OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Kila upande katika ndoa au mahusiano unafanya kila namna kuhakikisha mwenzake hachepuki. Namna ni nyingi ikiwa ni pamoja na kuridhishana kitandani, kutunziana heshima, kutafuta pesa na matunzo mazuri kwa mke/muwe. Lakini pia ipo namna ya kufuatiliana kwenye simu na mitaani kujua anafanya nini na nani.
Je, mkwara wa kumuweka wazi mwenzi wako kwamba kama atachepuka mahusiano yataishia hapo, unasaidia? Ninajua kutokana na hali na hofu ni ngumu kwa mwanamke wa ndoa kutoa mkwara kama huo kwa mmewe. Lakini vipi kwa mwanamme? Mkwara huu ukiutoa kwa mke kwamba akichepuka na ndoa inaishia hapa, unasaidia?
Ninauliza hivyo kwa sababu kuna kesi ya jamaa yangu ambaye alimpa kipondo mkewe na kulazimisha kuachana mpaka leo baada ya kumkamata pasipo shaka mkewe akiwa na mahusiano na mwanaume mwingine. Nikaijiwa na wazo, kwamba kama jamaa msimamo wake ni huu si ni bora angempa msimamo mkewe kwamba siku ukitoa nje ya ndoa ninakuacha, pengine angejiongeza na kuchukua hatua mapema?
Nawasilisha