Sababu zinazowafanya wanawake wachepuke kwenye mahusiano

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Asilimia mpaka 45 ya wanawake waliopo kwenye ndoa wanachepuka.

Kumbuka sababu za mwanamke kuchepuka ni nyingi na hakuna namna wewe kama mwanaume unaweza kufanya ili kumzuia mkeo asichepuke. Haijalishi wewe mwanaume ninani na una nini. Mkeo akiamua kuchepuka atachepuka tu, huwezi kumzuia.

Kuna vitu unaweza kufanya kama mume ili kuzuia uwezekano wa mkeo kuchepuka na vinaweza kusaidia hilo.

Lakini mwisho wa siku ni uamuzi wake BINAFSI yeye mwenyewe mkeo kuamua kwamba hataki kuchepuka kwa sababu yoyote ili kukuheshimu wewe na ndoa yenu.

Wanawake wanakutana na vishawishi vingi karibu kila siku.

Tofauti na mwanaume kwamba mpaka uamue au upange kwamba nataka nimtongoze mwanamke fulani, mwananmke yeye hapangi, akitoka tu nje kuna mwanaume fulani lazima atamtaka. Wanasema mwanamke mzuri wa kawaida anaweza kutongozwa walau na wanaume tofauti 180 kwa mwaka.

1. Ikiwa mumewe ni mtu asiyejiamini


Wanawake wana akili sana tofauti na wanaume wengi wanavyofikiri na kuwaona.

Mwanamke akikusoma na akakuhitimisha kwamba hujiamini na kuwa umekufa kwake mazima basi hiyo inaweza kuwa ni sababu ya yeye kuchepuka. Unaambiwa dume lenye uhakika halimchungulii mkewe.

Mwanaume ukiona kila mara upo bize unamwambia mkeo asichepuke, asikusariti basi tegemea atafanya hayo bila wasiwasi wowote. Ni kama mtoto anapokua kama mzazi upo bize kila siku kumwambia usifanye hiki usifanye kile kila siku hayo ndiyo mahubiri yako kwake amini kuna siku lazima atafanya hayo hayo unayomkataza kila siku. Atataka kujua kuna nini hasa? Mbona baba yupo bize sana na kunikataza hili kwani kuna nini hasa huko? Na atataka ajaribu aone matokeo. Hata mkeo unao uwezo wa kumwambia mara moja moja mke wangu naomba usichepuke, naomba unilindie penzi langu kwako.

2. Ni mwanamke mpenda hela sana


Je ni kweli amekupenda kutoka moyoni na amekupenda wewe kama ulivyo au amekupenda sababu una pesa?

Kuna baadhi ya wanawake mawazo yao yote masaa yote yapo kwenye hela tu. Mwanamke wa aina hii yeye yupo bize zaidi na pesa ulizonazo na bata unazoweza kumfanyia kuliko hata kukuwaza au kukujali wewe. Kwa hiyo mara utakapoishiwa pesa au mara tu maisha yako yatakapoyumba basi uwe na uhakika mwanamke huyo lazima atachepuka. Kwa sababu hitaji lake kubwa siyo mahusiano au uwepo wako, hitaji lake kubwa muda wote ni pesa. Tabia ya kupenda pesa kupita kiasi ndiyo sababu kubwa na sababu ya kwanza ya wanawake wengi waliopo kwenye ndoa kuchepuka. Kwa mwanaume ni kupoteza muda wako bure kuishi na mwanamke wa aina hii.

Mwanamke huyu kuishi naye itakulazimu uwe na uhakika na pesa wakati wote. Na shida kubwa hapa ni kuwa mara zote kutakuwa na mwanaume mwingine mwenye pesa nyingi wewe sasa sijui utafanyaje kumdhibiti

3. Ikiwa mwanamke anapitia magumu kwenye ndoa yake

Watu wengi huwa wanafikiri ndoa ni sherehe na furaha tu kila siku jambo ambalo si kweli. Ndoa ina misimu na vipindi vingi. Kuna wakati wa furaha tu, pia kuna wakati wa kugombana au kutofautiana. Kila ndoa ina shida zake. Kila ndoa ni ya pekee.

Kila wawili uwaonao kuna muda fulani wananuniana na kugombana.

Ndivyo maisha yalivyo. Badala ya kutoka nje ya ndoa na kutafuta faraja na tulizo ni vizuri ukikaa na mumeo na kuyatatua matatizo yenu ikiwa yanaweza kutatulika. Changamoto zipo kwa ajili ya binadamu na unapozivuka na kuzishinda ndiyo maana hasa ya kuishi.

Sasa kuna mwanamke mwingine badala ya kupambana na tatizo uso kwa uso anaanza kutafuta njia rahisi za kulikimbia tatizo na kuchepuka.

4. Ikiwa mwanamke hafikishwi kileleni


Hili siyo kosa la mwanamke moja kwa moja. Shida kubwa ya maisha ya ndoa ni kuwa mara nyingi mnafundishwa namna ya kusali pamoja, namna ya kupendana na kujaliana lakini hakuna wakati wowote mtafundishwa namna ya kutoshelezana kitandani. Wazazi, Viongozi wa dini na walezi wenu wengine wote hakuna hata mmoja atakayewaeleza tendo la ndoa linafanyika hivi na hivi.

Wanawake nao kwa asili wanategemea mwanaume utakuwa unafahamu namna ya kumfikisha kileleni na kumtosheleza mkiwa kitandani. Kwa bahati mbaya zaidi ya asilimia 80 ya wanaume wengi wanapoingia kwenye maisha ya ndoa huwa hawajui namna nzuri na sahihi ya kushiriki tendo la ndoa.

Wanaume wengi hawajui namna ya kumfikisha mwanamke kileleni, wengi wana tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume. Wanaume wengi wameathirika na punyeto tangu wakiwa mashuleni.
 
kila siku mnalalamika wanawake viumbe wa ajabu ila mnaowat..mb ndio nyie nyie

wanaume mkitulia ndio wanawake watatulia

unalia mkeo asichapwe we unakula vya watu unategemea uliyemla mkewe nae atamfanya nn mkeo

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Ukweli mchungu huuo. Wanaume tuache ujinga wakusema wanawake viumbe wa ajabu. Hawa ni viumbe watamu...na kitamu kinaliwa basi
 
Point no 4..;;;;
NGUVU ZA KIUMEEEEEEEE

wanaume wasasa mna majanga HAMSIMAMISHI....period

Vijana wadogo wanatumia Erecto...etc kwajili ya erection....na anasema kbs anatatizo...NGOMA HAISIMAMI....

Mwanamke atavumilia atachoka naye binadamu ..Ana hamu km nyie mlivyo nazo....wanaume

Kwahiyo wala msiwaze sana kuhusu kuchapiwa...ilimradi heshima imo ndani ya ndoa.......na magonjwa mnajilinda


Shuhuda nnazo nyingi sana wanalalamika wanawake....hawafanywi....
N ziko za wanaume. Wenyewe wanaconfess shughuli kwao sio tena..ngoma imelala doro...si asubhi akiamka wala katikati ya usiku
.mtu ht 40s hajafika

JITAFAKARINI....
 
Point no 4..;;;;
NGUVU ZA KIUMEEEEEEEE

wanaume wasasa mna majanga HAMSIMAMISHI....period

Vijana wadogo wanatumia Erecto...etc kwajili ya erection....na anasema kbs anatatizo...NGOMA HAISIMAMI....

Mwanamke atavumilia atachoka naye binadamu ..Ana hamu km nyie mlivyo nazo....wanaume

Kwahiyo wala msiwaze sana kuhusu kuchapiwa...ilimradi heshima imo ndani ya ndoa.......na magonjwa mnajilinda


Shuhuda nnazo nyingi sana wanalalamika wanawake....hawafanywi....
N ziko za wanaume. Wenyewe wanaconfess shughuli kwao sio tena..ngoma imelala doro...si asubhi akiamka wala katikati ya usiku
.mtu ht 40s hajafika

JITAFAKARINI....
Umeolewa
 
Sasa mbona ume comment kama binti wa mtaani
tatizo.hampendi kusikia ukweli....

Nguvu za kiume ni shida....period...

Uliza madaktari..uliza wahusika wa sekta za afya.

.kundi linaoongoza kwa kukosa nguvu zakiume ni kina nani kwasasa....

20s - 40s......
Kuambiwa mkae kwa kutulia mkigongewa ndio comment km.bint wa kiswahili

Mnatakaga raha wenyewe tu
...ila wakike hawana hamu eti
 
Kama wanaume wengi wako hivi, huko nje wanapochepuka huwa wanafikishwa kileleni na wanawake wenzao?
Wanaume wengi hawajui namna ya kumfikisha mwanamke kileleni, wengi wana tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume. Wanaume wengi wameathirika na punyeto tangu wakiwa mashuleni.
 
Mwanamke atavumilia atachoka naye binadamu ..Ana hamu km nyie mlivyo nazo....wanaume

Kwahiyo wala msiwaze sana kuhusu kuchapiwa...ilimradi heshima imo ndani ya ndoa.......na magonjwa mnajilinda


Shuhuda nnazo nyingi sana wanalalamika wanawake....hawafanywi....
N ziko za wanaume. Wenyewe wanaconfess shughuli kwao sio tena..ngoma imelala doro...si asubhi akiamka wala katikati ya usiku
.mtu ht 40s hajafika

Komenti yako inasikitisha sana.,, Umeongea kwa hisia sana Bidada...

Unawasaidiaje hao vijana wasioenda mnara,, wewe kama Dada yao?
 
Back
Top Bottom