Mkurugenzi PSSSF hebu walipeni mafao yao wazee wastaafu wanateseka sana

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,233
2,000
Hakika kuna Mzee kanisimulia na kunionyesha Nyaraka zake jinsi anavyohangaika na kulipwa Mafao yake baada ya Kustaafu July 2018.

Mzee huyo anadai Mafao yake Mfuko wa PSSSF Kitengo cha Wastaafu waliokuwa Serikali Kuu.Mzee huyo ameenda Dodoma mara 2 bila mafanikio .

Nakuomba Mkurugenzi wa PSSSF hebu Wasaidie Wazee hawa Wanasumbuliwa na Watendaji wako kuambiwa tunashughulikia njoo kesho.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,478
2,000
Mleta mada bwana...siku nyingi jaribu kufikiria ni mada ipi ya kuleta humu jamvini pia ujue hii ni Afrika na zaidi ni Tanzania.

Iwe wanaharakati,wanasiasa, watawala ,viongozi wa dini nk awawezi kuliongelea ili kamwe...wameweka ndimi tumboni.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,994
2,000
Mzee zile hela huwa washkaji sijui wanazifanyia shughuli gani maana huwa wanazimind utadhani ni jasho lao.....

Ila ni hela za laana kuzitumia kwa mambo binafsi ni sawa na kutumia hela ya michango ya msiba/rambirambi kama mtaji wa biashara haitafika mbali.

Dhuruma huwa haina faida mbele bali huwa inakuja na majanga...
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,351
2,000
Ila huyo Mzee atakuwa na tatizo binafsi kwenye mchakato wake na si kwa wastaafu wote.

Nina ushuhuda wa wazee 2 wamestaafu June& October 2019 wamekaa 8 months tu wakapata chao bila kwenda Dodoma wala Dar.

Mkuu,Kama ni kweli nakushauri tembelea ukurasa wa psssf kule Instagram (customer care ni 100% kama siyo bongo vile)

Just DM utajibiwa in 0 minutes,kwa kuwatumia namba ya uanachama tu watamuambia huyo Mzee shida ni nini au mchakato umefikia wapi.
 
Junior Nicky

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
476
500
Aisee huu mfuko ni hatari sana,juzi nilifika kwenye ofisi zao pale samora kufuatia mafao yangu asee huu mfuko unachangamoto nyingi sna kwenye utaratibu wa kupata stahiki yako,nilifika pale ofisini kuna muda nilipatiwa form ya kujaza nikajaza na viambatanishi vyote nilifanikiwa kukamilisha na nikapeleka ofisini kwao then wakaniambia nimpelekee mwajiri wangu baada ya wao kuniambia hivyo nilifanikiwa kupeleka kwa mwajiri wangu,kilichotokea ile form ilirudishwa na kumwaambia mwajiri wangu kuna una taratibu mwingine wa kuomba niandike barua ya kuhamisha michango yangu kutoka mfuko wa lazima kwenda hiari,kwa kweli sikimuelewa mwajiri wangu ili nibidi nirudi tena pale ofisini kwao nikiwa na maform yangu.ndipo nikahoji kuna haja gani ya mimi kuandika ya kumuomba mkurugenzi kuhamisha michango yangu alafu yy kupitia uongozi wa psssf watanipa utaratibu mpya kwakweli wanatukatisha tamaa yaan unakuta mtu unafuatilia pesa zako kama unaomba kazi jamani...

Kilichonisikitisha zaidi nilikakutana na mama anafuatilia mafao yake tangu mwaka jana alijaribu kufuatilia akaambiwa tutakupigia simu utaratibu utakapokuwa tayari mama yule alivuta subra kwa muda kaona kimya akaamua kuja tena (juzi)ile siku ya alhamisi ndipo tulipokutana pale ofisi ya Psssf samora akiwa ajui aende wapi maana dana dana zimekuwa nyingi ndipo nilipomshauri akaonane na zone manager wa psssf anaweza kumpa ufumbuzi juu ya suala lake.

Kwakweli mfuko wa psssf una changamoto nyingi sana.nini kifanyike kupunguza changamoto hizi.
-Watoe utaratibu husika kwa wale ambao wanafuatilia mafao,sio leo umejazaa form na kukamilisha taratibu zote baadae unaambiwa kuna kitu fulani kinatakiwa kifanyike ili hali form uliojaza inaeleza viambata vyote vinavyohitajika ya nini tena kupewa taratibu nyingine ambazo hazikuanishwa kwenye ile form
-Watupe utaratibu wa kutuambia lini pesa yako inatoka toka pale uliporejesha form ya uanachama...hawa Psssf hawana huo utaratibu wa kutuambia
-Wasitusumbue wanachama pindi tunapofuatilia stahiki zetu kwa kutupa ahadi za uongo za kila siku kesho kesho.kinachotakiwa waseme pesa yako itaingia baada ya miezi miwili hili litampunguzia mizunguko yule anayefuatilia pesa zake.
-Walipeni wastaafu stahiki zao kwa wakati.
 
road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
277

Hali ni mbaya pesa hakuna
 
mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
25,728
2,000
Na wanasema eti wanapigania wanyonge,mara tuna maheraaa mengi sana...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom