Huu ushuhuda ni upendo au kashfa?

Huu ushuhuda ni upendo au kashfa?

MY LOVE

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
161
Reaction score
68
Mwezi uliopita kaka yangu alioa na tukasherehekea kwa furaha sana, jpili iliyopita wanandoa hao wakaja kanisani kushukuru Mungu pamoja na wote walioshiriki, wakapewa nafasi ya kushuhudia lolote juu ya safari yao mpaka kufikia hapo.
Mume alishukuru kwa ufupi then akamwachia mke amalizie ili awakaribishe wati home.

MKE SASA, "Mimi namshukuru sana Mungu kwani nilipata mtihani sana wakati wa uchumba wetu maana nilikuwa najiuliza sana huyu ndiye au la maana nikiangalia KIELIMU mimi nipojuu yeye form IV mi VI, na hata katika swala la kazi ni hivyo hivyo maana yeye fundi nguo mi nimeajiriwa na serikali. lakini nikasikia Roho akinishuhudia kuwa ndiye na nikafikia maamuzi ya kukubali na sasa ni mke na mume"

Kusema ukweli mimi hiyo sikuipenda kabisa, na kwawalio sikiliza ushuhuda huu waligawanyika wengine wakampongeza mke kwa hatua hiyo wengine wakasema alimdhalilisha mumewe, wewe je unasemaje? ungekuwa ni mume ungejisikiaje?
 
Mke ni mhaya?maana kwa masifa hawajambo.huna jinsi mkuu ndoa imeshafungwa pamoja na usomi wake mme atakua juu yake kitandani
 
Ningemfata na kumkumbatia kwani si ukweli?
Hamna haja ya kujiona umeonewa wakati ni ukweli mtupu.
 
Hivi ushuhuda unaumuhimu gani huko makanisani kwa wachungaji au wanatangaza biashara? All in all hiyo ni Kashfa, lakini wa kulaumiwa ni huyo aliyetoa nafasi ya kutoa ushuhuda bila ya kuwapa muda wa kujiandaa!! Sasa hiyo ndoa ikivunjika nashauri huyo mwanaume arudi kwenye kanisa hilo hilo akatoe ushuda jinsi ushuda ulivyovunja ndoa yake!!
 
Ungemuliza huyo kaka yako yeye alijisikiaje ili sisi tutoe hoja zetu.
 
Watu wengi huwa hawapimi wanayozungumza so shemejio yawezekana alisema kwa roho safi ila haikuwa sehemu sahihi kwake na wakati sahihi. ningeweza kumshauri ningumuomba kwa usalama wake hiyo kitu ya kijilinganisha na mumewe aifute akilini mwake maana muda si mwingi itampa kiburi sana ambacho hakina maana.
 
Nafikiri huyo dada hajui kutofautisha kati ya Kushukuru na kutoa shuhuda na pengine hata maana halisi ya shuhuda alikuwa haifahamu. Ni vyema wapendwa wenzie au marafiki zake wa karibu wamfundishe maana halisi ya kutoa shuhuda na kushukuru.
 
oooooh hiyo shukrani nayo ni toleo jipya.
 
Kha, Watu wengine kwa kupenda ujiko-eti mimi ni VI na nimeajiriwa serikalini (messenger?) kwa hiyo niko juu. Ulimbukeni++
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom