HUU NI UNABII WA MUNGU AU NINI???

HUU NI UNABII WA MUNGU AU NINI???

comesucces

Senior Member
Joined
Feb 21, 2017
Posts
160
Reaction score
105
Habari za mchana ndugu zanguni!

Kuna mambo mengine hata upinge kiasi gani yatabaki palepale hii ni kutokana Na uthibitisho nilioweza kuushuhudia kwa macho yangu mwenyewe jinsi mambo yanavoenda !
KUNA WATU FULANI HIVI WALIKUJA MITAA YETU NA KUTOA MATANGAZO KWA NJIA YA REDIO WAKIDAI KUWATABIRIA WATU NA KUWAPONYA MAGONJWA MBALIMBALI SUGU KWA KUTUMIA JINA LA YESU KRISTO NA MKUTANO WAO ULIPANGWA KUWA WA WIKI NZIMA kwa upande wangu sikuamini kama kweli hicho kitu kinawezekana kwa namna rahisi ile lakini Siku ya tatu nikaenda mchana Na kumkuta nabii huyo cha kushangaza ni kweli kaeleza vitu ambavyo nimekutana navyo Na mambo mengi ambayo hata Mimi nilishangaa ameyajuaje?? [emoji134] nahapa naomba msaada kwa wajuvi unapataje / unawezaje kumtambua MTU jinsi alivyopitia maisha yake bila hata ya yeye kujieleza???

kizaa zaa kikaendelea ndani ya ukumbi hapa napo nikapata maswali mengi sana pindi hawa manabii wanavolazimisha WATU kutoa sadaka tena wakidai lazima utoe Pesa kubwa kuliko zote ulizonazo, Na kingine ni mchungaji gani au nabii gani hatumii biblia mwanzo mwisho Wa mafundisho yake, hatujakaa sawa anatoa maji Na kuyaita haya ni maji ya baraka Na kuwanawisha watu mikono akiaminisha kuwa anakomboa mikono yao kutoka kwa wachawi, katoa tena kitu inaitwa mafuta hapo ndipo angusha wengi kwa mapepo Na kusababisha ukumbi mzima kujaa makelele ila ilikuwa ngumu sana kuanguka baada ya kumaliza shughuli hizo ndipo kadai kuwa anaanza kumtabiria MTU mmojammoja mzee mzima nikaenda kufika pale hakuna cha kutabiri Bali ni maagizo tu ati lete noti ya elfu kumi Na mishumaa mitatu hapo nilipoondoka ikawa jumla SWALI LANGU JE HII NI INJIRI NA MBINU GANI WANAITUMIA KUMTABIRIA MTU?????
 
Maigizo na wizi mtupu..kimbiaaa...Baki na imani yako tu
 
Heeeeh unabii mkuu uwoni ata aibu kwa karne hii kuna nabii kweli

Ngoja tumsikilize yesu atatimba siku sio nyingi wee vunga vunga kwanza
 
Njia panda lakini imeandikwa ktk vitabu vya dini manabii wa uwongo watakuwa wengi cku za mwisho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom