Huyu Baba Mkwe atanivunjia Ndoa

Ongea na wife mwambie unakosa amani pindi dingi anapojichetua nyumbani kwako

Mpe makavu live tena bila ya chenga
 
Ndoa Yako Ina Mda Gani?
Una Watoto Wangapi?
Mazoea Ya Mkeo Na Mama Yake(mkweo)Yakoje?

Pole Kiongozi!!
 
Huyu Baba Mkwe simuelewi kabisa, saa sita au saba usiku eti anampigia simu bintie, kha, umelala usingizi unashtuka simu inaita au mtu anaongea na simu, haya mwenzetu nani huyo usiku huu, oooh Baba anatusalimia!!! Saa hizi!!!

Haya kuna siku kaja, mmmh niko zangu job wife yeye karudi mapema ile narudi namkuta Mkwe kavaa pensi tu miguu iko juu ya sofa mgongo uko chini ya sakafu kwenye jamvi, bintiye yuko sofa ya jirani wanapiga story!!!!!! Sina mawazo mabaya but huyu dingi jamani na hii mikao yake mbele ya binti yake!!! Yaani umevaa pensi halafu miguu juu, kweli si maeneo yote hatarishi yanakua exposed???

Mara oooh wewe Suzy wewe (Ni Housegirl-sio jina lake halisi) nataka nikuoe, nataka Mama fulani (mke wangu) nimtafutie Mama mdogo, naona wewe unafaaa....kwakweli ananinyima raha bhana, yaani mtu aje kwenye himaya yako halafu anaongea huu mchuzi huu, ahaaaaa

Haya kama kawaida yake, muda wa kuondoka lazima ampetipeti mke wangu, mara ooh baba fulani wewe pumzika tu subiri mama nanihii anisindikize.....mmmh haya basi Mama msindikize kwa gari baba hadi hapo kituoni, eti hapana ngoja tutembee tu, kuanzia saa moja kasoro hadi saa mbili ndio anarudi kumsindikiza baba, distance ya dakika kumi hadi kituoni????

Jamani, jamani sihisi chochote but huyu Dingi huyu nitakuja kumkata kidevu, Nice weekend,

huyo lazma alikua anakula mayai yake
 
mmb, baba mke analala chini miguu mezani?
Kule nakotoka anayeweka miguu mezani ni baba mwenye nyumba tu.

Ndo haya haya, ya kupakata mabinti hadi walovunja ungo. Wanadhani baoloji ina macho?
 
Mwanangu Elli, kwanza pole kwa yanayokukuta. Pili ni kwamba hisia na shaka yako yana ukweli. Kutokana na neno na "hiyo mikoa yao" kama sikosei unaongelea mikoa ambayo baadhi ya mila zao ni chafu. Kuna uwezekano hapa kuna kitu kibaya kinafanyika. Nipe full CV ya huyo bi mkubwa hasa mkoa atokao nitasema mengi.
 
Kuna wazee wengine wa hovyo sana
Huyu ni mmoja wao hana maana kabisa!
 
Huyu Baba Mkwe simuelewi kabisa, saa sita au saba usiku eti anampigia simu bintie, kha, umelala usingizi unashtuka simu inaita au mtu anaongea na simu, haya mwenzetu nani huyo usiku huu, oooh Baba anatusalimia!!! Saa hizi!!!

Haya kuna siku kaja, mmmh niko zangu job wife yeye karudi mapema ile narudi namkuta Mkwe kavaa pensi tu miguu iko juu ya sofa mgongo uko chini ya sakafu kwenye jamvi, bintiye yuko sofa ya jirani wanapiga story!!!!!! Sina mawazo mabaya but huyu dingi jamani na hii mikao yake mbele ya binti yake!!! Yaani umevaa pensi halafu miguu juu, kweli si maeneo yote hatarishi yanakua exposed???

Mara oooh wewe Suzy wewe (Ni Housegirl-sio jina lake halisi) nataka nikuoe, nataka Mama fulani (mke wangu) nimtafutie Mama mdogo, naona wewe unafaaa....kwakweli ananinyima raha bhana, yaani mtu aje kwenye himaya yako halafu anaongea huu mchuzi huu, ahaaaaa

Haya kama kawaida yake, muda wa kuondoka lazima ampetipeti mke wangu, mara ooh baba fulani wewe pumzika tu subiri mama nanihii anisindikize.....mmmh haya basi Mama msindikize kwa gari baba hadi hapo kituoni, eti hapana ngoja tutembee tu, kuanzia saa moja kasoro hadi saa mbili ndio anarudi kumsindikiza baba, distance ya dakika kumi hadi kituoni????

Jamani, jamani sihisi chochote but huyu Dingi huyu nitakuja kumkata kidevu, Nice weekend,
swala hapo ni siyo kuhisi..... huyo mkwe wako hana adabu. tena wewe umemwachia sana. mimi wala nisingesema kupitia kwa binti yake. ningemsema mimi mwenyewe. kuwa amvalie kaptula mama lakini si ndani kwangu.wewe ni mkuu wa nyumba yako... wewe ndo unapanga watu wakae vipi waongee vipi wale saaa ngapi walale saa ngapi. baba akitaka avae kaptula kwake na aite binti yake wakapetiane huko. siyo kwako. ni dume jenzio hilo... au umeambiwa mkwe wako mkameruni?
 
Doubt any get many! Jaribu kuchunguza utajua kitu kinacho endelea!

Kwangu mimi hapo hakuna usalama hata kidogo cha kufanya ni kuwa macho wazi!
 
Mkuu Elli, Niungane na Yericko kwa kiasi kikubwa amenena vyema. Kuna kaukweli flani kuwa watoto wa KIKE hupenda sana kuwa karibu na Baba zao na watoto wa KIUME huwa karibu sana na mama zako. Lakini inabidi iwe katika limits flani kuwa huyu ni mzazi na huyu ni mtoto hata mtu asiyewafahamu akiwaona tu mlivyookaa au akiwasikilza ajue huyu ni mtu na mzazi wake, unaweza kuwakuta wengine ukadhani ni mtu na kiserengeti chake kumbe la.

Nakusihi utumie akili sana kusimamia misimamo yako, wife asijeakadhani unafanya hivyo labda umemuhisi vibaya na baba yake, nakuhakikishia atakuwa downhearted sana pengine ikaleta shida sana kati yenu. Mkwe akija kusalimu mpe nafasi ya kuzungumza na mwanawe, ila ni heshima/vyema wewe kumsindikiza kama upo.

Endelea kudadisi tabia za mkwe, pengine mkeo ndio mtu anayemwamini sana kwenye familia yake so huwa ndio msiri wake wa vitu vingi, who knows?, ila shetani siku hizi hazoeleki mkuu, mtu akimzoea sana lazima amuaibishe tu.
 
recodi alafu siku muoneshe mama mkwe mikao na anavo ongea hapo kwako. Je anakuwa hivo mukienda kwake pia?
pengine anafanya mapenzi na mwanawe. Mie nimeona kwa macho yangu jirani yetu alikuwa kama huyo bwana, mkewe akitoka analala na mwanawe.

Na mzee mwingine alifumaniwa na mwanawe.
Mtoto wake wakike aliolewa mkoani, alikuja kutembelea wazazi wake, (huyo mzee akijifanya mwenye dini sana), tulishangaa kusikia kafumaniwa na mwanae, aliemfumania ni mama, (yaani mkewe). Aibu, mama akadai talaka, mtoto akapewa talaka na mumewe, akakimbia kusiko julikana.
 
tatizo la watanzania/africs tunapenda sana copy and paste, kama huyu ni baba yake mzazi basi ni kosa sana na kama sio baba yake mzazi ni baba yake wa kufikia basi atakuwa anakula mtoto. Naomba uwe makini maana mazoea yakizidi sana siyo mazuri yanatakiwa yawe na mipaka
 
Sasa nimeamini kamba kabla hatujaoa lazima tufanye uchinguzi ......................... ndo matokeo yake haya. Ndo maaana wazee wa zamani walikuwa wanawachagulia vijana wao wake kutoka familia wanazozifahamu vizuri.
 
ukiingia ndani ukimkuta baba mkwe amekaa kiboya boya,unamchapa jicho moja kali sana,halafu sura ya mbuzi unapitiliza mpaka rum bila kumsalimia,unarudi kam dakika tano hivi ndo unamsalimia na sura ngumu,hakuna kucheka cheka hapo,akitaka kuondoka unasindikiza ww hakuna cha kumruhusu mke wako kutoka,halafu haumfikishi kituoni,ni hatua tatu tu unarudi,akipiga simu usiku mwambie mkeo asipokee,ikishakata mpigie wewe kwa namba yako umuulize anashida gani kupiga simu usiku,lazima ambwele mbwele,..problem solved
 
Una tatizo wewe binafsi!

... Hicho kinachookea hadi wewe kutilia shaka ni ishara ya vacuum ambayo tayari iko kati ya mkeo na wewe mwenyewe ... You should have filled it long before!!

... Kama wewe hupendi mienendo ya huyo Mzee ..Iweje Mkeo ..aendelee nayo? Hajui your likes and dislikes?

Where is your firm lovely character in all this??
 
Back
Top Bottom