Huyu baba mwenye nyumba vipi?

Huyu baba mwenye nyumba vipi?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Baba mwenyenyumba alipata mpangaji, kijana aliyetokea kijijini kwenda kutafuta maisha. Msimu ule alivuna mahindi na mihogo, aliuza vyakula vile na kujifungasha na pesa aliyoipata akiwa amechoka kushika jembe kila siku.

Alipofika mjini siku za kwanza aliishi katika nyumba ya wageni, hakuwa na mtu yeyote aliyemfahamu pale mjini, alianza mazoea na wahudumu wa guest, aliwauliza ni vipi anaweza kupata chumba. Si muda mrefu alipata chumba kwa masharti ya kulipa kodi ya miezi sita mbele.

Akiba aliyokuwa nayo ikianza kuyeyuka alihamia kwenye chumba na kufanikiwa kununua mahitaji ya muhimu kama ndoo, sufuria, sahani, jiko na vinginevyo. Akaanza kutafuta kazi mjini, kila akizunguka, nauli, pesa ya kula ndiyo akiba inavyozidi kuyeyuka.

Kabla hajakaa vizuri, miezi sita ilikuwa imekatika bila kupata ajira ya kueleweka ilhali anatakiwa alipe kodi. Aliugua homa kali sana, siku tatu alikuwa chumbani kwake hajatoka nje, mwenye nyumba aliuliza wapangaji wengine kama walimuona, mlango uligongwa lakini jamaa alishindwa kufungua, ilibidi mlango uvunjwe na majirani walichukua tax mpaka hospitali, kwakweli alilazwa kwa drip za maji, hali yake ilikuwa dhoofu sana.

Mwenye nyumba akiwa ameweka mikono kichwani, anauliza madaktari kila dakika, jamaa atapona? Walimuonea huruma sana, wakamwambia kama unauchungu hivi na ndugu yako, kwanini ulimchelewesha hospitali, alijibu kwa nguvu mimi si mfahamu huyu mtu, ninaomba apone ili anilipe kodi yangu. Madaktari walibaki wanahamaki.
 
kweli pesa imekua ngumu sana mpaka baba mwenye nyumba anahofu kudhulumiwa na pango la nyumba
 
Tena hofu yake ni kifo kisisababishe yeye kukosa pango. Ajira zimekuwa ngumu sa siku hizi, hata zile kazi za kuchanganya zege zamani ukianzia Sinza, Mwenge, Mbweni, mpaka Boko zilikuwa za kumwaga, siku hizi wajenzi si wengi.
 
Baba mwenyenyumba alipata mpangaji, kijana aliyetokea kijijini kwenda kutafuta maisha. Msimu ule alivuna mahindi na mihogo, aliuza vyakula vile na kujifungasha na pesa aliyoipata akiwa amechoka kushika jembe kila siku.

Alipofika mjini siku za kwanza aliishi katika nyumba ya wageni, hakuwa na mtu yeyote aliyemfahamu pale mjini, alianza mazoea na wahudumu wa guest, aliwauliza ni vipi anaweza kupata chumba. Si muda mrefu alipata chumba kwa masharti ya kulipa kodi ya miezi sita mbele.

Akiba aliyokuwa nayo ikianza kuyeyuka alihamia kwenye chumba na kufanikiwa kununua mahitaji ya muhimu kama ndoo, sufuria, sahani, jiko na vinginevyo. Akaanza kutafuta kazi mjini, kila akizunguka, nauli, pesa ya kula ndiyo akiba inavyozidi kuyeyuka.

Kabla hajakaa vizuri, miezi sita ilikuwa imekatika bila kupata ajira ya kueleweka ilhali anatakiwa alipe kodi. Aliugua homa kali sana, siku tatu alikuwa chumbani kwake hajatoka nje, mwenye nyumba aliuliza wapangaji wengine kama walimuona, mlango uligongwa lakini jamaa alishindwa kufungua, ilibidi mlango uvunjwe na majirani walichukua tax mpaka hospitali, kwakweli alilazwa kwa drip za maji, hali yake ilikuwa dhoofu sana.

Mwenye nyumba akiwa ameweka mikono kichwani, anauliza madaktari kila dakika, jamaa atapona? Walimuonea huruma sana, wakamwambia kama unauchungu hivi na ndugu yako, kwanini ulimchelewesha hospitali, alijibu kwa nguvu mimi si mfahamu huyu mtu, ninaomba apone ili anilipe kodi yangu. Madaktari walibaki wanahamaki.
Hadithi yako nzuri,aliyekufundisha alikwambia ina maana gani vile?
 
Dunia tambara bovu ndugu zangu.
Utu umetoweka kabisa, Mungu atusaidie tubadilike jamani.
 
Hadithi nzuri sana, nadhani mods waanze kufikiria kuweka jukwaa la hadithi
 
Baba mwenyenyumba alipata mpangaji, kijana aliyetokea kijijini kwenda kutafuta maisha. Msimu ule alivuna mahindi na mihogo, aliuza vyakula vile na kujifungasha na pesa aliyoipata akiwa amechoka kushika jembe kila siku.

Alipofika mjini siku za kwanza aliishi katika nyumba ya wageni, hakuwa na mtu yeyote aliyemfahamu pale mjini, alianza mazoea na wahudumu wa guest, aliwauliza ni vipi anaweza kupata chumba. Si muda mrefu alipata chumba kwa masharti ya kulipa kodi ya miezi sita mbele.

Akiba aliyokuwa nayo ikianza kuyeyuka alihamia kwenye chumba na kufanikiwa kununua mahitaji ya muhimu kama ndoo, sufuria, sahani, jiko na vinginevyo. Akaanza kutafuta kazi mjini, kila akizunguka, nauli, pesa ya kula ndiyo akiba inavyozidi kuyeyuka.

Kabla hajakaa vizuri, miezi sita ilikuwa imekatika bila kupata ajira ya kueleweka ilhali anatakiwa alipe kodi. Aliugua homa kali sana, siku tatu alikuwa chumbani kwake hajatoka nje, mwenye nyumba aliuliza wapangaji wengine kama walimuona, mlango uligongwa lakini jamaa alishindwa kufungua, ilibidi mlango uvunjwe na majirani walichukua tax mpaka hospitali, kwakweli alilazwa kwa drip za maji, hali yake ilikuwa dhoofu sana.

Mwenye nyumba akiwa ameweka mikono kichwani, anauliza madaktari kila dakika, jamaa atapona? Walimuonea huruma sana, wakamwambia kama unauchungu hivi na ndugu yako, kwanini ulimchelewesha hospitali, alijibu kwa nguvu mimi si mfahamu huyu mtu, ninaomba apone ili anilipe kodi yangu. Madaktari walibaki wanahamaki.
Mwenye nyumba atakuwa Mchagga.
 
Hiyo stori ni ya uongo maana umesema kodi alilipa miezi 6
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom