Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,405
HAUWEZI KUMUABUD Mungu WA KWELI ALAFU UKAOGOPA JAMBO DOGO NA RAHISI LA KUTETEA HAKI AU KUPINGA WAOVU. UTAKUWA HAUMJUI MUNGU WEWE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Mungu haabudiwi na watu waoga. Mtu mwoga atakuwa na sifa nyingine mbaya ya unafiki.
2. Ni rahisi Muuaji na mtekaji au muuza madawa ya kulevya kuonana na Mungu kuliko mtu anayeshinda kanisani na misikitini kinafiki wakati ni mwoga.
3. Mtu mwoga hawezi kuwa mkweli. Mtu mwoga hawezi kutenda haki.
Mtu asiyetenda haki hawezi kumwamini Mungu.
4. Yesu alisema, wauaji, makahaba ndio watawatangulia mbinguni kuonana na Mungu mwenyewe. Kwani wao watakuwa wamefanya kazi kubwa hapa duniani.
Wakati wewe unayeshindwa kusema tuu hutaki uuaji, utekaji, dhulma, ufisadi ukibaki umekosa bara na pwani.
5. Huwezi juwa mtakatifu na mcha Mungu kama jambo dogo tuu la kupinga uonevu na dhulma linakushinda.
6. Kama jambo linakushinda, ukishikiwa panga au ukitaka kuchinjwa na mtu akakuambia umkufuru Mungu hautamkufuru wewe?
7. Watu kama Daniel, Ibrahim, Shadrack, meshaki, Abednego, Mtume Muhammad unafikiri walikuwa waoga?
8. Huyo Yesu mwenyewe mpaka anasulubishwa unafikiri angekuwa muoga angefikia hatua hiyo. Si angemkana tuu Mungu na kuendelea na mambo mengine.
9. Unashika Sabato kila siku lakini unashindwa kutetea haki, kuwapinga waovu waziwazi na msimamo wako ujulikane. Alafu unajidanganya unamuabudu Mungu. Hivi uko serious kweli?
10. Unaswali swala tano, unafunga ramadhani, unamuamia Mungu wako, Allah. Lakini unaogopa kutetea haki na kupinga uhalifu na uovu kwenye jamii yako. Hivi unauhakika kweli unamuabudu Allah?
11. Muuaji kaamua kuwa muuaji na anajua hilo ni kosa. Sio ajabu akimuomba Mungu atamsamehe haraka sana.
Lakini Mungu hawezi kumsamehe mtu mwoga, mnafiki na ambaye anashindwa mambo madogo tuu.
12. Hivi ikitokea mtu kwenye hii duniani au nchini kwetu akasema yeye ni Mungu mumuabudu. Na asiye muabudu atakula chuma hamtamuabudu nyie.
Kama mnashindwa jambo dogo tuu. Dogo sana yaani kusema tuu na kupinga uovu utaweza kusimama mbele ya Muuaji .
13. Unajua waovu, hasa wauaji hujisikia raha kubwa kuua watu wanafiki, waoga na wasiomcha Mungu. Unajua hilo?
14. Unajua mzinzi na uzinzi wake wote hujisikia hatia kubwa na huona vibaya kumuumiza mwenza wake aliyemuaminifu? Unajua hilo?
Lakini mzinzi huyo huyo husika raha na starehe kumsaliti mwenza wake mwenye vitabia vya ajabu ajabu.
15. Hivi unajua mashetani wanaumia sana kufanyia watu wema ubaya?
16. Muuaji akimuua mtu asiye na hatia huteseka sana. Wengi hujikuta wakitumia madawa ili kujiweka sawa.
Lakini muuaji huyohuyo akimuua mtu muovu huona raha na ameona ameifanya kazi ya Mungu vyema? Unazijua hiyo.
17. Hivi unajua, muuaji akifika kanisani au msikitini anawaona wote waliopale ni wanafiki hawamuabudu Mungu wa kweli. Na hata akiambiwa wapigwe risasi wote anajisikia afadhali.
18. Ni kweli mimi ni muuaji. Kweli kabisa. Na wewe? Wakati naua wewe ulifanya nini kuhakikisha kwamba unapinga mauaji? Ulifanya nini?
Wauaji hufikiri kwa namna hiyo.
19. Ni sawasawa na upo na mtoto. Anafanya vitu vya ajabuajabu mtaani huko unashindwa kumkanya, kumkemea, kumpinga. Mtoto yule anakuona wewe mzazi ni mbaya kuliko yeye anayefanya.
20. Wauaji pia hulaumu jamii kwa kushindwa kuzuia wao wasifanye mauaji.
21. Kwa sisi watibeli tunawaamini na kuwa huru na Wauaji au waovu kuliko kuwaamini watu wanafiki na waoga.
22. Watibeli ni rahisi kuwapa nafasi na kuwasamehe waovu na wauaji walioamua kuwa hivyo. Kuliko kumsamehe mtu anayenyamazia maovu na wauaji.
23. Mungu mwenye nguvu ni rahisi kuongea na kumsikiliza shetani na muuaji na kumfanikisha na kumlinda kuliko kuongea na watu wanafiki, waoga, wanaonyamazia mabaya.
Ndio maana wauaji na waovu kufanikiwa na kustawi, na wakitubu lazima wamwone Mungu.
24. Unadai unamuabudu Mungu wakati huohuo unaogopa kumpinga shetani. Hivi unaakili kweli. Yule unayemuagopa ndiye unayemuabudu.
25. Mungu ni rahisi kumpa muuaji au kahaba kazi akafanye kwa sababu sio mwoga. Na ataifanya bila kusita na bila kujali.
26. Muuaji anapoenda kuomba Mungu huongea na Mungu moja kwa moja. Wao humaanisha na hawana unafiki nafiki.
Na toba yao husikilizwa kwa haraka.
Kama anavyosikilizwa mwenye haki ambaye lazima awe anafanana na muovu sema tofauti wapo pande mbili tofauti.
27. Lakini watu vuguvugu, wanafiki nafiki, wasaliti, waoga, wasioweza kusema nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe hao ndio wabaya wenyewe.
Leo yupo kwa wenye haki, kesho yupo kwa wauaji. Kijeshi watu hao huuawa.
28. Kwenye vita ni rahisi kumshika mateka adui na kumhifadhi bila kumdhuru lakini ni ngumu kumhifadhi mtu msaliti na vuguvugu.
Nafikiri somo litakuwa limeeleweka.
Usijifanye unamuabudu Mungu wakati hata kupinga uovu au kusema kweli unashindwa ambalo ni jambo dogo na rahisi kabisa. Na hapo hujashikiwa hata bunduki. Je ukishikiwa? Si ndio utaanguka na kusujudu kabisa.
Uwe na moyo wa ushujaa, uwe hodari. Kwa. Maana hutomwona Mungu hata ufanyeje bila mambo hayo.
Taikonmaster
Kwa sasa Dar es salaam