Kitu ambacho kimenisikitisha ni kauli zake, na vitisho. Hii inaonesha kiasi gani mfanyakazi wa nchii hii anavyodharaulika. Rais anaongea kwa uhakika namna ile wakati karibia na uchaguzi? na wale wajinga wajinga waliokwepo pale shida zimewajaa mpaka midomoni eti wanashangilia tuu, aaaagh waDanganyika lini tutazinduka jamani? Hivi kwa nini wafanyakazi wa nchi hii hatuna nguvu katika serikali yetu? tunachezewa tuu kama watoto wadogo! hivi kauli kama hizi zingetolewa kule Bondeni kwa MADIBA nadhani COSATU wange zaa na mtu. Kule wenzetu chama chao ni very very powerful, tatizo sisi tulifanya cha cha wafanyakazi ni jumuia ya CHAMA, wakajazwa ma shushushu tu huko, na hakukuwa na lolote miaka yote iliyopita. Sasa hivi ndo tunazinduka na kukuta mfumo mbaya mno. Kingine nimestajaabu ni idadi ya wafanyakazi serikalini. Miaka yote nasikia Serikali ndo mwajiri mkuu yaani serikali ndo imeajiri watu wengi kuliko sekta binafsi. Lkn idadi niliyosikia jana kumbe watu laki tatu na nusu tu ndo wapo serikalini, nchi yenye watu millioni arobaini, ukitoa watoto na wanafunzi labda wabakie millioni ishirini, waliobakia hapo labda laki moja wapo sekta binafsi, wengine wakulima na jobless. Ndo maana nchi hii ukukaa Dar utadhani imepiga hatua sana lkn nenda mrogoro tu hapo utashangaa maisha jinsi yalivyo ya kijima. Ule Umati na mshikamano na kutomwalika pale shamba la bibi (Uwanja wa Uhuru) ndiko kulikomfanya jasho limtoke, kaona mambo yanaweza kwenda mrama, ndiyo tunaweza badilisha serikali, kwa nini hatuwezi? huu mshikamano wa wafanyakazi ni muhimu sana kwa maslahi ya taifa hili. Tusikubali kuburuzwa tuuu wakati wao wanamaliza keki ya nchi hii halafu sie tunaonekana tunawabugudhi katika ulaji wao.