Huu muujiza wa maombi na mimi umenishtua

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,242
103,943
Asubuhi ya jana nikiwa nasikiliza redio kipindi cha dini. Kwenye kipindi kulikuwa na mchungaji anaombea wenye shida na wengine wakawa wanatoa ushuhuda.

Jamaa mmoja akapiga simu kueleza shida yake kwamba kuna hela zimepotea kiutatanishi hapo kwake. Kabla hajamaliza mchungaji akadakia na kuanza kumuelezea mambo ya hapo kwake. Akamwambia hapo kuna mapepo makali sana na pia kupotea hizo pesa kumesababisha mtafaruku wa yeye na mke. Mchungaji akamwambia jamaa hizo hela zipo ndani zimefichwa moja ya room.

Palepale mchungaji akiwa live kituo cha redio akaanza kumpa maelekezo jinsi ya kuzipata hizo pesa. Akamwambia nyumba yake ina vyumba vitatu anaende chumba fulani. Kupitia redio ikawa tunasikia movement za kuelekea chumbani.

Ile hali sikuipotea vizuri nikabadilisha station.

Kwa kweli bado sijashawishika kama kuna maombi ya kiwango hiki. Yaani inakuwa kama upo live na Yesu mwenyewe kumbe ni mchungaji tu.
 
ulifanya la maana kubadili station ila kulileta hapa ni kama bado linakutatiza.

puuzia tu hakuna haja ya kuendelea nalo.
 
subiri upoteze hela ndani chief hata buku tu, halafu nawewe mtwangie...
 
Unachotaka kusema ni kwamba dunia hii haina watu wa aina hiyo mkuu???
Namjibia....

Hakuna watu watu wa haina hiyo...
Kila mtu ana limit ya uwezo katika kila jambo..

MUNGU Aliweka limit kwa kila mtu kwa kila jambo kwa dhumuni maalumu ...

Back to the topic,,,kitendo hicho kimevuka limit,,
Ni sawa kujua mtu anawaza nini-haiwezekani
 
Asubuhi ya jana nikiwa nasikiliza redio kipindi cha dini. Kwenye kipindi kulikuwa na mchungaji anaombea wenye shida na wengine wakawa wanatoa ushuhuda.

Jamaa mmoja akapiga simu kueleza shida yake kwamba kuna hela zimepotea kiutatanishi hapo kwake. Kabla hajamaliza mchungaji akadakia na kuanza kumuelezea mambo ya hapo kwake. Akamwambia hapo kuna mapepo makali sana na pia kupotea hizo pesa kumesababisha mtafaruku wa yeye na mke. Mchungaji akamwambia jamaa hizo hela zipo ndani zimefichwa moja ya room.

Palepale mchungaji akiwa live kituo cha redio akaanza kumpa maelekezo jinsi ya kuzipata hizo pesa. Akamwambia nyumba yake ina vyumba vitatu anaende chumba fulani. Kupitia redio ikawa tunasikia movement za kuelekea chumbani.

Ile hali sikuipotea vizuri nikabadilisha station.

Kwa kweli bado sijashawishika kama kuna maombi ya kiwango hiki. Yaani inakuwa kama upo live na Yesu mwenyewe kumbe ni mchungaji tu.
Mchawi huyo si mchungaji....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom