Huwezi kutawala Taifa kwa hisia, ila kwa hekima

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,196
11,231
Hisia nikitu hatari sana moyoni mwa kiongozi. Kiongozi akiwa na hisia Fulani au tawaliwa na hisia moyoni wakati wa maamuzi yake basi mara nyingi maamuzi hayo huwa na athari mbeleni. Hisia nikitu cha hatari kama ilivyo furaha. Ndio maana Una ambia huwezi fanya maamuzi ktk hisia ya furaha au huzuni.

Hisia inaweza kukufanya ukatamka neno likaumiza watu wengi au likawabariki Kwa muda mrefu. Hisia zakutaka mfano pinduliwa zitakufanya kukandamiza nakuwaumiza watu ukiamini hao ndio wabaya wako pasipo juwa haipo salama hata na wale wanakulamba miguu. Tangu kuwepo Kwa dunia hisia ndio chanzo cha maangamizi makubwa ya Binadam.

Hisia mbaya za Hitler kwa Mayahudi zilimfanya kutengeneza camp zakuwamaliza mayahudi. Kwa maelfu Yao. Watu walio Kuwa eng ya uchumi wa German wakajikuta wahanga wa mauwaji pasipo makosa.

Hisia mbaya ya Kuwa kila anaye fanikiwa ni mwizi na fisadi zaweza kulifanya Taifa kujikuta halina WAWEKEZAJI na watu kukimbia nchi na mwisho watu wako wengi wakakosa ajira.

Hisia za kuamini kwamba MTU anaye pinga wazi lako basi ni mhaini laweza kukufanya ukauwa watu wengi wasio na hatia Ila Tu wamekuwa na mawazo tofauti na wewe, ukasahau sio Raia Tu Ila hata ndani ya familia watoto au mke wanaweza Kuwa na mawazo tofauti na weww. Hisia ni zaidi ya boom la nyukilia ktk moyo wakiongozi.

Hisia zinaweza kukuaminisha kabla Fulani hawafai au dini Fulani hawafai Ila hauna ukweli wowote sema hisia ndio zina kuongoza na hisia ikisha kuongoza huwezi shaurika na huwo ndio ubaya wa hisia.

Hisia haina Jambo Jema siku zote ukiongozwa na hisia yule MTU anakupa wazo zuri utamchukia why hisia mbaya ulizo nazo juu yake. Tayari ubongo wako unasema Ibrahim ni mbaya akikushauri unakumbuka ubaya unao muwazia na sio ushauri anao kupa the tegemea maafa.

Hisia hisia ni hatari kiasi watu wenye hisia Wana angaliwa Kwa jicho la Tatu. Hisia ujenga chuki angalia Rwanda hisia mbaya Kati ya wahutu na watutsi walikatana mapanga na kuuwana Kwa ma million na mpaka Leo hisia inawatesa.

Hisia zakuamini wewe ni Bora kuliko wale wewe ndio Una akili kamwe hazitoweza kukufanya ufanye correct decision utafanya maamuzi Ila at the end unagunduwa Alaa kumbe kuna wenye akili kuliko Mimi. Hisia ni hatari Sana hisia zinafanya washauri wako kukuongoza vile hisia zako zinakuongoza . Nahapo ndipo unapokuja gunduwa huna wakukupinga kila MTU yes Mzee.

Hisia mbaya za Hayati Mugabe Kwa wakulima wakizungu nakuwafanyia ukatili nakuwafukuza akitawaliwa na wenye hisia kama zake walijikuta wakibeba pesa kwenye magunia kununua mkate na mwisho uchumi ukiharibika mpaka leo.

Hisia zakijinga za Ghadaffi kwenye makampuni ya mafuta nakubadilisha Sheria na kujipa serikali akiamini yupo salama zilifanya Taifa kuja umia pasipo sababu. Hisia hisia

Hisia za Nyerere Kwa walanguzi zilileta madhara makubwa Sana kiasi mpaka Leo maswali hajajibiwa. Na hii no baada ya kuja kigunduwa mlanguzi alikuwa mpaka ndani ya Taifa mbaya zaidi kwa viongoz wa kitaifa.

Vita Ile ambayo inalitesa Taifa mpaka leo ilikuwa ni Vita Kati ya walio nacho na wasio Kuwa nacho tuka dhulumu na Ile dhuluma mpaka Leo ina litesa Taifa.

Hisia ni mbaya Sana hisia ni hatari Sana moyoni mwa kiongozi
 
Hakika, na hizo hisia ndizo ninazoziona, sifanyi hiki kwa hawa kwa kua walinifanyia hiki, nafanya hiki kwakua huni ni nani hii, nk
Pia hisia za kuona mtu mmoja ndio mwenye maono na wengine wote hamnazo
 
Huna lolote wewe! Baada ya kutolewa kwenye system ya kula basi akili kidogo ulizokuwa umeshikiwa zimeanza kurudi!

Kumbuka ulivyokuwa unamtisha Ben Saanane kwamba ataliwa na Chatu akiwa pekee yake!

Wakati huo wewe na wenzako tena nyie wote wenye upeo mdogo sana mlijiona Miungu watu kwa kuwa mlikuwa mnakula makombo!

Leo umepigwa nje unajifanya una maarifa wakati watu wenye maarifa waliwaambia mapema mkajifanya wajuaji wakati nyie ni washamba tu!

Ebu angali leo pamoja na maendeleo makubwa tuliyopiga lakini watu hawana furaha kabisa mitaani!

Tunaelekea Christmas ,ebu pita mitaani uone watu walivyochoka mbaya!

Tumejua sasa ni kwa nini Waethiopia,Wasomali wanakimbia Nchi zao kila kukicha pamoja na maendeleo ya vitu walivyonavyo.

Mlijitahidi sana kusifia kwa nyimbo na mapambio lakini watu wenye maarifa tulijua mapema kabisa kuwa nyie ndo mtaongoza kwa kukashifu huko tuendako kwani nyie ni wanafiki mnaongalia kila jambo kwa jicho la UGALI!
 
Mkuu, si tu hisia peke yake, bali pia ikaambatana na mihemuko na kuchagizwa na nasaha kutoka milingotini kwa akina kalimanzira.

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Huna lolote wewe! Baada ya kutolewa kwenye system ya kula basi akili kidogo ulizokuwa umeshikiwa zimeanza kurudi!

Kumbuka ulivyokuwa unamtisha Ben Saanane kwamba ataliwa na Chatu akiwa pekee yake!

Wakati huo wewe na wenzako tena nyie wote wenye upeo mdogo sana mlijiona Miungu watu kwa kuwa mlikuwa mnakula makombo!

Leo umepigwa nje unajifanya una maarifa wakati watu wenye maarifa waliwaambia mapema mkajifanya wajuaji wakati nyie ni washamba tu!

Ebu angali leo pamoja na maendeleo makubwa tuliyopiga lakini watu hawana furaha kabisa mitaani!

Tunaelekea Christmas ,ebu pita mitaani uone watu walivyochoka mbaya!

Tumejua sasa ni kwa nini Waethiopia,Wasomali wanakimbia Nchi zao kila kukicha pamoja na maendeleo ya vitu walivyonavyo.

Mlijitahidi sana kusifia kwa nyimbo na mapambio lakini watu wenye maarifa tulijua mapema kabisa kuwa nyie ndo mtaongoza kwa kukashifu huko tuendako kwani nyie ni wanafiki mnaongalia kila jambo kwa jicho la UGALI!
Waliokuwa wakisifu nakuabudu now ndio wanaongoza kwa maneno makali yakuikataa hiyo Ibada ya jiwe

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom