Huu nao ni ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu nao ni ufisadi

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jan 12, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Umewahi kwenda kwenye duka la vifaa vya computer ukakuta kuna matangazo kama WE DON’T INSTALL UNLICENCED SOFTWARES , au MICROSOFT CERTISFIED PARTNER , MICROSOFT PREFERED PARTNER 2008 ? Tembelea maduka mengi ya vifaa vya computer jijini dare s salaam utakuta matangazo haya wengi hawapendi kujiuliza uliza matangazo yale yana maanisha nini haswa na kama wanajua wanachomaandisha wenye maduka haya je watahakikisha vipi ?

  Haya unasoma matangazo hayo kisha ingia ndani ya duka lolote lile nunua computer watakwambia hatuweki operating system kama iko basi unakuta imetoka nayo huko huko majuu lakini maajabu mule ndani wanatoa cd zake wengi wenye maduka hayo huwa wanasema hizo cd zinaibiwa na kwenda mikononi mwa watu ambao sio waaminifu ila mbona mtu akinunua computer yenye operating system hapewi cd zake kama inavyotakiwa ingawa nyingine zinakuwa na programu maalumu inayokuwezesha kutengeneza cd ingine kwa ajili ya recovery baadaye .

  Kama unakumbuka mwaka jana kipindi cha aprili watu kadhaa maduka kadhaa yalivamiwa na watu wa hati miliki pamoja na wengine wanaohusika na mambo ya programu toka kusikojulikana , maduka mengi yalifungwa baada ya kusikia jamaa wanaenda duka kwa duka na workshop kwa workshop .

  Wale waliofanikiwa kukamatwa tuliwasikia katika vyombo vya habari , lakini maduka hayo hay oleo ukipita mjini unaona bado kuna nembo hizo za MICROSFOT PREFERED PARTNER 2009 na kadhalika , Maduka haya yalikuwa na tenda za kufanya kazi katika idara zingine nyeti za serikali waliwauzia serikali programu ambazo ni bandia na zenye walakini

  Serikali kwa kushirikiana wenye maduka haya wameendelea kupeana tenda za kuuza programu hizi na bidhaa zingine katika idara zake mfano mzuri ni chuo cha afya muhimbili wale waliouza software kadhaa pale Duka lao linadaiwa karibu mil 200 kama fidia kwa kuuza programu bandia lakini muhimbili wameendelea kuwa vipofu wanaendelea kuhudumiwa na watu hawa .

  Serikali na wadau wengine wa ICT wanatakiwa wajue maduka haya yanavyoendelea kufanya hivi wanadidimiza sekta hii na kuumiza wengine wengi ajira nyingi zinapotea hapa fikiria kama dare s salaam tungekuwa na maduka angalau 5 yanayouza programu halali ajira ngapi zingepatikana ? nyingi sana tu .

  Au kama kuwabana inashindikana basi kuwe na utaratibu mtu anavyochukuwa leseni ya biashara yake kwamba leseni yako inakuruhusu kufanya hivi na vile kuuza hiki na kile hivi hutakiwi huna wataalamu wa kutoa support katika uwanja huo au wenye uelewa katika uwanja huo .

  Nashindwa hata nielezeje kwa ufupi hawa wenzetu wanadidimiza ICT katika ulingo huo kwa makusudi kabisa na hawachukuliwi hatua zozote za kisheria au kinidhamu , tunataka tufike mahala nasi tuweze kusema kitu katika majukwaa makubwa ya kimataifa Jamani

  Kama tunaungana mkono katika vita dhidi ya ufisadi – huu pia ni aina ya ufisadi unaoumiza wengi na kusosesha vijana wengi ajira na njia muafaka za kuweza kupanua wigo wao wa taaluma zao
   
Loading...