Huwezi kuwa na Akili Timamu ukawa Mfuasi wa Mwanasiasa au Chama flan Daima. Haiwezekani kamwe.

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Huamini? trust me. ukiwa na akili timamu kabisa bila kujitoa ufaham huwezi ukawa mfuasi wa mwanasiasa flana au chama flan daima. ni ngumu. ngoja nikupe mifano.

1.miaka yoote tulikuwa tunaaminishwa kuwa kikwete ni mmoja ya marais wabovu(kitu ambacho ni kweli) lakini leo hii anaonekana ni mtu wa maana na watu wanamkumbuka kuwa alikuwa ni bora wakisahau kashfa za ufujaji wa pesa nyingi sana alizohusishwa nazo akiwa rais
2.miaka yote wapinzani walisema lowassa ni fisadi mzee wa watu akanyamaza wakapita huku na kule wakitangaza haabri hizo na kumuita majina yoooote mabaya.leo wapo naye wamesahau yooote waliyowah mtukana imekuwa ni zamu ya ccm kumtukana. hapo huoni nawe mfuasi utakuwa umeyumba kimsimamo?
3. mwakyembe aliandika waraka akielezea umuhimu wa serikali 3/1 lakini alikuja kuyakana maandiko yake yeye mwenyewe pale alipotakiwa kushabikia serikali mbili.kama ulikuwa unamwamini hapo kabla nawe si umeyumba?
4. nape alikuwa akipita na kutangaza magufuli ndo rais anayefaa kwa taifa hili na asiyeyumbishwa na watu , msafi n.k leo hii anapita mitandaoni na kwenye vyombo vya habari akilia lia ....
5. rais magufuli alisema yeye hatofuga wachafu na wenye kufoji vyeti katika serikali yake akitimua wafanyakazi mbalimbali serikalini lakini leo hii anaye mtu aliyefoji vyeti wanakaa naye pemben kwa pembeni kwenye mikutano hajamwondoa kwenye nafsi yake.kama ulimwamini huoni tayari unakosa msimamo?
6.mwakyembe alimhukumu lowassa pasipo kumsikiliza na kumpa nafasi ya kujieleza ila leo hii anamtetea makonda kuwa anapaswa asikilizwe ingawa ushahidi wote upo kuw alivamia kituo cha tv cha clouds. na alikwepa kuhojiwa. lakini mwakyembe hakuwa tayari kumhoji mtu aliyekuwa tayari kuhojiwa kuhusiana na suala la richmond. hapo unashangaa.
7.nape alishiriki kupitisha sheria ya kuvibana vyombo vya habari lakini leo hii yeye ndo mtumiaji sana wa vyombo hivi vya habari na pia akitaka kujitengenezea jina kupiia vyombo hivi.
8.liPumba alipigwa mabomu sana na ccm na akawa anawasema vibaya kumbe ukifika wakati wa uchaguzi anawasaidia kushinda. na sasa anatumika sana na ccm kwa ukaribu wa hali ya juu. unajiuliza aliyekuwa anasema ccm imekwisha na imelala mlalo wa mende ndo huyu huyu au mwingine? aliyekuwa ameamua kuijuluzu cuf ndo huyu huyu ambaye amerudi kuja kuongoza cuf?

na mengine mengi sana ambayo ukiyafuatilia utashangaa kwa nini ni ngumu kumuamini mwanasiasa. nimeamua kujiamini mimi mwenyewe na mambo yangu binafsi. acheni kushabikia wanasiasa na vyama. kama kuna hoja ya msingi simamia hoja na si nani kasema hiyo hoja kwa maana ya kuwa sababu ni yeye kasema basi atakuwa sahihi au ni sawa.
 
Yote ni kweli....
 
a good human being is the one who can change his atittude and life and decission according to time and invaroment .the one who do not alow his brain to be rigid
 
Ungetumia tu kiswahili ungeeleweka kuliko kutumia lugha usiyoifaham.
Decission?
Invaroment?
Alow?
Use.... The one who doesnt. Since you have used singular from the beginning. Hii lugha tuachie wenyewe ambao pamoja na kuifaham we always use swahili except when needed.

Back
Top Bottom