Huu ni mwanzo mzuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni mwanzo mzuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, May 4, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kiukweli kikwete anahitaji changamoto ili aamke alikolala. Jana aliongea sana juu ya TUCTA. Mengine ya ukweli, mengine vitisho, mengine kujitetea, na mengine ushauri, n.k. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa tunahitaji kina mgaya wengi wa kumchangamsha rais anayeona kuwa kila kitu ni shwari kumbe sio. Takwimu zake alizotoa si za kimantiki kiivyo. Kuna hela nyingi sana zinavuja nchi hii ambazo zingeweza kuboresha mambo. Rais asingoje kuwaka na kutoa vitisho yanapotokea ya tucta. Ni kweli katishika kwani hajawahi kuona hayo yakitokea. Rais wetu ni muongeaji mzuri ila si mtekelezaji. Kasema kuwa yeye ndie mwajiri mkuu. Hajajua kuwa sisi wananchi ndio tumemwajiri? Kama haamini hilo basi asitekeleze matakwa ya watanzania
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwa lipi la maana aliloongea hususani jana? sijaona maneno ya hekima hata moja,labda mipasho na taarabu.Hata kama ana point ya kuongea,presentation ni very poor nasikitika kusema hilo.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kitu ambacho kimenisikitisha ni kauli zake, na vitisho. Hii inaonesha kiasi gani mfanyakazi wa nchii hii anavyodharaulika. Rais anaongea kwa uhakika namna ile wakati karibia na uchaguzi? na wale wajinga wajinga waliokwepo pale shida zimewajaa mpaka midomoni eti wanashangilia tuu, aaaagh waDanganyika lini tutazinduka jamani? Hivi kwa nini wafanyakazi wa nchi hii hatuna nguvu katika serikali yetu? tunachezewa tuu kama watoto wadogo! hivi kauli kama hizi zingetolewa kule Bondeni kwa MADIBA nadhani COSATU wange zaa na mtu. Kule wenzetu chama chao ni very very powerful, tatizo sisi tulifanya cha cha wafanyakazi ni jumuia ya CHAMA, wakajazwa ma shushushu tu huko, na hakukuwa na lolote miaka yote iliyopita. Sasa hivi ndo tunazinduka na kukuta mfumo mbaya mno. Kingine nimestajaabu ni idadi ya wafanyakazi serikalini. Miaka yote nasikia Serikali ndo mwajiri mkuu yaani serikali ndo imeajiri watu wengi kuliko sekta binafsi. Lkn idadi niliyosikia jana kumbe watu laki tatu na nusu tu ndo wapo serikalini, nchi yenye watu millioni arobaini, ukitoa watoto na wanafunzi labda wabakie millioni ishirini, waliobakia hapo labda laki moja wapo sekta binafsi, wengine wakulima na jobless. Ndo maana nchi hii ukukaa Dar utadhani imepiga hatua sana lkn nenda mrogoro tu hapo utashangaa maisha jinsi yalivyo ya kijima. Ule Umati na mshikamano na kutomwalika pale shamba la bibi (Uwanja wa Uhuru) ndiko kulikomfanya jasho limtoke, kaona mambo yanaweza kwenda mrama, ndiyo tunaweza badilisha serikali, kwa nini hatuwezi? huu mshikamano wa wafanyakazi ni muhimu sana kwa maslahi ya taifa hili. Tusikubali kuburuzwa tuuu wakati wao wanamaliza keki ya nchi hii halafu sie tunaonekana tunawabugudhi katika ulaji wao.
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ni kweli,hasira na mipasho ya jana ni hasira ya kutoalikwa kuwa mgeni rasmi.
   
 5. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2010
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hivi wageni rasmi huwa wanalipwa posho?
   
 6. M

  MJM JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mimi simo. Jana muungwana ndiyo katoa best speach ever. Hivi ukitaka kuongea na TUCTA unaita wazee au TUCTA wenyewe? Hauwezi kuwaita watu ambao hawafanyi kazi kuwaelezea madai ya wafanyakazi. Ni kuwadhalilisha wazee hao japo wao hawajitambui. Mbona hawaiti kuwaeleza Kagoda and kinds ni nini na kwa nini kama anataka kuwashirikisha informations.
   
 7. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Hatuna rais jamani. Hv hajui kuwa anapocheza na wafanyakazi anachezea familia zaidi ya laki 3 na nusu? Hela za kununua mashangingi, posho, mishahara mikubwa ya makatibu wakuu na wanasiasa zinatoka wapi? Hv kwa hotuba kama ile kuna tofauti gani kati yake JK na sofia simba, mwatum mahiza na Hawa ghasia? October wadanganyika tuamke nchi imeliwa.
   
 8. M

  Maimbe Member

  #8
  May 4, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 5
  Kwa kweli rais wetu alichemsha, hotuba yake haikuwa na hadhi ya Urais. Isitoshe naamini madai ya TUCTA ni ya msingi na bila shaka walipopendekeza kima cha chini walitoa pia na altervative source of funds. Serikali ingepunguza matumizi makubwa yasio ya laziam kwa maofisa wake na wanasiasa pamoja na kudhibiti kodi za wafanyabiashara wakubwa, secta za madini, maliasili nk ili mfanyakazi naye aweze kujikimu. Huu ni unynyasaji maana gap kati ya mbungu na mwananchi anyewakilishwa naye ni X X X (12 mIL KWA LAKI 1) DUH!MASHAKJI HAPO HAKUNA USAWA WALA UWIANO!
   
 9. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hoja ya mapato ya serikali haina msingi sana maana alitakiwa kujibu juu ya mianya ya kuvuja mapato ya serikali ambayo wafanyakazi waliizungumza wakati wa Mei mosi. Sasa hivi wafanyakazi si mbumbumbu, wana takwimu zote sahihi.
  Kibaya zaidi, baada ya kuona ameshindwa kujibu hoja, akaanza kumsakama Mgaya kama mtu binafsi. Anapaswa kujua kuwa Mgaya anawakilisha wafanyakazi na yeye mwenyewe akiwemo kama mfanyakazi. Alipoona amekosea katika hilo akaanza kuwa 'mbogo' eti mkigoma mtakiona -hivyo ni vitisho tu; eti tutawafukuza na kuajiri wengine? Hakika huu ni upuuzi. Haiwezekani rais ukawaza kuwa unaweza leo ukafukuza wafanyakazi wote na ukaajiri wengine hapohapo - hii siyo engine kwamba unaweza ukaitoa na kufunga nyingine hapohapo na ukaaza safari! Unatakiwa uzoefu nk; eti utachukua wasioajiriwa mitaani na kuwajiri hapo hapo. Fikiria madaktari, wahasibu, makarani, makatibu wa wizara, wakurugenzi wa wizara - eti leo unaokota tu mitaani unajaza nafasi zao? (Labda ndiyo alivyozoea kufanya)
  Rais aliwahamasisha hao 'wazee' kumshangilia na kupandisha jazba na kutoka nje ya mada kabisa - hapa akaanza kuonyesha usanii wake jukwaani
  Hakika wafanyakazi mmeishika pabaya serikali, gomeni, mkiachia mwanya huu mkagawanyika mtaendelea kupondwa vichwa kama nyoka. Kumbukeni rais amewaambieni kuwa hata mkigoma kwa miaka minane, hiyo 315,000/= hamuipati n'go. Kwa maana hiyo msipogoma mgomo ambao utaitikisa serikali, mjue madai yenu yatakuwa ndoto tu.

  Juu ya sekta binafsi, serikali ilishatangaza kuwa waongeze 100%. Kwa maana hiyo serikali iliwapangia tena bila ya kuwapa muda wa kujiandaa, lakini yenyewe inaaza kusema hili haliwezekani, je haioni kuwa hata hao waajiri binafsi watatumia kigezo kama cha serikali? Rais hakuwa na haja ya kutoa mifano ya wafanyakazi wa ndani au wa grocery au madreva wa daladala, kwani hao hawawezi kugoma kwani serikali imeshaagiza sekta binafsi iongeze 100%. Kwanini hakusema madaktari gomeni halafu muone mwajiri wenu atakavyowafukuza? Nk.
  Dear workers, divided you fall united you stand. Msikubali kugawanyika.

  Kwa mujibu wa tucta, sheria imefuatwa kikamilifu ili kufikia kutangaza mgomo; kama hii ni kweli, basi hakuna atakayegoma na akafukuzwa kazi, na kama akifukuzwa, atakwenda mahakamani na kupata haki yake ikiwa ni pamoja na fidia kubwa tu

  Eti kama mnataka kuninyima kura ninyimeni tu! Maskini wafanyakazi – mmeshiriki mara nyingi kuwaweka madarakani (tena wakati mwingine kwa mbinu chafu) sasa wameshika mpini wanawaringia, mmekuwa kama "takataka', hamna thamani tena kwao na hawawahitaji! Poleni sana –sikutegemea maneno haya yatoke kinywani mwa Rais
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Wandugu mmesema ukweli. Rais anaamini kuwa watanzania laki 3 walio katika serikali hata wakimnyima kura bado atakuwa rais! Ni kweli hakupaswa kuongea na wale wazee, tena wa ccm. Angekuwa hodari angeitisha mkutano na waandishi wa habari na kucheza na hoja kama kina Blair. Wale wazee wana shida zao hivyo watacheza na mdundo wowote watakaopigiwa. Ni watu ambao hawana taarifa za kutosha kuhusu nchi hii na yale yanayoendelea. Sema tu alikuwa anatupasha kwa mlango wa nyuma akijua fika kuwa ujumbe ungetufikia huku akishangiliwa. Ili rais athibitishe kuwa yeye yuko sawa, aitishe mkutano na waandishi
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huyu alikataliwa sana hata na Nyerere kuwa asiwe Rais...Ona sasa mambo yake yalivyo ya kimabavu!...Kwa wafanyakazi mkali, lakn kwa mafisadi anafyata mkia!
   
 12. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Sasa tufanye nini na kesha shika rungu na jamaa Gen DM yuko kwa nyuma na jamaa yake mzee jamii IGP mwanangu ukikohoa tu unalo kichwani na kasema mwenyewe kila mtu atakuwa na PLASTA USONI we ngoja ushuhudie hiyo kesho,hata mimi naitafuta hiyo PLASTA.
   
 13. Lowenstern

  Lowenstern Member

  #13
  May 4, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebwana jana Mh. Kikwete ameongea sana na kuna mengine ya ukweli na mengine yanahitaji unagalizi wa karibu sana na utekelezaji. tatizo kubwa la nchi yetu ni kwamba mabossi ndio wanao jaliwa sana kuliko watendaji wengine. kwanini viongozi wetu wasifany kama kenya na uganda. kila kiongozi anunue gari mwenyewe au kama ni la serikari liwe la bei ya kawaida. serikari inasema haina hela but kila mkurugenzi wa taasisi ya serikari anatembelea VX ukiuliza bei ni million miamoja sabini na na kulihudumia sio chini ya million moja kwa mwezi, achilia mbali vikao na safari waendazo ambazo hazina umuhimu sana na gharama zitumikazo ni kubwa sana kiasi ambacho zinaweza kupunguzwa na kuboresha maslahi ya watanzania au WAFANYA KAZI WAKE. Ukiuliza eti serikari haina hela.

  Tukija kwenye kodi sio mbaya serikari ikapunguza kodi wanayo katwa watanya kazi wa serikari ni kubwa sana.
  naishauri serikari ifikirie kwanza na kufanyia kazi haya mambo sio kuanza kujibizana na TUCTA wakati hawana (serikari) evidence za kutosha.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Well said mfalme: hao wazee ni kaput. miaka ya nyuma wakati wa Ruksa walimpigia makofi pale rais alipowaita na kuwatangazia uchangiaji wa ada vyuo vikuu. Baadaye wazee hao waliuma meno pale vijana wao walipofukuzwa vyuoni kwa kukosa ada. Ni zero kabisa hawa.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  mungu amewapa watu IQ kubwa sana ..
   
 16. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mimi nina hasira tena sana tu, hivi huu ushabiki wa kisiasa bila kujali maslahi ya nchi na watu wake utaisha lini? Watanzania kwakweli inabidi tuamke sasa na tunahitaji mabadiliko makubwa katika uongozi wa nchi. Inasikitisha sana kuona mheshimiwa kiongozi mkuu wa nchi aliyewekwa madarakani na wavuja jasho na walalahoi wa nchi hii leo anatoa kejeli na majibu mabaya kiasi hicho....badala ya kutatua mambo kisomi na kujenga hoja za maana analeta ushabiki wa kisiasa, jazba na ubabe usiokuwa na maana. Kuwakusanya wale wanaccm pale diamond tena wengi wao wakiwa ni vihio na kudai eti ni wazee wa dar ni kashfa kubwa kwa nchi...eti watu jobless wamejaa mtaani tutafukuza na kuajili wengine na bado watu wanashangilia kweli inauma sana, hivi kama kiongozi wa nchi na msomi anajua gharama ya kuwatrain wafanyakazi wapya kwa wakati mmoja? Ni kazi gani hizo zitaendeshwa bila kuwa na wazoefu? Anataka kunambia ni hao wasomi wapya waliotoka vyuo vikuu jana na vyuo vya ufundi tena wakiwa wamesoma kwa miaka mitatu theory bila mazoezi ya vitendo? Pesa za kuboresha maisha ya wafanya kazi kila siku hazipo ila za kutafuna mafisadi ndiyo zipo...pesa za kusafiri na msafara wa zaidi ya watu 120 kila kukicha zipo ila za kuboresha maisha ya wafanyakazi hazipo...pesa za kusafiri na msafara wa kwenda kuona real madrid spain zipo ila za kuboresha maisha ya wafanyakazi hazipo..kuna umuhimu gani kwa wizara moja kuwa na mashangingi zaidi ya 20? Kuna umuhimu gani wa kumpa mkuu wa wilaya shangingi? Goldon brown anasafiri kwa train kufanya campaign, lakini ingekuwa bongo mashangingi na helkopta ndiyo hutawala, inauma sana...kila kukicha vinaundwa vikao visivyokuwa na vichwa wala miguu ili tu wapate nafasi ya kulipana posho kwa pesa za walipakodi. Wafanya kazi ni wakulindwa kama mboni ya jicho kwani ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo yoyote katika nchi..huo ubabe usiokuwa ma mantiki yoyte ndiyo uliyoiponza zimbabwe na ugiriki kwa hivi sasa. Kama yeye aliona kua umuhimu wa kuleta hii hoja kwa wananchi kwa nini basi hakuwaalika wasomi na waandishi wa habari waliobobea tuone kama angepumua kwa hayo maswali....? Watanzania tusikubali kuendelea kuburuzwa na viongozi uchwara, bado tunanafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko ya uongozi na utawala bora katika hii nchi.
   
 17. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #17
  Mar 12, 2013
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Jipeni moyo.
  A Simple Analysis.
  Hebu count idadi ya waliokosoa na Walio support.
  Utapata Jawabu...
   
 18. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #18
  Mar 12, 2013
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  A simple analysis.
  Count idadi ya waliokosoa uzi na walio support.
  Utapata jawabu ni nini Wa TZ wanataka...
   
Loading...