Huu ni wakati wa wanaume kujiangalia upya

miamiatz

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
505
Reaction score
941
Hebu tafakari matumizi yako yanakuletea baraka ama yanakuongezea mikosi? Hebu fanya hesabu ya pesa umewahi kuhonga afu ukaishia kuumizwa je kama kwamfano ungeenda zile shule za mission ukachukua mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ukamsomesha hadi kidato cha nne. Unadhani Mungu
angekulipa nini? Unadhani huyo mwanafunzi angekuombea yepi?

Ushawahi sikia jamaa amegombana na mwanamke wake mpaka mwanamke anamwambia jamaa 'ulaaniwe we'. Je unadhani kama ni mwanafunzi uliemsomesha kidato cha kwanza hadi cha nne baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada ukamkuta analia mtaani na
ukaamua kumsomesha angeweza kudiriki kusema 'ulaaniwe we'?

Nadhani kwa wenye kutafakari mmenielewa. Hata hela ya saluni tu unayohonga inaweza lipia ada shule ya mission kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka mmoja.

Ukimpa mwanamke 30,000 ya saluni kila baada ya wiki mbili ina maana kwa mwaka unampa 720,000/=. Je unajua kuwa shule nyingi za mission ada zao ni za kiwango hicho? Kama hujui basi ni wakati wa kufanya jitihada kuulizia. Ukiuliza mijini ukaona ada ni kubwa hebu nenda shule za mission za vijijini.

Hebu sasa twende kwenye uhalisia. Uwe na mwanamke unampa hela ya saluni tu bila matumizi mengine. Kwa mwaka unatumia takriban 720,000/=.

Ukisema ujiongeze kwenye vocha/bundle, simu, nguo, pesa za matumizi, michango ya vichen parties, etc etc etc utajikuta hiyo 720,000/= inakuwa kama robo ya matumizi yote. Kwaiyo
unakuta unatumia 720,000x4. Hii ni sawa na 2,880,000/= kwa mwaka. Mmmhhh inatosha hata Kulipia ada wanafunzi wanne kwa mwaka.

Mbaya zaidi unakutana na huyo mwanamke kwenye hoteli/lodge ndogondogo za 20,000 ama 30,000 afu mnakutana mara tatu kwa mwezi. Hii ni sawa na 90,000 kwa mwezi. Kwa mwaka sawa na 1,080,000/=. Hii ungetunza mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT

Ingekuwa ni akiba ambayo ingesaidia kama unapoteza kazi gafla utaishi bila mateso wakati unatafuta kazi nyingine. Hebu tafakari leo hii ukipoteza kazi utaweza ishi miezi mingapi kabla hujaishiwa kabisa? Pengine kamwe hata akiba ya mwezi mmoja huna.

TUBADILIKE, HAKO KAMKIA HAKATOSHEKI HATA KAPEWE
WANAWAKE ELFU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hesabu za kibwegebwege hizi, mleta uzi lazima utakua mwanaume wa Dar aliechunwa mpaka umekoma. Kuhonga ni sunah sheikh wangu. Achana na sisi wanaume wee tuache maana tunajijua wenyewe.
Hebu tafakari matumizi yako yanakuletea baraka ama yanakuongezea mikosi? Hebu fanya hesabu ya pesa umewahi kuhonga afu ukaishia kuumizwa je kama kwamfano ungeenda zile shule za mission ukachukua mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ukamsomesha hadi kidato cha nne. Unadhani Mungu
angekulipa nini? Unadhani huyo mwanafunzi angekuombea yepi?

Ushawahi sikia jamaa amegombana na mwanamke wake mpaka mwanamke anamwambia jamaa 'ulaaniwe we'. Je unadhani kama ni mwanafunzi uliemsomesha kidato cha kwanza hadi cha nne baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada ukamkuta analia mtaani na
ukaamua kumsomesha angeweza kudiriki kusema 'ulaaniwe we'?

Nadhani kwa wenye kutafakari mmenielewa. Hata hela ya saluni tu unayohonga inaweza lipia ada shule ya mission kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka mmoja.

Ukimpa mwanamke 30,000 ya saluni kila baada ya wiki mbili ina maana kwa mwaka unampa 720,000/=. Je unajua kuwa shule nyingi za mission ada zao ni za kiwango hicho? Kama hujui basi ni wakati wa kufanya jitihada kuulizia. Ukiuliza mijini ukaona ada ni kubwa hebu nenda shule za mission za vijijini.

Hebu sasa twende kwenye uhalisia. Uwe na mwanamke unampa hela ya saluni tu bila matumizi mengine. Kwa mwaka unatumia takriban 720,000/=.

Ukisema ujiongeze kwenye vocha/bundle, simu, nguo, pesa za matumizi, michango ya vichen parties, etc etc etc utajikuta hiyo 720,000/= inakuwa kama robo ya matumizi yote. Kwaiyo
unakuta unatumia 720,000x4. Hii ni sawa na 2,880,000/= kwa mwaka. Mmmhhh inatosha hata Kulipia ada wanafunzi wanne kwa mwaka.

Mbaya zaidi unakutana na huyo mwanamke kwenye hoteli/lodge ndogondogo za 20,000 ama 30,000 afu mnakutana mara tatu kwa mwezi. Hii ni sawa na 90,000 kwa mwezi. Kwa mwaka sawa na 1,080,000/=. Hii ungetunza mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT

Ingekuwa ni akiba ambayo ingesaidia kama unapoteza kazi gafla utaishi bila mateso wakati unatafuta kazi nyingine. Hebu tafakari leo hii ukipoteza kazi utaweza ishi miezi mingapi kabla hujaishiwa kabisa? Pengine kamwe hata akiba ya mwezi mmoja huna.

TUBADILIKE, HAKO KAMKIA HAKATOSHEKI HATA KAPEWE
WANAWAKE ELFU.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matter of priority..hii in life style yangu nashkuru sjafirisika na ntaendelea na utaratibu wangu binafsi huu ushauri wapewe vijana wadogo wanaoanza kutafuta maisha
 
Back
Top Bottom