Huu ni utoto au utaahira?

Ni hivi yalimtokea shost, boyfriend anakwenda kwake, lakini hamfahamishi nyumbani. Mpaka wamepata mtoto, mama mkwe amekuja kumwona mtoto, ubatizo wa mtoto umefanyika kwa shost mama amekuja kama mgeni. Sasa siku moja shost anakwenda Kariakoo shopping, anakutana na jamaa yuko na mother, khe, baada ya salamu aliuliza mnakwenda wapi, mama alijibu kupanda basi twende nyumbani, mama alikuwa na mzigo, shost aliofer lift, jamaa alitaka kutoa nje, mama aliona unafuu ule alikubali.

Wamefika home, masikini mama anaishi kwenye nyumba ya nyuma mbele ameweka msingi tu na ni wa muda mrefu. shost aligundua kwanini jamaa alikuwa hataki afike home. Sasa kama mtu umesha zaa nae, haya si ni mambo ya kawaida tu. Hakuna aliyeumbiwa umasikini.
Sijawahi ona umepost mambo yako. Kila siku ni mashost zako ndo wana matatizo au wanaomba ushauri. Fake ID bado unaona aibu? Sema ni wewe.

Kama nadanganya pitia nyuzi zako zote uone
 
Ukiona mwanaume hataki kukupeleka home/ghetto au hataki kukutambulisha kwa close friends and relatives, ujuwe kuwa he's using you (most of the time).

Mtu akiwa serious na wewe lazima atatamani ujuwe anapoishi, ndugu zake walau uwaone au apige simu uwasalimie, otherwise jiulize.
Hii ni red flag pia, right?
 
Sijakuelewa ila acha nicomment kwa nilichoambulia,sio kila msichana ni wakupeleka home wengine tunapiga tu,na nikumegee siri kuna wasichana wengine ni wakukutana nao usiku au gest hata barabarani hatuongozani nao kwa sababu hawana mvuto,tunaondolea hamu tu.
Duuuuh heshima zenu wanaume
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Ni kweli kabisa kama shost alipoona ile hali alimpa jamaa support ya kumaliza nyumba ya mama. Mwanzo alifikiri jamaa atakuwa na mke nyumbani kumbe masikini haikuwa hivyo
Shosti muelewa.
Watu wengine ni bora uwaibie kuliko kuwadanganya wengine wangemwacha siku hiyo hiyo. Au alilinda mtoto?
 
Ni kutokujiamini tuu, kama mtu una Malengo naye kwa nini asipajue kwenu sasa..

Hii huwapata wale wanaoigiza maisha kumbe ni kina sie humu, we kwenu hutaki pajulikane kwa nini??
 
Shosti muelewa.
Watu wengine ni bora uwaibie kuliko kuwadanganya wengine wangemwacha siku hiyo hiyo. Au alilinda mtoto?
Yah alifanya vile basically kuwa ni kwa bibi wa mtoto wake.
 
Ni hivi yalimtokea shost, boyfriend anakwenda kwake, lakini hamfahamishi nyumbani. Mpaka wamepata mtoto, mama mkwe amekuja kumwona mtoto, ubatizo wa mtoto umefanyika kwa shost mama amekuja kama mgeni. Sasa siku moja shost anakwenda Kariakoo shopping, anakutana na jamaa yuko na mother, khe, baada ya salamu aliuliza mnakwenda wapi, mama alijibu kupanda basi twende nyumbani, mama alikuwa na mzigo, shost aliofer lift, jamaa alitaka kutoa nje, mama aliona unafuu ule alikubali.

Wamefika home, masikini mama anaishi kwenye nyumba ya nyuma mbele ameweka msingi tu na ni wa muda mrefu. shost aligundua kwanini jamaa alikuwa hataki afike home. Sasa kama mtu umesha zaa nae, haya si ni mambo ya kawaida tu. Hakuna aliyeumbiwa umasikini.
Acha umbea
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Sijawahi ona umepost mambo yako. Kila siku ni mashost zako ndo wana matatizo au wanaomba ushauri. Fake ID bado unaona aibu? Sema ni wewe.

Kama nadanganya pitia nyuzi zako zote uone

Asante ulikuwa kichwani mwangu.. Naumia mtu kujivikia kiremba cha kuwasemea wengine ilahali story inamhusu yeye kwa nini???? Huu ndio Utahira na Utoto plus Ulimbukeni wakujiona kuwa yeye hawezi kuwa na mapungufu au matatizo yakusaidiwa ila kuwatolea mfano wenzie..JF Bwana
 
Kutokujikubali ni kubaya sana! Wengi wana tabia ya kujiona much know mjini..ila usiombwe apate majanga kama kufa au kufiwa ni aibu au fedheha ukikuta maisha ya majumbani kwako lol..penden makwenu mtakuja kuaibikaaa
 
Wanawake wengine hawaelewi wanataka nn ukimuita kwako anaogopa anataka kwrnda guest sasa unadhani mtu kama huyo utampeleka kwa wazazi kweli?!
 
Umepata mapenzi kwa kuwa umejiwekea ka status mjini unaona aibu kumpeleka kwenu kutokana na hali halisi . Hii ni kukosa confidence ya maisha, utoto au ni utaahira?

Usiombe kuolewa na mwanaume mwenye roho ya ki-maskini

Kuna Nyingine Uliaga na kusema upo busy na hutaweza kuhudumia vyote kwa wakati mmoja sasa Yamekuwaje... Pole Huyo Mwanaume kwa unavyomsimanga Humu Ndani Laiti kama angekuwa Member basi Sijui..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom