Huu ujumbe usomwe na wanaume tuu

Huu ujumbe usomwe na wanaume tuu



*Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!*

*Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.*

*Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".*

*Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.*

*Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.*

*Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!*

*Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.*

*"Hii ni siri wewe ukiwa kama mwanaume .

Uko sahihi sana kwani watoto ni wa mwanaume? mbona watoto ni mali ya mwanamke; mwanamke ndo anaenda labour Anazaa yeye hakuna mwanaume anayezaa watoto labour. Mwanaume daima hupewa mtoto sana sana unaambiwa na mkeo/mpenzio kwamba huyo mtoto wako ona unavyofanana naye kucha...wewe unachekelea kumbe mtoto ni wa rafiki yako wa karibu sana. kwahiyo hoja yako ni sawa wanaume ni wakiwa hawana mke wala mtoto bali kazi yao kutumikia wanawake na watoto wasio wao.
 
Imeniingia akilini hii kitu vizuri sana,hawa watu sio wenzetu tuishi nao kwa akili..
 
Mwanaume asipokuwa na akili atazeeka kwa tabu sana, kuna wanaume hawana kipato wanawake wao ndo watafutaji ila mwanaume anatunzwa hadi uzee wake na watoto wanamuona baba ndio King.....

Akili ndio kila kitu kama hutumii akili yako vyema lazima ulizwe.
 
Kumbuka pia unaweza ukafa kwa utapiamlo wakati unamabilioni pembeni ya kitanda chako. Pesa yako haitatoka ndani kwenda kukununulia chakula wala haitakuogesha uzeeni, hivyo ni wajibu wa watoto wako kukulea endapo watakuwa wastaarabu. Wastaarabu kwa vipi! Pamoja na pesa yako kuwepo wanaweza kuitumia kwa mambo yao binafsi na wewe kukutelekeza bila chakula na usafi.
Ukiwa na pesa hauwezi tafuta wakukuhudumia watakuja wengi hadi utawarudisha warudi makwao
 
Nimesha wai kuona kwenye groups la what's up hii story
 
Nimeyaona mengi..........umenikumbusha mbali sana kwa huu uzi.............yupo mzee mmoja jirani yangu ameachwa na watoto wake, historia yake inasemekana kuwa alikuwa hawatambui watoto wake kipindi alipokuwa na kazi alikuwa anachoma nyama na kula mwenyewe baa na marafiki zake lakini nyumbani mmmmmmh.... watoto wanakesha na ugali mlenda na maharage....mungu atusaidie
hakika ukiwatunza watoto wako hata pale wanapopevuka watakutambua wakati wa uzee wako
mungu atusaidie
kumbukeni kuwa wakati tunapofunga ndoa maandiko yalituambia kuwa nanuukuu "mko tayari kupokea na kuwalea watoto mtakaojaliwa" sote tulijibu kuwa tuko tayari..................leo hii unachoma nyama na marafiki zako watoto wako wanakula mlenda na maharage................wakati ulikiri kuwa utawatunza??
kumbukeni kuwa yakitokea haya ni laana imekurudia
 
Ujumbe mzuri sana wanaume mmesikia lakini
 
Mwanaume asipokuwa na akili atazeeka kwa tabu sana, kuna wanaume hawana kipato wanawake wao ndo watafutaji ila mwanaume anatunzwa hadi uzee wake na watoto wanamuona baba ndio King.....

Akili ndio kila kitu kama hutumii akili yako vyema lazima ulizwe.
Uko sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom