Huu ni mkosi au nyota?

Huu ni mkosi au nyota?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,146
Reaction score
7,683
Jamani mimi nina tatizo moja sielewi ni nini yaani mdada mmoja awe rafiki yangu au demu wangu akiniomba hela basi ujue siku hio akina dada watano au hata watatu wataniomba hela na siku inayo fuata au rafiki yangu wa kiume mmoja akiniomba tu ujue siku hyo wengine wa nne wataniomba na hela sio ndogo sasa mimi sina kazi wala nini nipo kwa baba na mama najiuliza huu ni mkosi au bahati na siku zote ipo hivyo na kila mmoja anasema ana tatizo na ukiangalia tatizo unaona kweli ni kubwa linahitaji msaada sasa kwann wengi waniombe siku moja?

Asipo niomba yeyote yule basi ujue siombwi wala sikii matatizo sasa sielewi naombeni ushauri nifanyaje
 
yani hypothesis yako imekimbilia ushirikina.. hahaha!
pole sana mtanzania..
 
vipi ukipewa wewe, wengine pia wanakupa au ww huwa unatoa tu
 
Wapeni watu vitu nanyi mtapewa, kipimo kile kile upimiacho ndicho utakacho pokea.
 
Sijakuelewa, huna kazi na uko kwa baba na mama, rafiki zako/demu wako wanaelewa hilo? lakini wanakuomba hela, unawapa? kama unawapa unazitoa wapi? na kama huwapi mbona wanarudi tena kukuomba?
 
vipi ukipewa wewe, wengine pia wanakupa au ww huwa unatoa tu

Sijawahi pewa na wote ambao huwa nawapa siku hata nikitaka kuwa jaribu wanatoa visingizio mia kidogoo ni baba na mama angu tuu huwa wana nipa pesa
 
sasa hujui nyota zilipo au makusudi ?
 
Back
Top Bottom