Mfuko wa PSSSF walipeni wazee wastaafu mafao yao

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Hakika inasikitisha sana mahangaiko wanayopitia wazee wetu wastaafu kudai Mafao yao. Kuna Mzee alistaafu Julai 2018 lakini mpaka leo anahangaishwa na Mfuko wa PSSSF kulipwa Mafao yake ya Serikali kuu.

Mzee huyu aliamua kwenda Dodoma; kufuatili Mafao yake Septemba 2019 akaahidiwa mwezi Novemba lakini mpaka hivi leo hajalipwa na ifikapo Julai 2020 atakuwa katimiza Miaka 2 ya kudai Mafao.

Hebu tujiulize; anaishije na familia yake?
 
Kama anapata zile monthly pension walau zitasaidia kidogo, ingawa ule mzigo wenyewe bado una umuhimu wake.

Mimi nadhani hii mifuko iwekewe penalt/interest kadiri inavyochelewesha.

Haiwezekani ukae na fedha za mtu in 2 yrs halafu bado unakuja kumlipa kiasi alichotakiwa apewe 2yrs back.

Ni upumbavu kuwatesa watumishi walioitumikia nchi hadi kustaafu, wakati wengine wameshia njia kwa kukosa uadilifu.

Tuwaenzi wazee wetu.
 
Kama anapata zile monthly pension walau zitasaidia kidogo,ingawa ule mzigo wenyewe bado una umuhimu wake.

Mi nadhani hii mifuko iwekewe penalt/interest kadiri inavyochelewesha.

Haiwezekani ukae na fedha za mtu in 2 yrs afu bado unakuja kumlipa kiasi alichotakiwa apewe 2yrs back.

Ni upumbavu kuwatesa watumishi walioitumikia nchi hadi kustaafu,wakt wengine wameshia njia kwa kukosa uadilifu.

Tuwaenzi wazee wetu.
Hii ya penalt taasisi nyingi za serikali inabidi zipewe aiseee
 
Sijui nimesoma uzi gani humu JF,

Ila kiufupi hiyo mifuko imekauka.

Hao jamaa wa pensheni walichezea pesa enzi za JF kujenga maghorofa makubwa kama kitega uchumi kumbe yakawa kifukuza uchumi kisha alivyoingia mkuu ndio akapigilia msumari wa mwisho ili kukausha na kutoboatoboa mifuko.
 
Wahuni AKA maccm wameshakwapua pesa zote za wastaafu bila hata woga na kuwaacha wazee hao bila uwezo wowote wa kugharamia gharama zao za maisha za kila siku.

Hakika inasikitisha sana mahangaiko wanayopitia wazee wetu wastaafu kudai Mafao yao. Kuna Mzee alistaafu Julai 2018 lakini mpaka leo anahangaishwa na Mfuko wa PSSSF kulipwa Mafao yake ya Serikali kuu.

Mzee huyu aliamua kwenda Dodoma; kufuatili Mafao yake Septemba 2019 akaahidiwa mwezi Novemba lakini mpaka hivi leo hajalipwa na ifikapo Julai 2020 atakuwa katimiza Miaka 2 ya kudai Mafao.

Hebu tujiulize; anaishije na familia yake?
 
Linapokuja swala la watumishi wa umma kwa utawala huu Ni huruma sana, wanaigiza kuwa sawa wakiwa mbele ya mzee lakini ukweli ni kwamba AMEWAUMIZA SANAAA!
 
Mimi bado naona huu mchezo wa serikali na taasisi zake kutowajali wastaafu wa mashirika. Wastaafu wa ATCL yaani Air Tanzania hadi leo wana pigwa dana dana kati ya Katibu Mkuu Kiongozi, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, ATCL, na PSSSF. Japo mahakama ilisha toa hukumu kwa wastaafu hao kulipwa lakini serikali inakataa kutekeleza baada ya wizara UUM kuahidi kulipa. Nao PSSSF hawataki kabisa kulipa japo sheria inawataka kuwalipa wastaafu halafu wao waidai ATCL/Serikali hii ni kwa mujibu wa sheria namba 2 ya 2018 kuhusu PSSSF.
Dhuluma kwa wazee haifai. Kumbukeni nanyi mna wazee mnapo watesa hawa wastaafu naye Mungu atawatesa wenu kwa njia nyingine hadi pale mtakapo jitambua.
 
Muheshimiwa Raisi tunaomba aingilie hili kwa dhati mtu anastaafu mshahara unakoma kazi imeishia hapo hata viposho na vimarupurupu vimekoma mshahara unakoma anaanza upya kuzunguka na bahasha wengine wanarudi huku maofisini kuomba omba matibabu nayo yanakoma mpaka aanze process upya hana hata nauli kama alikuwa muadilifu kuanzia nyumba hana anapanga Mungu amguse Muheshiwa kuwaonea huruma wanakufa kabla hata ya kupata viinua mgongo
 
Hakika inasikitisha sana mahangaiko wanayopitia wazee wetu wastaafu kudai Mafao yao. Kuna Mzee alistaafu Julai 2018 lakini mpaka leo anahangaishwa na Mfuko wa PSSSF kulipwa Mafao yake ya Serikali kuu.

Mzee huyu aliamua kwenda Dodoma; kufuatili Mafao yake Septemba 2019 akaahidiwa mwezi Novemba lakini mpaka hivi leo hajalipwa na ifikapo Julai 2020 atakuwa katimiza Miaka 2 ya kudai Mafao.

Hebu tujiulize; anaishije na familia yake?
Ni uonevu mkubwa, tumekuwa tukiwatumikia Wabunge maana wao hata siku ya mwisho ya muda wa utumishi haijaisha tayari pesa yote ya mafao inaingia kwenye akaunti zao. Huu ni unyanyasaji mkubwa kwa wavuja jasho waliolitumikia Taifa.
 
Back
Top Bottom