Huyu Baba Mkwe atanivunjia Ndoa

Huyu Baba Mkwe simuelewi kabisa, saa sita au saba usiku eti anampigia simu bintie, kha, umelala usingizi unashtuka simu inaita au mtu anaongea na simu, haya mwenzetu nani huyo usiku huu, oooh Baba anatusalimia!!! Saa hizi!!!

Haya kuna siku kaja, mmmh niko zangu job wife yeye karudi mapema ile narudi namkuta Mkwe kavaa pensi tu miguu iko juu ya sofa mgongo uko chini ya sakafu kwenye jamvi, bintiye yuko sofa ya jirani wanapiga story!!!!!! Sina mawazo mabaya but huyu dingi jamani na hii mikao yake mbele ya binti yake!!! Yaani umevaa pensi halafu miguu juu, kweli si maeneo yote hatarishi yanakua exposed???

Mara oooh wewe Suzy wewe (Ni Housegirl-sio jina lake halisi) nataka nikuoe, nataka Mama fulani (mke wangu) nimtafutie Mama mdogo, naona wewe unafaaa....kwakweli ananinyima raha bhana, yaani mtu aje kwenye himaya yako halafu anaongea huu mchuzi huu, ahaaaaa

Haya kama kawaida yake, muda wa kuondoka lazima ampetipeti mke wangu, mara ooh baba fulani wewe pumzika tu subiri mama nanihii anisindikize.....mmmh haya basi Mama msindikize kwa gari baba hadi hapo kituoni, eti hapana ngoja tutembee tu, kuanzia saa moja kasoro hadi saa mbili ndio anarudi kumsindikiza baba, distance ya dakika kumi hadi kituoni????

Jamani, jamani sihisi chochote but huyu Dingi huyu nitakuja kumkata kidevu, Nice weekend,

Una wasiwasi wa nini? hujiamini? au kwani ni vibaya kula kuku na mayai yake?
 
Inaelekea unatoka katika familiar Baba akiingia hata sisimizi anafyata mkia. Hukuwa na chance ya kucheka, kuongea mazungumzo ya kawaida na hata kutaniana na Baba. Akiondoka ndiyo vicheko na maongezi. Lakini mwenzako hakutoka huko.
Ni lazima tukubali tofauti zetu ili kuepuka migongano isiyo ya lazima
 
Haahaaa kuna baadhi ya madingi tz yamekengeuka, mkuu kuwa makini, hapo kama hajamtafuna basi anataka kumtafuna!

Mwambie mkeo kwasauti kiume kuwa ni MARUFUKU kuchekacheka na baba yake, MARUFUKU baba yake kumpigia simu usiku labda kuwe na msiba hata hivyoo akitaka kupiga basi apige kwenye namba yako!

Kuna kaugonjwa umekalea wewe mwenyewe mkuu, HATA siku moja usimrusu mkeo amsindikize mkweo!

Labda nikufahamishe, kwa imani yangu ya Kirasta Fari na mila ya kabila langu la Kizanaki ni kuwa mwanamke akishaolewa mamlaka na udhibiti WOTE unakuwa kwa mumewe,

Wazazi wake chochote wanachotaka kumwambia au kukifanya kwa binti yao (mke wangu) ni lazima wapate kibali kwangu!

Mkuu badili mfumo wako wamaisha, MPIGE marufuko mkweo kuja hapo kwako bila sababu maalumu na akihitaji kuja kuongea na mwanae aombe kibali kwako na ikiwezekana shinda zake zote azifikishe kwako na wewe ndio utaamua kumfikishia mkeo!

NB
Tambua kuwa huyo ni MKEO wako wewe, wewe ndio mwenye mamlaka ya mwisho iwe mbinguni ama duniani! Ukisema NO na iwe NO kweli!

Ukicheka na NYANI utavuna mabua mkuu!

mwetu omuheri amang'ana amarito,omuroyo nduzi ana mang'ana gyakyana
 
Mkuu hapo ni kwako bana you are the only commander in chief hakuna mkwe wala baba yako mzazi.....

Set the rules na wengine lazima wafuate....usikose adabu ila lazima baba wa nyumba ajulikane

Mkeo mchane laivu kuwa anakuboa na mambo yake ya uzungu na huyapendi na anatakiwa aache......

By the way mume ndo kiongozi wa familia na una haki na wajibu wa kuongoza kwa matakwa yako bila kuathiri wengine.......na saa nyingine you shud be a dictator
 
Kaka Elli,,pole kwa maumivu ya kiakili
::
Jaribu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu uzito wa ukaribu wao,kabla ya kuchukua uamuzi mzito.
::
Mwambie mkeo apunguze mawasiliano,hususani nyakati za usiku,kama atabisha sana weka mashaka.Na ni vema ukawaweka wazi wote pamoja.Simama vema kama kichwa cha familia.
::
Tone moja la maji laweza kuleta gharika ktk familia.Nakumbuka mzee mmoja na mvi zake,hakuwa na mke,siku nilipomuuliza alinisimulia ambavyo alimfukuza mke wake alipobaini mkewe kubebeshwa mimba na mkwe wake,mke alipokiri alimfukuza na kujutia kudekeza ukaribu aliokuwa nao mkewe na bintie.
::
Jitahidi kama hali inaruhusu,uwe mbali na wakwe zako itakusaidia kuepuka migogoro isiyo ya lazima hasa kukugombanisha na mkeo.
=
 
Haahaaa kuna baadhi ya madingi tz yamekengeuka, mkuu kuwa makini, hapo kama hajamtafuna basi anataka kumtafuna!

Mwambie mkeo kwasauti kiume kuwa ni MARUFUKU kuchekacheka na baba yake, MARUFUKU baba yake kumpigia simu usiku labda kuwe na msiba hata hivyoo akitaka kupiga basi apige kwenye namba yako!

Kuna kaugonjwa umekalea wewe mwenyewe mkuu, HATA siku moja usimrusu mkeo amsindikize mkweo!

Labda nikufahamishe, kwa imani yangu ya Kirasta Fari na mila ya kabila langu la Kizanaki ni kuwa mwanamke akishaolewa mamlaka na udhibiti WOTE unakuwa kwa mumewe,

Wazazi wake chochote wanachotaka kumwambia au kukifanya kwa binti yao (mke wangu) ni lazima wapate kibali kwangu!

Mkuu badili mfumo wako wamaisha, MPIGE marufuko mkweo kuja hapo kwako bila sababu maalumu na akihitaji kuja kuongea na mwanae aombe kibali kwako na ikiwezekana shinda zake zote azifikishe kwako na wewe ndio utaamua kumfikishia mkeo!

NB
Tambua kuwa huyo ni MKEO wako wewe, wewe ndio mwenye mamlaka ya mwisho iwe mbinguni ama duniani! Ukisema NO na iwe NO kweli!

Ukicheka na NYANI utavuna mabua mkuu!

....kabla hujaufuata huu ushauri jiulize mkeo akipiga marufuku wazazi wako utaichukulia vipi.....unless kama unajiandaa kutengenezq ufa kwenye ndoa yako..........
 
.....zungumza na mkeo kwa upole na kiutani ila mfikishie hofu yako.....atakuelewa.........
 
tatizo ni mazingira yanayojitokeza baina ya mtoto na baba mtu,ni vizur mife akuweke wazi ,hawezekani kuvaliana vipensi!
 
....kabla hujaufuata huu ushauri jiulize mkeo akipiga marufuku wazazi wako utaichukulia vipi.....unless kama unajiandaa kutengenezq ufa kwenye ndoa yako..........

Haijalishili, lakini vivyo hivyo na wazazi wangu (hasa mama)wakitaka kuwasiliana na mimi waanzie kwanza kwa mke wangu tena wamuombe!
 
nimecheka naikwajaribu kulivaa hilo picha nikajikuta nacheka sana anakaa na pensi kwenye nyumba yako tena miguu juuu???????? kha swali mkeo ni mhindi??? hawa ndio wanatafunana baba na bintie kama sio ndugu mimi ni mtoto wa kike huo ukaribu na baba siuamini wanaume ni mashetani sometimes hawajui mtoto wala nani anatafuna tu taratibu hujawahi sikia baba amembaka mtoto wake ??? si hawa hawa wanaume ??? acha ujinga Elli mimi nyumbani kwangu i hve pricniple awe baba awe mama kaa kwa heshma na sheria ullizozikuta usizivunje kabisa other wise will throuw u ut ujipitishe na kikanga kipensi weweweewe nitakuonya ukirudia nakufukuza bila kujali mama mkwe mama yangu baba yangu au yeyote .nashindwa kuelewa wewe na huyo mkeo ni kabila gani la kitanzania ambalo hamna adabu na utashi wakuona mbali .
nakuhakikishia hivi keshakulaga huyo wife wako sasa anajisahau kabisa ,na kashazoea anashindwa kujizua .
1.mpige marufuku kuja ndugu yyte bila taarifa yako!
2.ukimkuta huyo baba amekukalia mkao huo tena mwambie live mzee hivi ukinikuta pale kwako nimejiachia hivi utafurahi
3.mwambie mkeo hupendi hayo mazoea ya baba yake visimusimu nakusindikizana.muumsindikize wote kwani wanaongea nini na mke wa mtu ,acha ujinga wewe

UNATAKIWA UACT LIKE COMMANDER IN CHIEF OF THE HOUSE SAUTI YAKO IKISIKIKA KWELI WAJUE BABA AMEONGEA SIO KIJINGA JINGA TU UNACHEKA CHEKA TU NAKUNYAMAZA MIMI MUME WANGU AKIONGEA TU U KNOW FATHER OF THE HOUSE IS TALKING AKIJISAHAU NAMRUDISHA KWENYE MSTARI .CHEZEA MABUA UVUNE MAHINDI ANGALIA SANA TENA KAPIME WATOTO DNA KATI YAO NI WA BABA MKWE.
 
Last edited by a moderator:
Ndo RAHA YA KUOA WATOTO WA MASAKI HIYOOOO!!!!!!!! Dady! Dady! Dady! 24/7, Hata mkijamba humo ndani uatsika Dady!!!! Sio sie FATHER! Akirudi WOTE MNAKAA MIKAO YA KUJENGA TAIFA!!!!!!!!! Akiondoka ndo uuuuuuuuuh! Mnahema! FATHER KAMA CHLOROQUINE!!!!! Ukiolewa unasema THANKS GOD! Nitarudi nyumbani KUTEMBEA!!!!!!!! Kwako haji ngoooo! Usipomuibukia kumpa HI! Baaaaaaass!!!

Think on the postive side, siku hamna HELA YA MBOGA, Dady will JUMP IN TO HELP ASAP!!!!!!!!

mnhhhh....wewe mbona wa masaki pia?lol
 
Inaelekea unatoka katika familiar Baba akiingia hata sisimizi anafyata mkia. Hukuwa na chance ya kucheka, kuongea mazungumzo ya kawaida na hata kutaniana na Baba. Akiondoka ndiyo vicheko na maongezi. Lakini mwenzako hakutoka huko.
Ni lazima tukubali tofauti zetu ili kuepuka migongano isiyo ya lazima

where have u been?
karibuu
 
kuna baadhi tena asilimia kubwa ya watu humu wanajifanya ni liberalists ktk ushauri..na kupretend kwao kua liberalists kutawacost..amini hivyo jamaa..huyo mdingi ni chenga kama vp mpe makavu live naamin kabisa km bi mkubwa wako angekua anaibuka home kwako, full vimini, ma-calls kibao night wife angewaka..inabidi useme yaliyo moyoni jombaa..uzungu kitu gani, wakishua wapi unaweza kuta hata mlango wa ndege haujui..hamnaga swaga za namna hiyo dingi anakula mzigo huo...so mfungukie km vp alale mbele tu..ova
 
Yawezekana ni mazoea ya huko walikotoka, ila sisi kama jamii yafaa tulijadili kwa mapana zaidi. Mimi nashauri ujaribu kufanya utafiti wa chinichini na kupata background history ya maisha yao (Hapa lazima tuwekane sawa kwani yapo makabila ambayo bado yana tabia za kutembea na binti zao haswa kwa wale wenye imani ya utajiri wa kimazingira) Sikutishi ila hali kama hii nilishawahi kuiona katika mkoa fulani, na styre ya maisha ilikuwa hivyo hivyo hata baada ya binti yake kuolewa waliendeleza mahusiano, na kubwa zaidi hata mama wa huyo binti alikuwa hajui kama binti yake anatembea na baba yake. Watch out unaweza kujikuta unachangia chungu na baba mkwe wako.
 
Napata shida sana kuupokea ushauri wako, subiri siku nitamwambia mwanae kuwa sipendi tabia ya mzee

usimwambie mkeo bana utamfanya afikirie unawadhalilisha ye na baba yake na itamfanya akose amani na furaha tena
 
Back
Top Bottom