Huu ndio ubabaishaji serikali imemfanyia Dangote alifikia hadi kutengeneza reli lakini imeshindikana

Kuwekeza Tanzania ni sawa na kuchezea shilingi kwenye tundu la choo.

Alafu mbona Magufuli hii issue anaonekana kutoipa uzito?

Hii ni awamu ya uhakiki na wala si awamu ya viwanda.
Hii ni laana hata Mungu atatuadhibu...mwanchi chukua hatua 2020
 
Hii story ina shida aisee.
Makaa ya mawe yapo ya kutosha na kila siku yanatoka unaposema wanapata tani 15 huu ni upotoshaji kwa sababu gari zinazobeba makaa zinapakia tani 32 per trip.
Na gari zinazotoka katai kwa siku moja ni zaidi ya 100 kwa makadilio ya chini.
Na sio kwamba anataka tani 2000 kwa matumizi ya siku moja.

Ni kampuni gani ilipewa tenda ya kusafirisha makaa ya mawe tika katai mpaka mtwara??.
Panye ukweli usemwe ukweli ila sio huu upotoshaji.
Na tani moja ya makaa ya mawe ni shiling 86,000 bei ya katai ukisafirisha kwa tani moja bei ya jumla haifiki 120,000 wakati ya kutoka S.A ni dola 100+ na ukiweka kwenye shilingi ni 200,000+.
Na kwa sasa njia ya kutoka katai mpaka mtwara ipo katika hari nzuri.

Maoni yangu.
Ni vyema serikali ikakaa na mwekezaji waende sawa lakini iwe win win situation na sio kumpa feva zisizo na tija mwekezaji.
Makaa ya mawe na gesi anunue kwa bei shindani kama wenzake na sio yeye ndo aoewe kipaumbele wakati soko la cement ni la ushindani.
Siku zote ni lazima kuheshimu makubaliano na mikataba. Mengine yote ni ubabaishaji. Kitazamwe kilichokubaliwa wakati wa uanzishaji wa mradi.

Kwenye jamii ya watu wenye akili na waliostaarabika, ni kosa kubwa kutoheshimu makubaliano. Mwekezaji aliweka mradi wake kwa kuzingatia terms za makubaliano. Huenda kama kusingekuwa na makubaliano hayo asingejenga kiwanda chake Tanzania.

Usipoheshimu makubaliano, wewe ni mhuni na mbabaishaji mkubwa. Serikali haitakiwi kuendesha mambo yake kihuni au kiubabaishaji. Tukilikubali ibabaishaji ndani ya serikali, itakuja kutuletea gharama kubwa kama Taifa siku za mbeleni. Tuukemee uhuni na ubabaishaji ndani ya serikali. Watu wasifanye uhuni serikalini kwa kisingizio cha uzalendo. Uzalendo wa kweli ni kulinda hadhi ya Taifa kwa kuheshimu mikataba. Ni lazima, siyo hiari, kuheshimu mikataba.
 
Halafu kuna watu bado wanampigia makofi huyu Janga la Taifa kila kukicha. Bilionea mkubwa duniani kama huyu anakuja kuwekeza nchini halafu anakuwa frustrated na wanasiasa uchwara kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu. Afungashe tu aondoke zake. Serikali hii iko busy kuikanyaga katiba ya nchi na hawana kipaumbele kingine chochote kile.
Akina Lizaboni na unafiki wao hutawaona hapa. Hili suala ni la kitaifa. Halafu kuna watu wamekifanya chama kama ndo taifa. Hivi huwa wakiwa peke yao na nafsi zao huwa wanapata hisia zipi? Utakuta ndugu zao na majirani hali mbaya, dhoofu kabisa halafu wanapiga tararira hapa.
 
Mkuu jaribu kurudia kusoma article nzima, huyu jamaa analeta habari za kutunga mno - kama amepewa taarifa hizi kutoka a third party basi wahusika wana lengo la kutaka kuidhalilisha Serikali ya JPJM kwa kutumia adithi za kutunga tu.

Kiongozi gani mwenye akili timamu anaweza kumkorofisha muwekezaji mkubwa na wa maana kama Dangote?? Kwanza Dk.Magufuli akipata taarifa kwamba kuna baadhi ya viongozi ndani ya Serikali yake wanataka kumuhujumu Dangote atawafukuza kazi on the spot.

Tuache kuleta adithi za kutunga, utasikia mara Dangote kakosa mkaa wa kutosha kutoka Tanzania, mara Dangote kakataliwa kuuziwa gesi kwa bei nafuu wakati gesi inapatikana huko huko Mtwara ambako hakuna gharama za usafirishaji, mara Dangote kanyimwa umeme - yaani tumejaa roho za kutu kama wachawi, kazi kuitakia mabaya Serikali ya JPJM - hakuna habari njema/nzuri wanazo zileta humu zaidi ya kulahumu chama tawala na Uongozi wake, nani kawambieni vyama vya upinzani vingeshinda uchaguzi saa hizi Tanzania ingekuwa ni Taifa lililo jaa maziwa na asali - nani??
Lazima tukiri serikali yetu imekosa kabisa intrepreneurial leadership. JPM amejaza serikali yake PhD holders kama vile anataka kufungua university Ikulu. Hajui kuwa PhD holders wengi are the worst managers and worst business people. Tafuta takwimu katika top 100 best performing international business companies, mangapi CEOs wao ni PhD holders.

Uongozi ndani ya serikali ulistahili kuakisi agenda ya Taifa. JPM anasema agenda ya Taifa ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda lakini anaamini wa kutufikisha huko ni lazima wawe watu ambao hata definition ya kiwanda hawajui, sifa yao kubwa ni kuwa makada waaminifu wa chama. Kwa kushindwa kuteua watu wenye uwezo kuisimamia agenda kwa vile wana uelewa, ana guarentee ya 100% ya kushindwa.
 
Kwani tungekubali kiasi anachohitaji dangote ni tani 10,000 sisi tumuuzie tani 15 tunazozalisha, zilizobaki akachukue south afrika wakati sisi tunaboresha uzalishaji wetu kungekuwa na shida gani wataalamu wa uchumi na mahesabu?
 
Serikali inapaswa kujua kuwa hapa inadeal na dangote ambaye ni mnijeria na wala sio mchina, na afrika nzima hakuna mjanja kwenye pesa kama mnijeria hapigwi kizembe!
Mbona yale ma Richmond,escrow,Epa,sijui kikoda hawayakatii viuno? yaani FISIEM kuna majitu majinga? haya yanatakiwa kung'olewa kucha kutobolewa macho shenzi sana.
 
Shida yetu kujifanya wajuaji wa kila jambo kuendesha mambo kwa majungu, hila, jeuri na visasi....kama tunalalamikia waliokubaliana na Dangote group of companies..mbona wanatoka ktk serikali ya chama hicho hicho? Mbona msiwaulize kwa ufafanuzi hata kama mnahisi.kuwa wana maslahi..sasa ndiyo mumkomoe mwekezaji.!!...jamanieee...majungu hayajengi..ebo!!!
Na kila siku wanakutana wanapigiana simu,
Sembuse sisi tunawaona tu kwenye tv na magazeti
 
Kwani tungekubali kiasi anachohitaji dangote ni tani 10,000 sisi tumuuzie tani 15 tunazozalisha, zilizobaki akachukue south afrika wakati sisi tunaboresha uzalishaji wetu kungekuwa na shida gani wataalamu wa uchumi na mahesabu?
Kwani hata tukiyaacha si wachina watayachukua tu au Mzindakaya na wanawe watajimilikisha hayo makaa ya mawe ya liganga
 
Sababu hasa za kujenga kiwanda Mtwara zilikuwa zipi? Upatikanaji wa mali Ghafi, gesi au kulikuwa na sababu za kisiasa? Je, isije ikawa kiwanda kilijengwa akitegemewa mkulu angetokea pande hizo ila upepo ukabadilika ghafla hivyo tunarudi kule kule kama yaliyompata Nchimbi?
 
Huwezi kusema kwa uhakika kwamba Serikali ikubali wawekezaji kama Dangote wanunue makaa nje ya Tanzania na kuwapa upendeleo kwenye biashara yao ati tu kwa sababu Dangote ana pesa nyingi. Huu ni ujinga wa kupindukia ambao JF imeukumbatia, Tanzania as a nation hatuwezi kupelekeshwa kama pimbi ati tu kwa sababu tuwaridhishe watu flani flani kufanya biashara zao wanavyotaka. Wanaweza kwenda kuwekeza nchi nyingine, na wawekezaji wengine watapatikana. Serikali iwe makini na hawa wezi wa kisasa.
 
Hakika kwa clip hii namuomba mh Rais aingilie kati ili kutimiza ndoto yake ya Tanzania ya viwanda pamoja na kulinda ajira za watanzania na kodi zao wanazochangia serikalini ,pia kulinda muonekano wetu kimataifa hasa katika kuwavutia wengine naamini iwapo Kama Dangote atakifunga hiki kiwanda basi familia nyingi zitaumia pia serikali itapoteza kodi kubwa.Naamini mkuu wa nchi yuko makini sana siku yoyote unaweza kutokea gafla hapo kiwandani.Nakuombea maisha marefu najua kwako ni Tanzania kwanza.HAPA KAZI TU.
 
Back
Top Bottom