Betterhalf
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 2,879
- 2,554
Habari za leo wadau,
Timu yetu ya Taifa yaani Taifa Stars imeanza harakati zake kwenye mashindano ya AFCON 2024 nchini Ivory Coast.
Tumeanza kwa kupoteza mbele ya timu bora Afrika na Wana Nusu Fainali wa Kombe la Dunia mwaka jana.
Pamoja na mambo mengine, lakini sehemu ambayo kama taifa, tumeshindwa kuwa na chaguo sahihi la makocha wetu.
Sitaki nimzungumzie Kocha wa sasa, bali ninatamani tusonge mbele kwa kuwa na Kocha sahihi kwa mtazamo wangu.
Kocha HERVE RENARD amekuwa nguli kwenye soka la Afrika kwa sasa. Akiwa Ivory Coast na Zambia kwa nyakati tofauti, ametwaa Kombe la AFCON na kuonesha uwezo mkubwa kwenye kuujua utamaduni wa waafrika na namna ya kuwatumia wachezaji.
Huyu ni Kocha sahihi ingawa sijajua kwa sasa yupo wapi.
Natamani nimuone akija Tanzania kuanzisha project mpya ya uundaji wa kikosi cha timu ya taifa.
Hapa simaanishi kama aipangeje timu, bali tuone mabadiliko ya kimfumo ambayo yatamsaidia kujua awatumie akina nani na awaage akina nani.
Naomba kutoa hoja.
Ahsante sana.