Huu ndiyo ukweli kuhusu Dr. Slaa

Huu ndiyo ukweli kuhusu Dr. Slaa

Status
Not open for further replies.
Huyo Jacton sidhani kama kuna kitu ataandika nije kukisoma haitatokea
 
Mleta mada wala usipatwe gadhabu. Wala mimi sina sababu ya kulumbana hapa. Nilichoposti juzi ndicho hicho hicho ninachoendelea kukisimamia. Hili ni suala la muda tu. Muhimu ni kuwa Dr. Slaa ameiacha Chadema, basi. Huo ndiyo ukweli hata kama kwako na wengine wa aina yako ni mchungu. Hapa hatuleti ushabiki, isipokuwa uhalisia wa mambo. Time will tell.
 
NENO litasimama,mambo yote yatapita LAKINI neo LITASIMAMA.
 
Ah huyu dokta kachoka aachie watu waendelee..naona yeye mwenyewe anapenda hii media frenzy.Kama anaunga mkono si afanye press conference hata ya dk5 kumaliza umbea.Na kama haungi mkono si aseme!Tatizo wanasiasa wanapenda kuwa vichwa vya habari.Eti mke wake anamjibia afu yy yupo kimya.Kweli huyu ndo alitaka awe raisi??ili mke alihutibie taifa au?
Sipo against CDM ila
Dr.Slaa ni so Old News!
 
leo hii ccm mnamtafuta dr.slaa mmekuwa wasemaji wa chadema leo hii ccm duuu haya tufanye tuamini kasepa km mnavyotaka atapunguza wapiga kura wangapi ukiweka na wapiga kura aliokuja nao lowasa la msingi ni kura za wananchi nani ana kura nyingi.ila dr.yupo na haondoki nyie endeleeni kutafuta nyeti za kuku na upepo ndio huu.
 
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.
Nenda makao makuu ya chama ili upate maelezo yatakayo kulidhisha.
 
kamanda Mbona lissu umemuondoa kwenye list? nakumbuka wakati enl anajiunga na cdm mliwauliza hao watatu wako wapi.
Kamanda, Lissu na Mwalimu ni askari watiifu kwa kamanda Mbowe.
 
uliosema ameondoka leta ushahidi hapa mwandishi gani unaandika madai za uchunguzi bila ushahidi thibitishia uma kwamba dr.slaa kaondoka chadema kama unavyosema.
 
maneno mengi huna hata ushashidi nyie kumaliza ubishi wekeni picha ya dr leo akipokea fomu ya lowasa mkishindwa sana tuwekeeni audio ya kukanusha huu uzushi mbona rahisi sana..
 
Wakuu salaam sana.

Ziko habari za uzushi kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa, zinaandikwa na kuenezwa na Gazeti la Raia Tanzania kwa siku kadhaa mfululizo sasa.

Uongo huo wa Raia Tanzania leo umeendelea kwa kiwango cha juu zaidi kiasi cha gazeti hilo kuandika kuwa eti Katibu Mkuu Dk. Slaa amekabidhi nyaraka za chama kwa dispatch saa 3 usiku juzi.

Wakuu, hakuna uongo uliokubuhu kama huo. Mtakumbuka uongo huo wa kwamba KM Dk. Slaa anarudisha mali za chama zilienezwa usiku wa juzi mitandaoni na mmoja wa waandishi wa habari aitwae Manyerere Jackton.

Kwa bahati nzuri wakati Jackton (mtu ambaye tunaheshimiana kwa sababu ya kikazi na kitaaluma) wakati akijipatia jukumu la kuandika uzushi badala ya habari na kusambaza uongo badala ya taarifa, binafsi nilikuwepo ofisini physically. Nilikanusha kupitia Jamii Forums ambako alidanganya kwa jina lake, huku 'akijiapiza'.

Uongo huo ambao leo umeshadidiwa na Gazeti la Raia Mwema leo, ulisababisha taharuki isiyokuwa ya lazima kwa waandishi wa habari kadhaa ambao walinitafuta (si Raia Tanzania wala Jackton) na nikawaruhusu waje Ofisini wakitaka usiku huo ili waone namna ambavyo wako watu au chombo cha habari kinaweza kujivika kazi ya kusambaza uongo. Kujeruhi na kuua ukweli.

Kazi ya kujeruhi na kuua ukweli hufanywa sana na maadui wakati wa mapambano kama ilivyo sasa katika mchuano wa kisiasa unaoendelea nchini kuelekea Uchaguzi. Maadui wa CHADEMA wako kazini. Lilitarajiwa hilo.

Wakati Raia Tanzania wakikoleza uongo wao kwa kusema eti 'majira ya saa 3.15 hivi' lilifika Gari aina ya Noah maeneo ya ofisini kisha eti watu wawili wakaingia ofisini wakiwa na mkoba mwekundu, muda huo mimi nilikuwa Ofisini. Hakuna kitu cha namna hiyo kilichofanyika. Labda kama Ni Kwenye Ofisi za gazeti hilo.

Naandika haya nikiwa na uchungu. Kwa sababu huwa sijisikii vizuri kabisa kulumbana na wenzangu (senior fellas) kwenye taaluma ya habari. Tena kwenye mambo ya hovyo yanayohusu kuvunja vunja kabisa misingi ya uandishi wa habari i.e accuracy, facts, truth, objectivity etc.

Inapofikia hatua Gazeti kama hilo linashindwa kabisa kusimama kwenye kitu kiitwacho Social Responsible Journalism inatia aibu na kichefuchefu kwa jamii ya watu makini wanaotaka ushindani wa kisiasa unaoendelea nchini ufanyike kwa misingi ya kila mdau kutimiza wajibu wake inavyotakiwa. Uwajibikaji.

Nimalizie kwa kusema yafuatayo; Katibu Mkuu hajajiuzulu. Nafasi yake haiko wazi kama ambavyo gazeti limepotosha.

Agenda ya kuandika uzushi na uongo kuhusu Katibu Mkuu Dk. Slaa na CHADEMA wanayotekeleza Gazeti la Raia Tanzania walioko nyuma yake wanajulikana. Ni agenda ya CCM na Mawakala wao. Wasaliti wa mabadiliko ambao hawajaamini kuwa ndege ya mabadiliko hatimaye inaruka wakiwa wametupwa nje kwa sababu ya usaliti wao wa kufanya kazi za CCM wakiwa ndani ya CHADEMA kabla hawajatimuliwa.

Mojawapo ya malengo ni kuwachanganya wanachama, wapenzi, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA katika kipindi hiki muhimu kinachohitaji utulivu wa mwili, akili na roho ili kupanga mikakati ya kumdhibiti adui na kuweka kila kitu sawa kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Inaitwa diversion. Ili badala ya kuendelea kuwa focused kwenye masuala ya msingi eti tuanze kukimbizana na propaganda!

Aidha, baada ya CCM kusambaratikia Dodoma na sasa iko vipande vipande ikiwa ni mwendelezo wa kuanguka kwa 'himaya' hiyo huku Wananchi wakipandisha mori wa mabadiliko kupitia BVR, lengo jingine ni kutaka kuuhadaa umma wa Watanzania kuwa eti CHADEMA nayo imegawanyika. Wanaota.

Mgawanyiko wa chama cha siasa huwa unatokea kwenye vikao pale ambapo maamuzi yanashindwa kufanyika au kufukiwa. Hakujawahi kutokea jambo la namna hiyo ndani ya chama.

Kwa sababu chama kimejenga utamaduni wa kusimamia misingi katika kusimamia na kuendesha masuala yote, kinaendelea kuwa imara kadri tunavyosonga kuelekea Uchaguzi mkuu.

Uimara huu wa CHADEMA kikijiandaa (kwa kushirikiana na vyama wenza katika UKAWA) kwenda kushinda Uchaguzi, kushika dola na kuongoza serikali, ni mpango wa Mungu. Tujiandae kwa propaganda kubwa zaidi ya hizo za Raia Tanzania.

Tutashinda.

Wew jamaa ni mpumbavu namba moja, maelezo yote hayo hamna point hata moja ,umetumia mda mwingi kulalamika ,badala ya kuueleza ukweli wenyewe ,ni hivi karibu kulikuwa na malalamiko kuhusu ujio wa ED CDM mkanza kusema hizo ni propaganda za CCM lakini mwenye akili amejua wenye propaganda ni akina Nani hasa ,
 
Habari zenu wanajamii,chama cha mapinduzi CCM kinagawa rushwa ya Tsh 5,000/= kwa kila mwenye kadi ya chama hicho.Rushwa hizo zinzgawiwa na wagombea wa nafasi ya ubunge na udiwani.Mamlaka husika mpooo.
 
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.




Ilitakiwa Dr. Slaa mwenyewe ajitokeze adharani akanushe habari nzito kama hii, sio wewe umsee kwani yeye hajaiona au yupo nje ya nchi?!

Kukaa kimya kwake lazima tuendelee kuamini lipo tatizo sio bure! Mpaka pale yeye binafsi atakapo kuja kukanusha habari hizo!
 
Mkuu huo kweli upo wapi naona unalalamika tu dhidi ya magazeti.

Kukata mzizi wa fitina tuambie rais wa mioyo yenu yupo wapi.

Kwa njia yeyote ile ulitakiwa kuonyesha Dr.Slaa na Mnyika wapo wapi ili watu wasiendelee kuhoji.

Ahasante.

Mnamtafuta Dr Slaa hammpati ng'o.
Hata muaundike hizo za mara milion bado watz hawawezi kuwaamini, mnang'oka october tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom