Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Suleiman Jaffo akiwa katika ziara Mkoani Ruvuma katika Mkaa ya Mawe ili kujionea hali halisi ya utunzaji wa mazingira amesema biashara ya Makaa ya Mawe imekuwa kubwa Duniani.
Katika ziara hiyo ya Juni 21, 2023 Jaffo amesisitiza kuwa Tanzania ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa hizo lakini mchakato wote lazima uzingatie utunzaji mazingira.
Amesema “Mfano Mgodi wa Ruvuma ni mkubwa na unazalisha wastani wastani Tani 200,000 kwa mwezi, pia nimefarijika migodi niliyotembelea inafanya shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe na kurejesha udongo sehemu walizochimba.
“Nimewataka wawekezaji wengine wa migodi mingine Nchini wahakikishe wanapochimba rasilimali madini, wanarejesha maeneo waliyofanya uchimbaji kama inavyofanyika Ruvuma.
“Nimemuelekeza Mtendaji Mkuu wa NEMC, Dkt. Samwel Gwamaka kutembelea migodi mingine yote hasa ya Kanda ya Ziwa ambao wanachimba lakini hawarejeshi udongo.”
Ameongeza kuwa katika kuzingatia utunzaji wa mazingira, ametoa maelekezo ya maji tiririka kutoka migodini kuwa yanapokutana na maji ya mvua inakuwa changamoto katika ardhi.
Pia ametoa maelekezo kuwa magari yanayosafirisha madini hayo yawe na mfumo mzuri wa ufunikaji wakati wanapokuwa wamebeba Makaa ya Mawe kwa kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wananchi kuwa wanadondosha makaa hayo mtaani.
Naye, Mtendaji Mkuu wa NEMC, Dkt. Samwel Gwamaka aliyekuwa ameandamana na Waziri katika ziara hiyo amesema kuna fursa nyingi ambazo zimezidi kujitokeza.
Amesema “Tuna maeneo mengi yenye Makaa ya Mawe, nawashauri wale wenye leseni ya kuchimba washirikiane na Serikali katika kukuza soko lao kwa kuwa mambo kama haya huwa yanaendana na teknolojia, majanga kama ya vita yanatokea mara chache.
“Pamoja na kutumia fursa ya kuchimba lazima mazingira yaendelee kutunzwa na kuhifadhiwa, katika ziara yaetu tumeona kuwa masharti ya utunzaji mazingira yanafuatwa na Kampuni zote tulizotembelea.
“Bado kuna maeneo machache ambayo tungependa waendelee kuyafangia kazi kubwa ikiwemo ufungwaji wa migodi ambalo ni takwa la kisheria, inatakiwa kuzingatiwa hasa katika Migodi ya Makaa ya Mawe ambayo inatumia sehemu kubwa.
“Wakati huohuo baada ya kuchimba na maeneo yaliyochimbwa yanarejesha katika hali ya awali kwa kuwa tunaamini vizazi vijavyo vinaweza kuendekeza maeneo hayo.”