Huu ni ulemavu au makusudi

Huu ni ulemavu au makusudi

ESPIRIT

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2014
Posts
665
Reaction score
524
Watanzania wengi sasa wameamua kuharibu kiswahili Lugha yetu ya taifa. SEHEMU ya 'L' wanaweka 'r na kinyume chake. Mimi hukasirishwa sana kuona lugha inakosewa na watu wazima. Mfano
1. Naomba ladhi
2. Naomba nikurishe chakula
3. Raini yako ya simu iko wapi.
4. Weka porepole jaman n.k. HUKU NI KUKOSA ADABU./ NAOMBA NAWE UONGEZE MANENO ULIOWAH KUSIKIA YANAKOSEWA ILI WAJIREKEBISHE/
 
Wengine hata uwachape bakora hawawezi kuacha kwa sababu ni lafudhi ya kikwao, eg wakurya hawana L wana R
 
"Uhongo" badala ya "uongo", Hacha badala ya Acha, Uraaniwe balada ya Ulaaniwe,
 
Watanzania wengi sasa wameamua kuharibu kiswahili Lugha yetu ya taifa. SEHEMU ya 'L' wanaweka 'r na kinyume chake. Mimi hukasirishwa sana kuona lugha inakosewa na watu wazima. Mfano
1. Naomba ladhi
2. Naomba nikurishe chakula
3. Raini yako ya simu iko wapi.
4. Weka porepole jaman n.k. HUKU NI KUKOSA ADABU./ NAOMBA NAWE UONGEZE MANENO ULIOWAH KUSIKIA YANAKOSEWA ILI WAJIREKEBISHE/

Hilo ni tatizo kubwa sana na linatokana na sababu kuu tatu.

1. Ni athari ya lugha mama (lugha ya kwanza) ambayo mtu hujifunza pale tu anapoanza kujifunza lugha kwa mara ya kwanza, lugha hii ndio huujaza ubongo wake sauti mbalimbali (Language acquisition) na kama lugha ya kwanza ya mtu huyo haina sauti fulani basi mtu huyo hataweza kuitamka sauti hiyo kwa sababu alasauti za mtu huyo hazitaweza kupokea taarifa sahihi juu ya sauti husika. Kwa mfano sauti /r/ ni kimadende cha ulimi ambacho ili kuitamka lazima ulimi uchongoke (tongue rolling) na kutengeneza ncha itakayogusa vituta juu baada ya ufizi kurudi ndani na kuleta mrindimo wa hewa. Kwa mtu ambaye lugha yake ya kwanza haina sauti /r/ basi kamwe hataweza kuitamka sauti hiyo kwa usahihi.

2. Sababu ya pili ni athari za kibayolojia ambazo huathiri baadhi ya alasauti za mzungumzaji,hii huweza kusababishwa na maradhi au matatizo mengine kama ajali ambayo huathiri sehemu zinazohusika na utamkaji wa sauti. Mathalan mtu akipata ajali na sehemu ya taya ikapata matatizo au meno yakapotea basi mtu huyu anaweza kushindwa kutamka baadhi ya sauti.

3. Wapo pia ambao huathiriwa na mazingira hasa maeneo ambayo yana mchanganyiko wa makabila na hivyo jamiilugha hujikuta imeibua upekee katika utamkaji wake kama ilivyo kwa watu wa maeneo kama Arusha, hawa pia huweza kuathiri utamkaji wao.

Masuala haya hujikita katika taaluma ya lugha ijulikanayo kama FONETIKI na hujipambanua katika tawi la Fonetiki Matamshi. Tawi hili huchunguza utamkaji wa sauti na usahihi wake. Iwapo mtamkaji atakuwa na tatizo basi hushughulikiwa na tawi liitwalo Fonetiki Tiba Matamshi ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye maabara ya sauti (kwa nchi zilizoendelea).
 
Na pia kuna matumizi ya herufi 'x' katika kiswahili.Kuna mtu anaweza akaandika kitu ukashindwa kuelewa kwa haraka.Na hiyo ni makusudi kabisaa.Mtu badala ya kuandika 'sasa' anaandika 'xaxa'.kuna ugumu gani wa kutumia herufi 's' hapo sasa!!sijui wana matatizo gani watu hawa!
 
Watanzania wengi sasa wameamua kuharibu kiswahili Lugha yetu ya taifa. SEHEMU ya 'L' wanaweka 'r na kinyume chake. Mimi hukasirishwa sana kuona lugha inakosewa na watu wazima. Mfano
1. Naomba ladhi
2. Naomba nikurishe chakula
3. Raini yako ya simu iko wapi.
4. Weka porepole jaman n.k. HUKU NI KUKOSA ADABU./ NAOMBA NAWE UONGEZE MANENO ULIOWAH KUSIKIA YANAKOSEWA ILI WAJIREKEBISHE/

ridhiki badala ya riziki nalo hukera sana.
 
Siku hizi hadi watangazaji wa Tv na Radio ndio balaa yaani wanavyozunguza kwa sisi wajuvi wa lugha unatamani hadi mchomoe kwenye tv umlampue makofi.
 
watanzania wengi sasa wameamua kuharibu kiswahili lugha yetu ya taifa. Sehemu ya 'l' wanaweka 'r na kinyume chake. Mimi hukasirishwa sana kuona lugha inakosewa na watu wazima. Mfano
1. Naomba ladhi
2. Naomba nikurishe chakula
3. Raini yako ya simu iko wapi.
4. Weka porepole jaman n.k. Huku ni kukosa adabu./ naomba nawe uongeze maneno uliowah kusikia yanakosewa ili wajirekebishe/

Uliowah = Uliyowahi.
 
Pia wanatamka "dha" badala ya "tha" kwa mfano thabiti wanasema dhabiti, hasa wasomaji wa matangazo
 
Hizo herufi L" na R " wahaya wanashida nazo sana sijui kwa nini alafu kuna neno Nideep badala ya Nibeep huwa silielewi kabisa
 
Watanzania wengi sasa wameamua kuharibu kiswahili Lugha yetu ya taifa. SEHEMU ya 'L' wanaweka 'r na kinyume chake. Mimi hukasirishwa sana kuona lugha inakosewa na watu wazima. Mfano
1. Naomba ladhi
2. Naomba nikurishe chakula
3. Raini yako ya simu iko wapi.
4. Weka porepole jaman n.k. HUKU NI KUKOSA ADABU./ NAOMBA NAWE UONGEZE MANENO ULIOWAH KUSIKIA YANAKOSEWA ILI WAJIREKEBISHE/
Thread hii iende jukwaa la lugha ambako maudhui ya hii thread yamejadiliwa sana, mfano kwenye thread ya Kibo10
 
Last edited by a moderator:
Yaani lugha ya siku hizi ni shida, eti nasikia wana jamii forum wote hawajui kinyume cha neno Machweo!
 
Na pia kuna matumizi ya herufi 'x' katika kiswahili.Kuna mtu anaweza akaandika kitu ukashindwa kuelewa kwa haraka.Na hiyo ni makusudi kabisaa.Mtu badala ya kuandika 'sasa' anaandika 'xaxa'.kuna ugumu gani wa kutumia herufi 's' hapo sasa!!sijui wana matatizo gani watu hawa!

hiyo xaxa hua inaboa.. na siku hizi touchscreen zina QWERTY keyboard muda wa kuandika sasa na xaxa ni uleule, wanafata fashion ujinga
 
Na pia kuna matumizi ya herufi 'x' katika kiswahili.Kuna mtu anaweza akaandika kitu ukashindwa kuelewa kwa haraka.Na hiyo ni makusudi kabisaa.Mtu badala ya kuandika 'sasa' anaandika 'xaxa'.kuna ugumu gani wa kutumia herufi 's' hapo sasa!!sijui wana matatizo gani watu hawa!

Kuiga kusikokua na faida...naonaga ni kama ujinga tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom