Huu uchafu kwenye sanamu ya Askari, wahusika wawajibishwe!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
attachment.php
Katika gazeti la Daily News leo 25/11/2015,kuna picha ya mzee wa KAR(Kings African Rifles) akiweka shada la maua kwa ajili ya kumbukumbu ya askari waliouwawa vita kuu ya kwanza na ya pili.
Mzee huyo katoka kwao Uingereza kwa shughuli nii ambayo pia ilihudhuriwa na balozi wa Uingereza nchini.

Cha kushangaza na kusikitisha ni jinsi mnara huu maarufu ulivyo mchafu huku picha za uchaguzi ikiwa kama zimebanduliwa masaa machache kabla yatukio.

Picha hii iliyopigwa itasambazwa dunia nzima kuonyesha uchafu wa watanzania.

Wahusika wa sanamu hiyo wachukuliwe hatua kwa kuidhalilisha nchi na kuionyesha kuwa ni nchi ya wachafu.
Kwa vyovyote vile kuna mtu hafanyi kazi yake hapa huku analipwa mshahara(sijui ni Idara ya Makumbusho au Halmashauri ya Jiji)
Lakini kwa vyovyote vile Idara inayohusika na Maadhimisho inaelekea hawakukagua eneo la tukio kabla.
Msingi wake ni kwamba watu hawafanyi kazi!!!

Hapa kazi tu iwaondoe mara moja.
 

Attachments

  • askari monument.jpg
    askari monument.jpg
    851.3 KB · Views: 864
huyu kubenea badala ya kushuguhulikia usafi jimboni kwake yeye yuko busy na mambo ya hovyo, mara kumshitaki ndugai!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom