Yote kwa pamoja. Ubora ni hafifu na hayapo ya kutosheleza mahitaji!Tatizo no ubora wa makaa ya mawe au idadi ya makaa ya mawe.Mbona kila Sikh hadithi zinabadilika kwa hiyo tumwamini nani?
Lazima tukiri serikali yetu imekosa kabisa intrepreneurial leadership. JPM amejaza serikali yake PhD holders kama vile anataka kufungua university Ikulu. Hajui kuwa PhD holders wengi are the worst managers and worst business people. Tafuta takwimu katika top 100 best performing international business companies, mangapi CEOs wao ni PhD holders.
Uongozi ndani ya serikali ulistahili kuakisi agenda ya Taifa. JPM anasema agenda ya Taifa ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda lakini anaamini wa kutufikisha huko ni lazima wawe watu ambao hata definition ya kiwanda hawajui, sifa yao kubwa ni kuwa makada waaminifu wa chama. Kwa kushindwa kuteua watu wenye uwezo kuisimamia agenda kwa vile wana uelewa, ana guarentee ya 100% ya kushindwa.
Same as it makes you sad!And that makes you happy?
That's your prerogative?Same as it makes you sad!
Mkuu jaribu kurudia kusoma article nzima, huyu jamaa analeta habari za kutunga mno - kama amepewa taarifa hizi kutoka a third party basi wahusika wana lengo la kutaka kuidhalilisha Serikali ya JPJM kwa kutumia adithi za kutunga tu.
Kiongozi gani mwenye akili timamu anaweza kumkorofisha muwekezaji mkubwa na wa maana kama Dangote?? Kwanza Dk.Magufuli akipata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi ndani ya Serikali yake wanataka kumuhujumu Dangote atawafukuza kazi on the spot.
Tuache kuleta adithi za kutunga, utasikia mara Dangote kakosa mkaa wa kutosha kutoka Tanzania, mara Dangote kakataliwa kuuziwa gesi kwa bei nafuu wakati gesi inapatikana huko huko Mtwara ambako hakuna gharama za usafirishaji, mara Dangote kanyimwa umeme - yaani tumejaa roho za kutu kama wachawi, kazi kuitakia mabaya Serikali ya JPJM - hakuna habari njema/nzuri wanazo zileta humu zaidi ya kulahumu chama tawala na Uongozi
[HASHTAG]#achakujipendekeza[/HASHTAG]!
Naona watu wapo busy kumsafisha dangote Kama malaika hakosei.
Hamna serikali ambayo inaweza kumzuia mtu namna hiyo Sema propaganda zenu nao Mmeamua kuishambulia serikali kwa kila inachofanya.
Halafu nahisi Salary Slip na technically ni mtu mmoja sababu kwenye thread Kama hizi Ndo huwa wanajitokeza kupost
Lakini zile za serikali kutoa trioni 1 kununua dawa hata huwaoni...!!
Kuna barabara aliyo kuwa anataka kujenga Bahkresa, serikali ikampiga stop
Hahaha daah!Anajua hata abonyeze wapi ili aisikilize hiyo clip,mwenzio anachojali ni kutoa povu tuu ilimradi ikifika jioni akachukue elfu 7 yake kule makao makuu yao.....
Swali kwa dangote, ,,Hayo makubaliano uliyongia na serikali au na watu binafsi walioko serikalini? Maana kama ni serikalini basi yalipaswa kufuata taratibu maalum sababu hiyo ni raslimali ya watanzania na sio ya watu binafsi.
Wewe dangote kama mfanya biashara mkubwa Africa na tajiri,utawezaje kuwekeza mali bila makubaliano ya kisheria? Kama uliamua kufanya hivo ukijua unakiuka taratibu,huoni kuwa ulikuwa na nia OVU,ya kujinufaisha wewe binafsi na sio umma wa watanzania??
TUTAKUAMINIJE WAKATI ULIKUWA NA LENGO OVU,hata kama umetoa ajira kwa watanzania walio wengi???
Elezea hayo makubaliano kabla ya kulalamika.Siku zote ni lazima kuheshimu makubaliano na mikataba. Mengine yote ni ubabaishaji. Kitazamwe kilichokubaliwa wakati wa uanzishaji wa mradi.
Kwenye jamii ya watu wenye akili na waliostaarabika, ni kosa kubwa kutoheshimu makubaliano. Mwekezaji aliweka mradi wake kwa kuzingatia terms za makubaliano. Huenda kama kusingekuwa na makubaliano hayo asingejenga kiwanda chake Tanzania.
Usipoheshimu makubaliano, wewe ni mhuni na mbabaishaji mkubwa. Serikali haitakiwi kuendesha mambo yake kihuni au kiubabaishaji. Tukilikubali ibabaishaji ndani ya serikali, itakuja kutuletea gharama kubwa kama Taifa siku za mbeleni. Tuukemee uhuni na ubabaishaji ndani ya serikali. Watu wasifanye uhuni serikalini kwa kisingizio cha uzalendo. Uzalendo wa kweli ni kulinda hadhi ya Taifa kwa kuheshimu mikataba. Ni lazima, siyo hiari, kuheshimu mikataba.