Huu ndiyo utofauti wa Kiba na Diamond

don88

Member
Jan 22, 2013
53
84
KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiyo anajua zaidi kuliko mwingine.

Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.

Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Ali Kiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa, ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, ni vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.

Ambwene Yessaya alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia, ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haonyeshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa. Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau!
 
Diamond anajua kukamata fursa kipindi yupo nigeria kushoot video ya namba one rmx alimuomba Davido waende wote kwny ya Peter wa P.square uko Mond alifanya juu chini nae akabahatika kutokea kwa mapicha na kukutana na wasanii wengine wengi wa Nigeria
P Square walipokuja bongo Peter akaulizwa unamjua Diamond akashangaa ndo nani wabongo walimcheka sn Mond kwamba anashobo mara alivamia harusi ya watu anatafuta kiki
Ila leo watu hao hao ndo wanacheza na kusikiliza kidogo by mond ft p.square
 
Attachments

  • 1471522539105.jpg
    1471522539105.jpg
    8 KB · Views: 211
Aiseeee ulichokisema kina ukweli 10000000% muanzisha thread hiii natamani Uzi huu ungeuamishia kwenye magazeti na social networks zoteeee watu wote waelewe ukweli huu uliokua umekosa mjanja wa kuudadavua........hoja zako zina mashiko yoteeee hazina chuki binafsi hata kidogo....
 
ni kweli kabisa
 
thanks mkuu kwa ufafanuz ulio bora hatutak team humu ukiwa na point ongea kama una ushabik nenda kwenye page zao ukaongee
 
ben pol ndio kiboko wa hawa wote

ila kinachonifanya niwe upande wa domo hustle zake
mtu ambaye hajui kuimba ila anawazidi wenzake umaarufu na fedha kupitia muziki kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake kumbeza mtu kama huyo unahitaji uwe na akili za mashabiki wa kiba
 
Thats diamond utadhani mchaga yani, manake hakuna fursa inayopita mbele yake ikapona, HAPO PA HAJUI KUIMBA mmmmh! pananichanganyaga lakini wengi wape na vile sijui mziki nakubaligi tu yaishe, lakini kwangu mimi sijaona msanii mwenye sauti nzuti na yenye ladha maskioni kama dai, (hapa nadhani MAHABA yametake control sio akili yangu, nyimbo zake ni tamu jamani, zinaimbika, zinachezeka melogy tamu,madhiri yaliyopangwa yakapangika, kwangu itakuwa ngumu sana kunielewesha juu ya kwamba dai hajui kuimba, nikakuelewa, turudi kwenye point ya MSINGI, KIBA NI MWANAMZIKI DAI NI MFANYABIASHARA WA MZIKI, HUO NDIO UKWELI, hata dai alishasemaga angejaaliwaga sauti ya kiba kwenye tasnia ya bongo fleva pasingetosha.
 
KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiyo anajua zaidi kuliko mwingine.

Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.

Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Ali Kiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa, ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, ni vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.

Ambwene Yessaya alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia, ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haonyeshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa. Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau!
Ali kiba anapenda kujilinganisha na diamond ili jina lake lisikauke midomoni mwa watu, kwa mfano sasa hivi kiba kaja na gia ya kushindana kipesa na diamond ili akuze jina lake
 
Inawezekana wewe ukawa zaidi ya kiba.

Wapi alikiba kashindana fedha na mtu yyte?.
 
Inawezekana wewe ukawa kiazi zaidi ya kiba.

Wapi alikiba kashindana fedha na mtu yyte?.
mfano pale diamond alipochangia million 20 yeye kiba akatoa 21 katika shirika hilo hilo moja kama kiba hakutoa zile pesa kwa ajilli ya kiki kwa nini asingechangia sehemu zingine
 
Diamond platnumz anayo sauti nzuri ya kuimba, ila kiba ana sauti NZURI SANA ya kuimba lkn wote wanaimba flat, ukija ktk mashairi diamond platnumz mwandishi mzuri wa mashairi kwani anafuata sheria ya vina na mizani tofauti na kiba, ila ukija upande wa kuziwahi fursa mondi uwezo wake Mkubwa kiba hampati hata robo nazani hata nyinyi mmeona sasa hivi makampuni yanavyomgombania mondi na wasanii wa kimataifa wanataka kufanya nae kolabo. ILA MWISHO WA SIKU KIBA NA DAI HATA WAIMBE VIP HAWAWEZI KUFIKIA UWEZO TDD, VANESA MDEE, BARNABA, MAUA SAMA na BELLA nadhani hata nyie mashahidi ktk nyimbo ya nagharamia kiba alifunikwa na si kiba mpaka linex ktk hii nyimbo yake na bella kapotezwa. Ila mwisho wa siku mafanikio ya DAI naweza kufupisha kwa kusema dogo ANAJITUMA na ANANIDHAM ya Hali ya juu kwa kile anachokipata, siku zote kuwa na kipaji au akili peke yake haziwezi kukusaidia kufanikiwa , ukasahau kujituma na nidham , lazima ufeli, ww hujiulizi kwa nini mtu anakuwa na One kali form 4 lkn six anakula III, IV au 0.
 
Yaan mtu aliyeimba kamwambie,mbagala,nitarejea,moyo wangu,ukimwona,kesho na nyngne nyng unasema hajui kuimba hahaha huwez kuwa sirious wewe,embu hao unaosema wanajua kuimba weka mashair ya nyimbo mojawapo then tufananshe na mashairi ya huyu jamaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom