Huu ni unafiki: Mnyonge mnyongeni...

Huu ni unafiki: Mnyonge mnyongeni...

Lawama kwa Nyerere si kwa tatizo hilo tu, bali matatizo yote yanayoikumba Tanzania ya leo.

Matatizo ya Tanzania ni uongozi mbovu na misingi mibovu aliyoiacha Tanzania.
Hakuna alichokifanya Nyerere hata kimoja kilichofanikiwa, kama kipo mimi sijakiona na sitegemei kukiona.
Utakionaje wakati roho yako na akili yako umevingandisha kwenye sehemu ya dharau na kukosa hekima,kwa jinsi ulivyo hatujali hata hutakuja kuona mafanikio ya mwalimu Nyerere mpaka ufe mupo watu wa aina hiyo ambao hatuwahesabii kwenye jamii
 
Nimesoma post moja yenye heading KIKWETE ALIVYOONDOKA MONDULI CHUO CHA JESHI KWA MSUKOSUKO. Kama yaliyoandikwa ni kweli, basi post hiyo nimeipenda sana na ninashauri kila mtu aisome.
Mara kwa mara nimekuwa nikisema members wengi wa JF ni wanafiki na wanaushabiki wa kitoto kabisa. Ni ajabu. Assume, kweli JK alitoa siri kuwa Mzee Sayore anafanya aliyokuwa akiyafanya, Huo ni uzalendo wa hali ya juu lakini unakuta mwana JF anaamua kumkanyaga JK kwa uamuzi wake wa kutoa siri kwa yale yaliyokuwa yakimkera. Je, mngependa JK afumbie macho uovu?

Mi nilitegemea tuseme Nyerere na Msuguri hawakufanya vema kwa kutom-protect informer. Kama kweli JK alifanya vile alikuwa na machungu na siasa ya ujamaa ambayo ilikuwa haitaki ubepari. Nadhani tunaweza kumpigia makofi.
Inawezekana mnamuona JK kuwa labda ni mnafiki kwa kuwa sasa rafiki zake ni matajiri wakubwa, hili ni jambo la kawaida kabisa kwani Sheikh, Mchungaji au Padri anaweza kugeuka na kuwa bedui mkubwa na bedui anaweza kuwa Sheikh au hata mchungaji.

Kilichofanyika hapa"kama ni kweli" ni kosa kwa Msuguri ambapo alitaka kumchonganisha JK kwa bosi wake. Ni sawa na kumwambia mtu bona fide kuwa spouse wake anamahusiano na mtu mwingine halafu badala ya kufanya uchunguzi anaenda kumwambia huyo mwenza wake kuwa habari hii nimepewa na fulani. Acheni siasa, Leo mnamsakama JK, kesho mtaandika jinsi Dr Slaa alivyopora mke wa mtu na jinsi Mbowe alivyoifisidi NSSF au pia hata jinsi Chacha Wangwe alivyouawa. Ni unafiki tuuu.

Tumekusikia lakini kwa taarifa yako kikwete wako hakusema vile kwa sababu ya uzalendo ni wivu tu ulikuwa unamsumbua kama wivu wako wewe wa kuona Slaa kapata mke bomba na mbowe kukopeshwa NSSF, mbona wengi wamekopa acha wivu kama wa kilaza mwenzio Kikwete.
 
wagonjwa wa akili jf wapo kibao.........hii habari ni ya kweli maana hata mzee wangu alinambia juu ya hii kitu

alikuwepo huko miaka hiyo.......

jk ni mpuuzi sana, mnafiki, mfitini, mchonganishi nk
 
Umeisoma vizuri hiyo habari weye?
Yule Sayore alikuwa anafuga hao wanyama na akawa anawauzia Jeshi..je kulikuwa na tatizo gani??
Mali yako mwenyewe unataka kuuza, jamani hapo kuna kosa gani?? hata Nyerere aliona kuwa huo ulikuwa ni upuuzi na wivu tu ndio maana aliamua tu kukaa kimya.
Hapo inaonekana wazi kabisa JK kilikuwa kinamuuma sana kwa Sayore kulipwa pesa na Jeshi, sasa alitaka awe anatoa maziwa bure??
na hao ng'ombe wangeendeleaje kuhudumiwa??
use ur common sense

Kumbuka hapo anaongelea kipindi cha siasa za ujamaa na kujitegemea. Pia kama alikuwa anaalisha jeshi kuna ama taasisi yoyote ya umma kuna taratibu za tenda. Usidhani kama una mali yako na wewe ni mkuu wa taasisi fulani ya umma basi unaweza ukaamua tu kuwasambazia vitu then ukachukua fedha. is a kind of UFISADI. Msitetee maovu na ndio maana tunasema HATA MBAYA WAKO, ANA MAZURI YAKE
 
Back
Top Bottom