Huu mwaka 4 mstaafu hajalipwa na mfuko wa PSSSF

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika inasikitisha sana kuona Serikali inayojinasibu kuwa ni serikali inayowajali wananchi waje wakati wapo wastaafu wana miaka 4 hawajalipwa mafao yao

Kuna mzee wangu alistaafu julai 2018 lakini mpaka leo mfuko wa PSSSF umeshindwa kumlipa mafao yake mwaka 2020 mzee aliambiwa mafao yake yamekwama kwa sababu ya kukosekana majalada binafsi.

Mzee alipeleka nyaraka zote walizozihitaji yakiwemo na majalada binafsi ya sehemu alizofanya kazi na kuambiwa cag anayahitaji.

Toka amekabidhi huu ni mwezi wa 7 bado anasubiri mafao yake hakika wastaafu wanateseka sana nchi hii

Tunaiomba Serikali ifike mahali iwalipe hawa wazee wastaafu kwani hawana kipato chochote zaidi ya mafao yao.
 
Juzi tu wamenunua ndege nne sijui. Kwanini wastaafu wasilipwe stahiki zao? Hizo hela za wastaafu ni haki zao siyo fadhila.
 
Pssf ni kero hao wajinga, mafao yako bado uwapigie magoti, ni bora wangekuwa wakweli kuwa pesa hakuna labda kwa miaka mitatu wapunguze usumbufu wa kuwafatafata
 
Hakika inasikitisha sana kuona Serikali inayojinasibu kuwa ni serikali inayowajali wananchi waje wakati wapo wastaafu wana miaka 4 hawajalipwa mafao yao

Kuna mzee wangu alistaafu julai 2018 lakini mpaka leo mfuko wa PSSSF umeshindwa kumlipa mafao yake mwaka 2020 mzee aliambiwa mafao yake yamekwama kwa sababu ya kukosekana majalada binafsi.

Mzee alipeleka nyaraka zote walizozihitaji yakiwemo na majalada binafsi ya sehemu alizofanya kazi na kuambiwa cag anayahitaji.

Toka amekabidhi huu ni mwezi wa 7 bado anasubiri mafao yake hakika wastaafu wanateseka sana nchi hii

Tunaiomba Serikali ifike mahali iwalipe hawa wazee wastaafu kwani hawana kipato chochote zaidi ya mafao yao.
Too much!👊
 
Back
Top Bottom