Huu si uanaume, ni aibu

Huu si uanaume, ni aibu

Mada nzuri, wachangiaji mnaleta UCHURO!
 
Mtoa mada kama sijamuelewa saaaana,Labda hapo kwenye namba 5 kidogo.
 
hasa hapo kwenye kujibu 'k' huwa wanaboa sana...... kuhusu kuomba ushauri kwa mambo ya kitoto hapo ndo huwa nawakemea sana watu humu ndani, mfano yule wa kusema mpenzi wake kaja ghafla na hakuwa na bajeti yake ya msosi na akataka ushauri jamaa aliniudhi sana yaani.
mi nishauri kuwa watu wanaowafahamu wanaume wa namna hizi pindi waonapo dalili kama hizi wawe wanawakea na kuwaelemisha sio unaona mtu anatoa maneno ya mipasho afu unamuacha tu jua unamuharibu maana atajiona yupo sahihi
 
Miaka 5 ijayo kizazi cha wanaume kitakuwa kimepotea kabisa kabisa.
Mjiandae kisaikolojia kukubali mitala na ikibidi kianzishwe chuo kikuu cha kupunguza wivu kama sio kuondoa kabisa maana tutakuwa wachache sana.
 
we kuna unao wawinda hapa ! [ sema tu tabia hizo ni za wavulana wa mkoa wa ....................]
 
Habarini wadau,

Kuna hizi tabia za kipumbavu ambazo unakuta mwanaume anazifanya halafu haipendezi aisee,tena ni tabia za kikekike na za kitoto. Wewe kama mwanaume na sio mvulana acha kufanya yafuatayo,tuwaachie warembo:-

1) Mwanaume kulalamika hovyo na kuzira wewe unalalamika halafu wa kike afanyaje? Ukipatwa na jambo si unagangamala mazee na sio kulialia? Mtoto mdg afanyaje? Acha hizo mambo.

2) Mwanaume kuhonga kisha kujutia/kulalamika. Sasa kama umeshamuhonga mwanamke kwa kuamua mwenyewe na aidha kakupa mzigo au hajakupa ukilalamika au kuhadithia masela inasaidia nini? Kuhonga ni kawaida na unapohonga basi fanyeni yenu na msichana wako kulalamika inasaidia nini mkuu?

3) Kutumia vijimaneno vya kike mfano:
-Haloo
-Mie
-Fyuu
-lol
-Badala ya "S" mwanaume anatumia "X"
-mara "Utantaka"
-Au kwenye Okay eti "K"

Msichana mwenzio anakutumia message mpaka unajiuliza aliyeandika ni yeye au mtoto wake au karibia anakuwa shosti?

Hapo hata ukitongoza mwanamke akakukataa ni haki kwasababu anakuona ni kavulana au wakike mwenzie.

4) Kuomba ushauri kwenye vitu vidogo na visivyo na umuhimu. Hii ni hapahapa jamvini kuna wanaume wanaomba ushauri kwenye mambo ambayo hata mtoto wa form two anaweza kutatua jambo hilo.

5) Kujisifia sanaa kwenye issue ambazo sio za msingi sana,mfano
-sura, umbo, kupendwa na mabinti, kugegeda n.k
Mimi nafikiri sifa tukufu kwa mwanaume ni kutafuta pesa na kumanage majukumu ya nyumbani.

Jistukie bana mkuu.

NAWASILISHA.
Ni hatari sana
 
Hapo kwenye red hapo, je kuandika bana badara ya bwana nao ni uanaume or uanamke?!😱
 
Mkuu tatizo la watu siku hizi akiona kitu yeye hakipendi basi atataka kukifanya kuwa ni kitu kibaya kwa watu wote.
 
Back
Top Bottom