Huu ndiyo ukweli kuhusu Dr. Slaa

Huu ndiyo ukweli kuhusu Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.

Yeyote anayempigania Rais wa moyoni mwake aende akamtafute huko ilipo hiyo mioyo.
Anayetakiwa ni mgombea u-Rais wa Watanzania, mgombea mwenye uwezo wa kuwashinda CCM na magoli yao ya mikono.
Asiyeliona hilo, ni ama mwanachama safi wa CCM, au mpenzi wa Chama cha Mapinduzi, au mkereketwa wa Lumumba, au kibaraka wa mfumo dhalimu wa CCM.
 
Upuuzi kabisa we ndo unaweka mioyo ya watu juuu na andiko lisilo na nyuma wala mbele. My take :mie ni muumini wa mabadiliko na sitayumbishwa na yeyote ata awe mbowe akiamua kujitoa ktk hii safari mie ntaendelea mpaka dk ya mwisho
But kama Chama kaeni muongee mmalize hii taharuki mturuhusu tuanze kazi tukiwa wamoja....
 
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.
Unafiki ni kitu kibaya sana
 
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.

mkuu chadema inaendesha kisayansi,kiumakini, na kitaasisi zaidi, aiwezi kukurupuka na kujibu propaganda na hoja dhaifu kama hizo zako.. Ulitakiwa kuhoji cdm mmejipangaje kushinda kwa kishindo izo ndyo hoja zenye mashiko.. Hyo mengine Ni ushuzi Tu WA ccm
 
Dr. Yuko bize na majukum ya chama hana muda wakujibizana na wapuuzi. Taarifa ilishatolewa Radio one juzi sasa kama mnataka kuiona sura yake nendeni ofisini mtamkuta.
 
mkuu chadema inaendesha kisayansi,kiumakini, na kitaasisi zaidi, aiwezi kukurupuka na kujibu propaganda na hoja dhaifu kama hizo zako.. Ulitakiwa kuhoji cdm mmejipangaje kushinda kwa kishindo izo ndyo hoja zenye mashiko.. Hyo mengine Ni ushuzi Tu WA ccm
Sawa kamanda.
 
Wakuu salaam sana.

Ziko habari za uzushi kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa, zinaandikwa na kuenezwa na Gazeti la Raia Tanzania kwa siku kadhaa mfululizo sasa.

Uongo huo wa Raia Tanzania leo umeendelea kwa kiwango cha juu zaidi kiasi cha gazeti hilo kuandika kuwa eti Katibu Mkuu Dk. Slaa amekabidhi nyaraka za chama kwa dispatch saa 3 usiku juzi.

Wakuu, hakuna uongo uliokubuhu kama huo. Mtakumbuka uongo huo wa kwamba KM Dk. Slaa anarudisha mali za chama zilienezwa usiku wa juzi mitandaoni na mmoja wa waandishi wa habari aitwae Manyerere Jackton.

Kwa bahati nzuri wakati Jackton (mtu ambaye tunaheshimiana kwa sababu ya kikazi na kitaaluma) wakati akijipatia jukumu la kuandika uzushi badala ya habari na kusambaza uongo badala ya taarifa, binafsi nilikuwepo ofisini physically. Nilikanusha kupitia Jamii Forums ambako alidanganya kwa jina lake, huku 'akijiapiza'.

Uongo huo ambao leo umeshadidiwa na Gazeti la Raia Mwema leo, ulisababisha taharuki isiyokuwa ya lazima kwa waandishi wa habari kadhaa ambao walinitafuta (si Raia Tanzania wala Jackton) na nikawaruhusu waje Ofisini wakitaka usiku huo ili waone namna ambavyo wako watu au chombo cha habari kinaweza kujivika kazi ya kusambaza uongo. Kujeruhi na kuua ukweli.

Kazi ya kujeruhi na kuua ukweli hufanywa sana na maadui wakati wa mapambano kama ilivyo sasa katika mchuano wa kisiasa unaoendelea nchini kuelekea Uchaguzi. Maadui wa CHADEMA wako kazini. Lilitarajiwa hilo.

Wakati Raia Tanzania wakikoleza uongo wao kwa kusema eti 'majira ya saa 3.15 hivi' lilifika Gari aina ya Noah maeneo ya ofisini kisha eti watu wawili wakaingia ofisini wakiwa na mkoba mwekundu, muda huo mimi nilikuwa Ofisini. Hakuna kitu cha namna hiyo kilichofanyika. Labda kama Ni Kwenye Ofisi za gazeti hilo.

Naandika haya nikiwa na uchungu. Kwa sababu huwa sijisikii vizuri kabisa kulumbana na wenzangu (senior fellas) kwenye taaluma ya habari. Tena kwenye mambo ya hovyo yanayohusu kuvunja vunja kabisa misingi ya uandishi wa habari i.e accuracy, facts, truth, objectivity etc.

Inapofikia hatua Gazeti kama hilo linashindwa kabisa kusimama kwenye kitu kiitwacho Social Responsible Journalism inatia aibu na kichefuchefu kwa jamii ya watu makini wanaotaka ushindani wa kisiasa unaoendelea nchini ufanyike kwa misingi ya kila mdau kutimiza wajibu wake inavyotakiwa. Uwajibikaji.

Nimalizie kwa kusema yafuatayo; Katibu Mkuu hajajiuzulu. Nafasi yake haiko wazi kama ambavyo gazeti limepotosha.

Agenda ya kuandika uzushi na uongo kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa na CHADEMA wanayotekeleza Gazeti la Raia Tanzania walioko nyuma yake wanajulikana. Ni agenda ya CCM na Mawakala wao. Wasaliti wa mabadiliko ambao hawajaamini kuwa ndege ya mabadiliko hatimaye inaruka wakiwa wametupwa nje kwa sababu ya usaliti wao wa kufanya kazi za CCM wakiwa ndani ya CHADEMA kabla hawajatimuliwa.

Mojawapo ya malengo ni kuwachanganya wanachama, wapenzi, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA katika kipindi hiki muhimu kinachohitaji utulivu wa mwili, akili na roho ili kupanga mikakati ya kumdhibiti adui na kuweka kila kitu sawa kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Inaitwa diversion. Ili badala ya kuendelea kuwa focused kwenye masuala ya msingi eti tuanze kukimbizana na propaganda!

Aidha, baada ya CCM kusambaratikia Dodoma na sasa iko vipande vipande ikiwa ni mwendelezo wa kuanguka kwa 'himaya' hiyo huku Wananchi wakipandisha mori wa mabadiliko kupitia BVR, lengo jingine ni kutaka kuuhadaa umma wa Watanzania kuwa eti CHADEMA nayo imegawanyika. Wanaota.

Mgawanyiko wa chama cha siasa huwa unatokea kwenye vikao pale ambapo maamuzi yanashindwa kufanyika au kufukiwa. Hakujawahi kutokea jambo la namna hiyo ndani ya chama.

Kwa sababu chama kimejenga utamaduni wa kusimamia misingi katika kusimamia na kuendesha masuala yote, kinaendelea kuwa imara kadri tunavyosonga kuelekea Uchaguzi mkuu.

Uimara huu wa CHADEMA kikijiandaa (kwa kushirikiana na vyama wenza katika UKAWA) kwenda kushinda Uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali, ni mpango wa Mungu. Tujiandae kwa propaganda kubwa zaidi ya hizo za Raia Tanzania.

Tutashinda.

We tulia uyaone acha kupiga mayowe
 
Ndugu mleta hoja pamoja na kukanusha lakini hujajibu swali wapi alipo Dr. Slaa kwa sasa. Dig down kidogo kwa kueleza hali ilivyo ndani na wewe tuone haupigi propaganda.

Nasikia leo ataenda kupokea fomu ya lowassa tusubiri tuone jamani. Kuweni wavumilivu
 
Hivi mnataka kutuambia kuwa mzee Dr. Slaa hawezi kujitokeza hadharani,na kutangaza rasmi kukihama chama?au kusema amejiuzulu ukatibu mkuu ama kusema kuwa yupo kazini kama kawaida?ili kuondoa hizi zinazo semekana ni propaganda????:crying::bowl::bathbaby:
 
Kwa nn slaa asijitokeze hadharani sasa hv. Tatizo nini?
 
Wewe ni nani? kwa nini Mhusika mkuu yupo kimya? kwa nini tukuamini wewe? namna pekee ya kutuaminisha ni mhusika kujitokeza na kusema ukweli! LA sivyo hauna tofauti na Manyerere na hilo gazeti!

huyo jamaa ni mtu wa karibu wa dr slaa na wanafanya kazi ofisi moja (cdm) kama assistant wake,so anacho kieleza hakina shaka hata chembe,kabla haja post huu uzi nilikua naongea nae nika muuliza kulikoni kuhusu habar za dr slaa? akacheka sna na kuni ambia dr yupo achana na uzushi wa magazeti.kukaa kimya kwa dr slaa ni mkakati wa kisiasa ili kuvuta umma kufatilia cdm na kumtoa magufuri kwenye mind za watu kwa kipindi hiki.

jiulize who talks about magufuri kwa wiki nzima hii?
 
Mbona raia mwema wamemqoute Dr.Slaa kabisa?

Hebu tumia akili japo kidogo basi! Watu wanachakachua hadi sauti ya mtu itakuwa maandishi! Kwani nikiandika chochote hapa nikasema nimekuquote ni sawa watu waniamini kuwa kweli wewe uliyasema hayo?
 
Mbona mnakuja na majibu yenu tu TUNAOMBA MTULETEE DR MWENYEWE NDO AKANUSHE
 
Wazee wa Lumumba hawajui kwamba wanazidi kutupa umaarufu zaidi pindi wanapohemkwa na chadema
 
It is confirmed that Dr Slaa and John Mnyika wameondoka Chadema. Ujio wa Lowassa ndani ya Chadema imetajwa kwamba ndiyo sababu kubwa ya wao kuondoka Chadema. Nami ninawaunga mkono kwa uamuzi huo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom