unashuka Moto wa kusambaratisha mapresha yote uliyonayo
 
Lowassa apata kikombe Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 23:47

Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.
Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile."Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole," alisema Lowassa na kuuliza: "Kwani hiyo nayo ni habari jamani?"
Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini ambao wameshafika kwa mchungaji huyo kupata tiba hiyo wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya.

Katika jitihada za kudhibiti usalama na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma kwa mchungaji huyo bila matatizo, Serikali imeimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), katika kijiji hicho na kusimamia magari. Pia imepeleka wauguzi kusaidia wagonjwa mahututi kabla ya kumfikia mchungaji na imetoa pia jenereta kwa ajili ya kufua umemeKaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymond Mushi alisema jana kuwa, sasa walau hali ni nzuri kwani msongamano umepungua.

"Ni kweli sasa hali inaridhisha na jana watu wamekwenda kupata tiba na kurejea makwao mapema hili ndilo serikali inalolitaka. Tunaomba watu wanaopeleka wagonjwa wawe wanauliza kwanza hali ya msongamano," alisema Mushi.Mushi alisema inawezekana watu wanaokwenda katika kijiji hicho kusubiriana katika Mji wa Mto wa Mbu ambako kuna huduma nyingi muhimu kuliko wote kwenda huko kwa wakati mmoja.

Alitoa wito kwa watu wenye wagonjwa mahututi kuacha kuwapeleka moja kwa moja kwa mchungaji huyo kabla ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao.Katika hatua nyingine, wagonjwa kadhaa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wameanza kutoroka wodini na kwenda Loliondo kupata matibabu ya magonjwa sugu yanayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile, Mwananchi imeelezwa.
Habari zilizopatikana hospitalini hapo jana zimeeleza kuwa wagonjwa hao walianza kuondoka Muhimbili juma lililopita baada ya Serikali kubariki matibabu hayo. Ofisa mmoja mwandamizi wa hospitali hiyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, amesema kuwa wakati baadhi ya wagonjwa hao wakiwa wanatoroka wodini, wengine wamekuwa jasiri kwa kuwaaga madaktari wao.
"Wagonjwa wameanza kuondoka na wengine bila hata ya kuaga, hivyo hatujui hatima yao kama watafika salama huko Loliondo," alisema.Ofisa huyo alisema juma lililopita, mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa chumba namba 15 katika Wodi ya Kibasila, aliondoka baada ya kusikia taarifa kuhusu huduma hiyo.
"Kuna mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa Kibasila Wodi namba 15 aliondoka aliposikia kuwa Babu ameanza tena kutoa matibabu hayo ambayo awali yalisitishwa," alisema.Hata hivyo, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaisha alisema hana taarifa za kutoroka wodini kwa wagonjwa hao na kwenda kufuata tiba huko Loliondo... "Sina taarifa zozote za kuondoka kwa wagonjwa hapa hospitalini."

Matibabu Loliondo yapandisha nauli Ubungo
NAULI za kwenda Arusha kutoka Ubungo, Dar es Salaam zimepanda kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na wingi wa wasafiri wanaoelekea Loliondo kupata tiba hiyo ya magonjwa sugu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka kituoni hapo zimeeleza kuwa, nauli hizo zimepanda kutoka Sh18,000 hadi Sh30,000 tangu juma lililopita.
Mmoja wa mawakala wa mabasi ya abiria katika kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ongezeko hilo la nauli limetokana na baadhi ya mawakala kukodi mabasi na kuwasafirisha abiria."Nikupe siri moja tu ambayo inatufanya tupandishe nauli. Lengo letu ni kupata faida, ujue sisi tunakodi basi zima kisha tunakatisha tiketi kwa bei yetu ili na sisi tupate faida," alisema.

Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Arusha, Charles Manyama alisema mabasi yaendayo huko yamegawanyika katika madaraja matatu yale ya bei ya juu, bei ya kati na bei ya chini lakini kwa sasa bei imekuwa ni moja kwa mabasi yote.
Kwa mujibu wa abiria huyo, zamani nauli za Arusha zilikuwa Sh25,000 kwa basi la daraja la juu, Sh18,000 kwa mabasi ya daraja la kati na Sh15,000 kwa daraja la chini, lakini sasa mabasi yote yanatoza kati ya Sh25,000 hadi Sh30,000."Mawakala hawa wanadhani kila mtu anayepanda magari haya anakwenda Loliondo lakini siyo kweli, wengine tuna safari nyingine kabisa," alisema Manyama na kuongeza:

"Unakuta bei zinashangaza na kupanda sana. Hata hivyo, inashangaza kuona wanadamu tunakosa utu. Watu wanakwenda kupata matibabu wanapandishiwa nauli, walipaswa kuwaonea huruma wagonjwa hawa," alisema Manyama.Jitihada za kumtafuta Meneja wa kituo cha mabasi Ubungo ziligonga mwamba baada ya taarifa kutoka ofisi kwake kueleza kuwa alikuwa nje kikazi.

Polisi Arusha wadhibiti usafiri wa Loliondo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha kuweka vituo vinavyotambulika kwa ajili ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu kwa Mchungaji Mwasapile ili kuepuka utapeli.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu kutaka kwenda Loliondo, kumezuka vituo vingi ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha utapeli kwa watu wanaotoka mikoani."Nafahamu hili ni jambo ambalo manispaa wanahusika nalo, wahakikishe kuwa hakuna vituo visivyo rasmi ili wananchi wasije kudanganywa na watu wabaya," alisema.

Katika kituo kilichoibuka ghafla baada tiba ya magonjwa sugu kuanza kutolewa cha Chini ya Mti, kulizuka vurugu za madereva na madalali waliokuwa wakibishania kiwango cha nauli, hatua iliyosababisha polisi wenye silaha kupelekwa katika eneo hilo.
Hatua ya polisi kuonekana katika kituo hicho, ilisababisha wasiwasi kwa wananchi kuwa huenda Serikali imesimamisha utaratibu wa wananchi kwenda Loliondo, jambo ambalo kaimu kamanda huyo alilikanusha.

"Tunachokifanya ni kuweka utaratibu mzuri, polisi wanasimamia sheria. Magari mengine yanazidisha idadi ya watu na kutoza pesa nyingi zaidi. Sumatra wakisema nauli sahihi ni kiwango fulani na madereva wakizidisha basi tunawakamata," alisema.
Wananchi waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao walisema kuwa wanashangazwa na bei ya nauli kuwa juu hata baada ya Serikali na KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati kuboresha mazingira ya kuwahi kupata tiba na kuondoka kijijini Samunge.

"Mwanzoni walikuwa wanasema magari yanakaa sana huko, kwa hiyo wanafidia hizo siku za kungoja wagonjwa lakini sasa hivi ukienda leo unarudi kesho na nauli bado iko juu," alisema mmoja wa wananchi hao.Nauli ya kutoka Mjini Arusha hadi Samunge, Loliondo ni Sh100,000 kwenda na kurudi kwa magari aina ya Land Cruser ,huku nauli ya mabasi ikiwa pungufu zaidi.
Habari hii imeandaliwa na Nevile Meena, Ibrahim Yamola, Dotto Kahindi Dar na Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Arusha

Comments

0 #5 Bakari 2011-03-16 04:57 Kulikuwa na umuhimu gani kwa Lowassa kwenda na viongozi wa DINI? Hiki ni kiashiria jinsi viongozi wa CCM walivyokumbatia UDINI.

Na ndio sababu ya wao kutumia UDINI kusambaratisha vyama vinavyotoa upinzani wa kweli.
Quote

+1 #4 matongo matongo 2011-03-16 03:45 hahahahaaaaaaaa aa.......... mwamba umenifurahsha sana, kweli ccm inatakiwa ikapate kikombe ina magonjwa mengi sana ya sugu
Quote

0 #3 milindim- Nagasaki 2011-03-16 02:17 Wakubwa shikamoo, wadogo salam.Nadhani Wagonjwa wa radiation wa hapa Japan watakuja huko.
Quote

+2 #2 mwamba 2011-03-16 00:59 INAONEKANA VIONGOZI WENGI NI WAGONJWA,LAKINI WANGEKUWA WANATAJA MAGONJWA YALIOKUWA YANAWASUMBUA ILI WATAKAPOPONA WAONESHE VYETI VYA UTHIBITISHO..CCM INATAKIWA IKAPATE KIKOMBE KWANI INA MAGONJWA SUGU MENGI
Quote

0 #1 valuvalu 2011-03-16 00:53 safi sana!imarisha afya baba ili ujiandae kuchakachua wenzako mzee wa ndege ya uchumi inapaa.
 
Lowassa apata kikombe Loliondo Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 23:47

Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.
Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”
Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini ambao wameshafika kwa mchungaji huyo kupata tiba hiyo wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya.

Katika jitihada za kudhibiti usalama na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma kwa mchungaji huyo bila matatizo, Serikali imeimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), katika kijiji hicho na kusimamia magari. Pia imepeleka wauguzi kusaidia wagonjwa mahututi kabla ya kumfikia mchungaji na imetoa pia jenereta kwa ajili ya kufua umemeKaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymond Mushi alisema jana kuwa, sasa walau hali ni nzuri kwani msongamano umepungua.

"Ni kweli sasa hali inaridhisha na jana watu wamekwenda kupata tiba na kurejea makwao mapema hili ndilo serikali inalolitaka. Tunaomba watu wanaopeleka wagonjwa wawe wanauliza kwanza hali ya msongamano," alisema Mushi.Mushi alisema inawezekana watu wanaokwenda katika kijiji hicho kusubiriana katika Mji wa Mto wa Mbu ambako kuna huduma nyingi muhimu kuliko wote kwenda huko kwa wakati mmoja.

Alitoa wito kwa watu wenye wagonjwa mahututi kuacha kuwapeleka moja kwa moja kwa mchungaji huyo kabla ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao.Katika hatua nyingine, wagonjwa kadhaa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wameanza kutoroka wodini na kwenda Loliondo kupata matibabu ya magonjwa sugu yanayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile, Mwananchi imeelezwa.
Habari zilizopatikana hospitalini hapo jana zimeeleza kuwa wagonjwa hao walianza kuondoka Muhimbili juma lililopita baada ya Serikali kubariki matibabu hayo. Ofisa mmoja mwandamizi wa hospitali hiyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, amesema kuwa wakati baadhi ya wagonjwa hao wakiwa wanatoroka wodini, wengine wamekuwa jasiri kwa kuwaaga madaktari wao.
“Wagonjwa wameanza kuondoka na wengine bila hata ya kuaga, hivyo hatujui hatima yao kama watafika salama huko Loliondo,” alisema.Ofisa huyo alisema juma lililopita, mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa chumba namba 15 katika Wodi ya Kibasila, aliondoka baada ya kusikia taarifa kuhusu huduma hiyo.
“Kuna mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa Kibasila Wodi namba 15 aliondoka aliposikia kuwa Babu ameanza tena kutoa matibabu hayo ambayo awali yalisitishwa,” alisema.Hata hivyo, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaisha alisema hana taarifa za kutoroka wodini kwa wagonjwa hao na kwenda kufuata tiba huko Loliondo... “Sina taarifa zozote za kuondoka kwa wagonjwa hapa hospitalini.”

Matibabu Loliondo yapandisha nauli Ubungo
NAULI za kwenda Arusha kutoka Ubungo, Dar es Salaam zimepanda kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na wingi wa wasafiri wanaoelekea Loliondo kupata tiba hiyo ya magonjwa sugu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka kituoni hapo zimeeleza kuwa, nauli hizo zimepanda kutoka Sh18,000 hadi Sh30,000 tangu juma lililopita.
Mmoja wa mawakala wa mabasi ya abiria katika kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ongezeko hilo la nauli limetokana na baadhi ya mawakala kukodi mabasi na kuwasafirisha abiria.“Nikupe siri moja tu ambayo inatufanya tupandishe nauli. Lengo letu ni kupata faida, ujue sisi tunakodi basi zima kisha tunakatisha tiketi kwa bei yetu ili na sisi tupate faida,” alisema.

Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Arusha, Charles Manyama alisema mabasi yaendayo huko yamegawanyika katika madaraja matatu yale ya bei ya juu, bei ya kati na bei ya chini lakini kwa sasa bei imekuwa ni moja kwa mabasi yote.
Kwa mujibu wa abiria huyo, zamani nauli za Arusha zilikuwa Sh25,000 kwa basi la daraja la juu, Sh18,000 kwa mabasi ya daraja la kati na Sh15,000 kwa daraja la chini, lakini sasa mabasi yote yanatoza kati ya Sh25,000 hadi Sh30,000.“Mawakala hawa wanadhani kila mtu anayepanda magari haya anakwenda Loliondo lakini siyo kweli, wengine tuna safari nyingine kabisa," alisema Manyama na kuongeza:

"Unakuta bei zinashangaza na kupanda sana. Hata hivyo, inashangaza kuona wanadamu tunakosa utu. Watu wanakwenda kupata matibabu wanapandishiwa nauli, walipaswa kuwaonea huruma wagonjwa hawa,” alisema Manyama.Jitihada za kumtafuta Meneja wa kituo cha mabasi Ubungo ziligonga mwamba baada ya taarifa kutoka ofisi kwake kueleza kuwa alikuwa nje kikazi.

Back
Top Bottom