Huwa najiuliza?

Martin BM

Member
Jul 2, 2020
16
22
Vitabu vingi vya dini vinaonyesha kumponda shetani na kumtuhumu kuwa yeye ndio baba wauovu, msababisha maasi na dhambi duniani.

Vitabu hivyo vilevile vinamtukuza Mungu kama ni baba wa upendo, vinaonesha pia hata ukaribu wa Mungu kwa baadhi ya wanadamu kama Mussa, Daud n.k.

Swali langu ni kwamba hivi mbona hakuna kitabu chochote ambacho kimeandikwa na shetani angalau hata akijionesha kujitetea juu ya yale alioandikiwa kupitia vitabu vitakatifu?

Hata Mahakamani kawaida ni lazima kesi isikilizwe pande zote mbili sasa yaani mshtaki na mshtakiwa ila huku mbona hatuoni huyu mshtakiwa shetani akijionesha angalau hata kuandika kitabu kimoja akijitetea au kukubali hizo tuhuma zote kuwa yeye ndio muhusika?

Samahani wanadini hebu nisaidieni hapa.
 
Batman akimkosa joker basi atabaki kukaa nyumbani na kukanda chapati tu..Ili afanye shughuli zake anamuhitaji joker
 
Hakuna ushahidi wa kimantiki kwamba Mungu (mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote) yupo wala Shetani yupo.

Habari za kuwepo kwa Mungu na Shetani zote ni hadithi zilizotungwa na watu kama mimi na wewe katika jitihada za kukabiliana na mazingira yao.
 
Mkuu unaona hakuna vitabu ambavyo shetani anajitetea kwakua unafuatilia mambo ya Nuru. Kama ungekua unafuatilia masuala ya giza basi ungekutana na vitabu vingi vya shetani vinavyopinga uhalali wa Mungu.

Jaribu kufuatilia uone kwa wanaomfuata mr Devil watakavyokupiga hoja hadi utabaki unashangaa. Baki huko huko Nuruni ulipo...!
 
Mkuu unaona hakuna vitabu ambavyo shetani anajitetea kwakua unafuatilia mambo ya Nuru. Kama ungekua unafuatilia masuala ya giza basi ungekutana na vitabu vingi vya shetani vinavyopinga uhalali wa Mungu.
Jaribu kufuatilia uone kwa wanaomfuata mr Devil watakavyokupiga hoja hadi utabaki unashangaa. Baki huko huko Nuruni ulipo...!
Kuna course inaitwa demonology akajaribu kuisoma.
 
Huyo shetani alivyo busy kuharibu ulimwengu kwa kusambaza
maovu na kuvuna wafuasi atapata muda saa ngapi wa kutulia na kuandika kwa ajili kujitetea?
 
Hakuna kitu kinachoitwa shetani wala majini duniani.

Ni taswira ya ajabu mmeitengeneza vichwani mwenu.
 
Nani aliyekudanganya hakuna vitabu vya shetani?

Hao wanaoabudu shetani unadhani wanaongozwa na vitabu vipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom