kyanaKyoMuhaya
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 1,952
- 939
Mwezi uliopita kaka yangu alioa na tukasherehekea kwa furaha sana, jpili iliyopita wanandoa hao wakaja kanisani kushukuru Mungu pamoja na wote walioshiriki, wakapewa nafasi ya kushuhudia lolote juu ya safari yao mpaka kufikia hapo.
Mume alishukuru kwa ufupi then akamwachia mke amalizie ili awakaribishe wati home.
MKE SASA, "Mimi namshukuru sana Mungu kwani nilipata mtihani sana wakati wa uchumba wetu maana nilikuwa najiuliza sana huyu ndiye au la maana nikiangalia KIELIMU mimi nipojuu yeye form IV mi VI, na hata katika swala la kazi ni hivyo hivyo maana yeye fundi nguo mi nimeajiriwa na serikali. lakini nikasikia Roho akinishuhudia kuwa ndiye na nikafikia maamuzi ya kukubali na sasa ni mke na mume"
Kusema ukweli mimi hiyo sikuipenda kabisa, na kwawalio sikiliza ushuhuda huu waligawanyika wengine wakampongeza mke kwa hatua hiyo wengine wakasema alimdhalilisha mumewe, wewe je unasemaje? ungekuwa ni mume ungejisikiaje?
Safi sana, MY LOVE si kaka yako alitaka watu wajue kaoa msomi, ushuhuda ulikuwa wa nini?
Last edited by a moderator: