Huu sasa umekuwa wimbo wa Taifa

Huu sasa umekuwa wimbo wa Taifa

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,322
Sina maneno ya kusema zaidi ya kusema huu ni "ugonjwa hatari" kama sio "janga" la taifa. Sio Pwani wala bara, sio uswahilini wala "ushuani", sio kwa walala hoi wala walala hai, si kwa watumishi wa Mungu wala wasio watumishi. Wote tumezama kwenye tope hili. Ni aibu watu wakitambua kuwa umefanya lakini ni haya na fedheha hata kufikiri kulifanya.

Kina dada wengi wa kazi maarufu kama "house girl" wamejikuta wakifanya mapenzi na "kina baba wenye nyumba". Mapenzi haya yamekuwa yakisababisha "mimba zisizotarajiwa" ambazo zimesababisha migogoro na kusuasua kwa ndoa nyingi. Kila uchwao habari ni "nimempa mimba msichana wa kazi naombeni ushauri".

Haya yanatokea huku tukiambiwa kuna kondomu ambazo pamoja na magonjwa ya zinaa husaidia kuzuia mimba. Je, mipira hii ni haramu kwa wanandoa? Au pengine imepuuzwa? Hebu leo tulijadili hili kwa kina. Haina maana kujifanya kusaidia vituo vya watoto wenye kuishi katika mazingira magumu huku sisi tukiwa ndio chanzo. Ma-house girl wengi wamekatishwa ndoto zao nyingi na za familia zao kwa sbb ya hili nililolisema.

Jamii ni mimi na wewe, tuna lipi la kusema
 
Ndio wanazidisha shida hao katika jamii....
 
sumtymz mama wa nyumbani ndo wanachangia...utakuta maza house anambana house girl balaaa..yani anasahau kabisa kama house girl ni binadamu pia ana hisia zake...hutaki atoke nje wala awe na mpnz..mtt wa watu anashinda ndani tu kama utumbo..

akitoka kaenda gengeni tena na muda anaesabiwa...mtt wa watu unamkuta genye zimemjaa hadi akitembea anatetemeka...sasa akichoka anaamua atumie plan B...hapo ndo faza house anapoanza kuchezewa masinema...maza house unakuja kushangaa tu miezi inakatika housegirl wala akuombi hela ya pedi...ukija kushtuka too late
 
Back
Top Bottom