Huu mkutano wa wanawake wa leo umenchekesha sana

okoyoko

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
2,664
3,639
Habarini,

Kongamano lilirushwa ITV leo asubuhi, Topic yao walidai usawa katika uongozi serikalini baina yao na wanaume.

Walilalamika kuwa wanakutana na changamoto kama kuombwa rushwa ya ngono nilicheka sana, coz kwenye rushwa kuna mtoaji na mpokeaji, kwani wao wanalazimishwa kutoa? Wakikataa kutoa rushwa ya ngono, hio rushwa itakuwepo?

Fact ingine ambayo hawakugusia ni kuwa wanawake wengi ndo wana-encourage wanaume wapokee rushwa ya ngono, mwanaume ukiwa na post muhimu kazini au serikalini, basi wanawake wengi (sio wote) watakutega kingono we, au watajirahisi kwako ili wapate kazi /fedha /Status /connection

Bahati yao sikuwemo kwenye hilo kongamano kwa maana jipu hili ningetumbua.
 
Wako busy!kwani ukiombwa kama hutaki si unakataa au kama unataka toa,naona hapo mbaya kama unaleweshwa pombe halafu unafanywa bila kujitambua hilo ni jambo lingine,lakini unaombwa,unapelekwa lunch,unapangiwa hoteli au lodge ya kukutana,unaingia chumbani,unavua nguo yaani mpaka hapo hujalazimishwa ni kwa hiari yako mwenyewe halafu unalaalmika kuwa umeombwa rushwa ya ngono.Sidhani kama kuna kuwa na terms kuwa nipe hiyo nikupe kazi hakuna kitu kama hicho,ukiombwa kama hutakii sema sitaki.
 
Whether they give or refuse, it delights women just the same to have been asked to offer something....
 
Akikataa ndo kazi hapati wala,sasa hapo ukute ndo unashida na kazi na hali yako ni ngumu
 
TAKUKURU chunguzeni hawa wanawake wanaotoa rushwa ya ngono maana ni kinyume cha sheria za kazi.Wanawake wengi ndo wanajirahisisha kwa boss zao na sioni kama kuna ulazima wa wao kutoa rushwa ya ngono hata kama wameombwa.
 
akikataa ataipata hiyo nafasi anayoita?
Kwahiyo nyie mna vyeti vingine tofauti na vyeti vya kawaida vinavyohitajika?Ukiombwa vyeti lazma utoe kwa mujibu wa sheria ila ukiombwa ngono ni sharti ukatae maana haipo kwenye masharti ya kazi/ajira.
 
Akikataa ndo kazi hapati wala,sasa hapo ukute ndo unashida na kazi na hali yako ni ngumu
Kwahiyo upo tayari ku sacrifice maisha yako kwa ajili ya kazi?Sasa kazi yenyewe itakuwa na amani/raha gani hali ya kuwa una wasiwasi na afya yako baada ya kutoa rushwa ya ngono?Badilikeni tafadhali mnajidhalilisha.
 
Ni kutokutulia tu, mbona wapo waliotema kazi kwa kuombwa mzigo na shida wanazo. Tunawafahamu.
Wenye ujasiri huo wapo,lakini kwanini hao waajiri wafanye mambo kua complicated na mtu vigezo vya kupata kazi anavyo?
 
Kwahiyo upo tayari ku sacrifice maisha yako kwa ajili ya kazi?Sasa kazi yenyewe itakuwa na amani/raha gani hali ya kuwa una wasiwasi na afya yako baada ya kutoa rushwa ya ngono?Badilikeni tafadhali mnajidhalilisha.
Badilikeni na nyie mnaofanya mambo marahisi kua magumu.

Nitakuja kwako kuomba kazi,utaomba ngono nitaweka ngumu,kazi sawa nitapata utaendelea kunifatilia nitapindua utaanza kunifanyia visa hatimae nipoteze kazi kama sio kukosa amani na ofisi kabisa...

Wewe kwanini usifate weledi wa kazi/cheo chako?
 
Back
Top Bottom