Huu Mgogoro na mzee unanipa wakati mgumu sana, Naombeni nanyi Mnishauri kama mmewahi kutana na changamoto kama hizi maishani

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Nadhani na umri nao umekuwa changamoto kwa mzee maana maamuzi yake yamekuwa kwa sasa hata hayaeleweki vizuri. Tumeingia mgogoro kwa jambo dogo sana. Lilianzia kwenye birthday yangu mwaka huu. Alitaka ninunulia gari ambalo kiuhalisia mimi niliona ningekuwa najichoresha sana. Lingekuwa gari pekee hapa nchini. Kiasi kwamba ingekuwa kila ninapopita watu wanajua Bill Lugano yuleee anapita. Binafsi huwa sipendi watu wajue nina uwezo au natoka familia ya kitajiri.

Mzee toka anunue visima vya mafuta kule uarabuni amekuwa tu na nia ya kutaka kutu spoil kila wakati. mimi maisha hayo nilikataa kabisa. naishi maisha ya kiugumu. ndo kisa cha kuamua kuja kuishi huku Oysterbay ambayo ni maeneo ya watu wa kawaida tu ukilinganisha na nyumba zetu nyingine za UK, Usa, Canada, Sweden, Egypt,VSouth Africa, Norway, Russia na China. yeye anaona mimi kuja kuishi Tanzania ni kujitesa sana.

Sasa shida ilianza kwenye birthday. Alitaka kuninunulia Rolls-Royce Cullinan 2022 hii si bei kubwa sana ni USD 360,000 mpaka 400,000 customized bado kusafirishisha na ushuru. hizi gari huwa zinasafirishwa kwenye meli ya peke yake au kwa ndege. Bila kuchanganywa na usafiri au gari nyingine. Nakumbuka nilienda TRA kuwauliza Ushuru wake wakasema kwa hii gari ni mpaka Mkurugenzi wao afanye kikao na Mh. Rais, Waziri wa Fedha, Mkuu wa Majeshi, Waziri wa Ulinzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali kujadiliana suala hili. nikaona mlolongo mrefu sana. Wanasema kwenye kikokotoleo chao hii gari haipo. Basi nikaanza kuona hapo sasa itakuwa issue niachane nao tu maana gari si ya gharama sana ila sasa ina maana Tanzania nzima ntakuwa nayo peke yangu?

Mzee nilimwambia hili akasema si shida wao waseme tu wanataka tsh ngapi na kuhusu mafundi na spares zake atanunua gari mbili moja ndo nitumie nyingine iwepo kwa ajili ya kutoa spares inapoharibika au kugongwa. na pia alitaka atume na mafundi wawili waje waishi huku kwa ajili ya kuangalia na mmoja jamaa ambaye angekuwa ndiye mtaalamu wa kuiosha hii gari. maana hata car wash za kuiosha hii gari kwa huku hamna. of course hili nilimwambia maana hizi gari zangu nyingine mara nyingi huwa nazipeleka Nairobi kwenda kuoshwa vizuri kwa week mara moja. kule angalau wana car wash za kisasa na wataalamu waliosomea kuosha magari.

Sasa hilo likawa limepita issue nyingine imekuwa ni kuhusu mke. mzee anataka nioe binti mmoja mrembo ambaye ni mtoto wa bilionea mmoja huko Uarabuni. yule binti aliponiona siku ya kwanza alichanganyikiwa kabisa... aliwaambia wazazi wake mimi ndo mume aliyekuwa anamsubiria.mimi nlishangaa sababu huu si utamaduni wa kiarabu hata kidogo. akawa anataka tuwe wapenzi nlikataa sababu sikuwa kwanza nimefuata zile taratibu za kuanza kudate mtu. basi akazila kula kama masaa 3 hivi .... ikawa issue familia yake ikawa imechanganyikiwa ikaita wataalamu wa saikolojia toka USA, UK na Canada wakaja kuongea na binti kumsihi angalau ale kitu. binti aligoma kabisa akasema atakuwa anakula cake, chocolate na ice cream ili awe bonge awakomoe wazee wake kwa kupoteza shape.

hili jambo lilivuruga sana familia yao. waliitwa mpaka watu mashuhuri duniani. akiwepo aliyekuwa Rais wa Marekani kipindi cha nyuma. Binti aliendelea kufanya msisito huo ndo ikabidi wazee wake wawasiliane na mzee kumwambia hiyo issue. mzee aliniambia kuwa nimuoe huyo binti ni mrembo sana .. ni kweli na ananipenda sana. ni kweli. lakini nilimwambia mzee najua binti ni bikra n.k lakini lazima apitie zile process zangu ...sasa mzee anaona kama watajisikia vibaya n.k

Mimi sioni sababu ya kupindisha kanuni na taratibu zangu eti kwa kuwa mtu atajisikia vibaya. hiyo kujisikia yeye vibaya mimi inanihusu nini? so hapo pia tumeingia kwenye mgogoro. sababu mzee anasema anataka agharamie harusi yote sehemu yoyote tunayotaka kwenda kufungia harusi hapa Duniani. nimemkatalia kuwa hilo silitaki maana atakuwa ananidekeza nami sitaki. anasema honey moon tuende mwezini.... ndo tukakae huko na kufanya mchakato wa kumpatia mimba mke. yaani mtoto akapatikane mwezini. hilo jambo naona mzee ni kama anataka ku control maisha yangu. na ndo kisa cha mimi kuamua kuja kuishi Tanzania niwe mbali na familia ili niwe huru.

Huyu binti kingine nachowaza ni mtoto wa kitajiri. sasa nawaza nikimwoa yeye ni kama naenda kuongezea tu utajiri kwao na kwetu.ni bora nitamfute binti wa kitanzania maisha ya kawaida kama mtoto wa Bakhresa au Marehemu Mengi ndo nioe. ili nao wafadikie na utajiri wangu. sasa kwenda tena kuoa mtoto wa Bilionea wa Kiarabu huko Dubai... na huku TZ kuna familia ambazo ni kipato cha chini si ni kuwaongezea wenye nacho?

Nikawa nawaza huku nitampata watu mtoto mzuri wa kiafrika ambaye ana akili na uelewa mkubwa?awe na figure nzuri na lugha at least azungumze min 5 kwa ufasaha? au awe tayari kwenda kusoma katika nchi tano tofaut tofaut. au hata akitaka aletewe watalaamu wa lugha waje mfundisha hapa hapa si mbaya.

Nimewaza sana haya maisha..nikamwaza binti ambaye aligoma kula vyakula vingine akawa anakula tu cake na chocolate ili awakomoe wazazi wake. nikawa kwa masikitiko na share na mfanyakazi mmoja mrembo hapa ofisini nikashangaa anasema anatamani angekuwa yeye.... nilishtuka sana. yaani anatamani kam angekuwa anakula tu chocolate na cake akishushia ice cream siku zote? wakati mwenzake anafanya hivyo kuonesha ana huzuni na anataka kuwakomoa wazazi wake? anyway sijui watanzania wamekuaje kwa sasa.

Wadau kama umewahi kukutana na mikasa kama hii yangu ulifanyaje? najua ningewaita washauri wangu but nimeona pia nijue maisha ya watu wa kipato chenu yakoje. kama mzazi anakulazimisha akununulie gari ambalo unajua utakuwa nalo nchini peke yako ungefanyaje? Maana mimi nakwepa ile kujulikana kila wakati nilipo. pili anakushauri umwoe binti mrembo mtoto wa bilionea mwenzie na wewe hutaki unafanyaje? Na kukutaka honey moon mkafanyie mwezini, haya yote yananipa hard time leo siku nzima sijawasiliana na mzee na simu zake sipokei. najua hachelewi kufunga safari kuja tanzania kujua naendeleaje. but nami nataka nimwoneshe tu kuwa sikubaliani naye katika hayo mambo.
 
Nadhani na umri nao umekuwa changamoto kwa mzee maana maamuzi yake yamekuwa kwa sasa hata hayaeleweki vizuri. Tumeingia mgogoro kwa jambo dogo sana. Lilianzia kwenye birthday yangu mwaka huu. Alitaka ninunulia gari ambalo kiuhalisia mimi niliona ningekuwa najichoresha sana. Lingekuwa gari pekee hapa nchini. Kiasi kwamba ingekuwa kila ninapopita watu wanajua Bill Lugano yuleee anapita. Binafsi huwa sipendi watu wajue nina uwezo au natoka familia ya kitajiri.

Mzee toka anunue visima vya mafuta kule uarabuni amekuwa tu na nia ya kutaka kutu spoil kila wakati. mimi maisha hayo nilikataa kabisa. naishi maisha ya kiugumu. ndo kisa cha kuamua kuja kuishi huku Oysterbay ambayo ni maeneo ya watu wa kawaida tu ukilinganisha na nyumba zetu nyingine za UK, Usa, Canada, Sweden, Egypt,VSouth Africa, Norway, Russia na China. yeye anaona mimi kuja kuishi Tanzania ni kujitesa sana.

Sasa shida ilianza kwenye birthday. Alitaka kuninunulia Rolls-Royce Cullinan 2022 hii si bei kubwa sana ni USD 360,000 mpaka 400,000 customized bado kusafirishisha na ushuru. hizi gari huwa zinasafirishwa kwenye meli ya peke yake au kwa ndege. Bila kuchanganywa na usafiri au gari nyingine. Nakumbuka nilienda TRA kuwauliza Ushuru wake wakasema kwa hii gari ni mpaka Mkurugenzi wao afanye kikao na Mh. Rais, Waziri wa Fedha, Mkuu wa Majeshi, Waziri wa Ulinzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali kujadiliana suala hili. nikaona mlolongo mrefu sana. Wanasema kwenye kikokotoleo chao hii gari haipo. Basi nikaanza kuona hapo sasa itakuwa issue niachane nao tu maana gari si ya gharama sana ila sasa ina maana Tanzania nzima ntakuwa nayo peke yangu?

Mzee nilimwambia hili akasema si shida wao waseme tu wanataka tsh ngapi na kuhusu mafundi na spares zake atanunua gari mbili moja ndo nitumie nyingine iwepo kwa ajili ya kutoa spares inapoharibika au kugongwa. na pia alitaka atume na mafundi wawili waje waishi huku kwa ajili ya kuangalia na mmoja jamaa ambaye angekuwa ndiye mtaalamu wa kuiosha hii gari. maana hata car wash za kuiosha hii gari kwa huku hamna. of course hili nilimwambia maana hizi gari zangu nyingine mara nyingi huwa nazipeleka Nairobi kwenda kuoshwa vizuri kwa week mara moja. kule angalau wana car wash za kisasa na wataalamu waliosomea kuosha magari.

Sasa hilo likawa limepita issue nyingine imekuwa ni kuhusu mke. mzee anataka nioe binti mmoja mrembo ambaye ni mtoto wa bilionea mmoja huko Uarabuni. yule binti aliponiona siku ya kwanza alichanganyikiwa kabisa... aliwaambia wazazi wake mimi ndo mume aliyekuwa anamsubiria.mimi nlishangaa sababu huu si utamaduni wa kiarabu hata kidogo. akawa anataka tuwe wapenzi nlikataa sababu sikuwa kwanza nimefuata zile taratibu za kuanza kudate mtu. basi akazila kula kama masaa 3 hivi .... ikawa issue familia yake ikawa imechanganyikiwa ikaita wataalamu wa saikolojia toka USA, UK na Canada wakaja kuongea na binti kumsihi angalau ale kitu. binti aligoma kabisa akasema atakuwa anakula cake, chocolate na ice cream ili awe bonge awakomoe wazee wake kwa kupoteza shape.

hili jambo lilivuruga sana familia yao. waliitwa mpaka watu mashuhuri duniani. akiwepo aliyekuwa Rais wa Marekani kipindi cha nyuma. Binti aliendelea kufanya msisito huo ndo ikabidi wazee wake wawasiliane na mzee kumwambia hiyo issue. mzee aliniambia kuwa nimuoe huyo binti ni mrembo sana .. ni kweli na ananipenda sana. ni kweli. lakini nilimwambia mzee najua binti ni bikra n.k lakini lazima apitie zile process zangu ...sasa mzee anaona kama watajisikia vibaya n.k

mimi sioni sababu ya kupindisha kanuni na taratibu zangu eti kwa kuwa mtu atajisikia vibaya. hiyo kujisikia yeye vibaya mimi inanihusu nini? so hapo pia tumeingia kwenye mgogoro. sababu mzee anasema anataka agharamie harusi yote sehemu yoyote tunayotaka kwenda kufungia harusi hapa Duniani. nimemkatalia kuwa hilo silitaki maana atakuwa ananidekeza nami sitaki. anasema honey moon tuende mwezini.... ndo tukakae huko na kufanya mchakato wa kumpatia mimba mke. yaani mtoto akapatikane mwezini. hilo jambo naona mzee ni kama anataka ku control maisha yangu. na ndo kisa cha mimi kuamua kuja kuishi Tanzania niwe mbali na familia ili niwe huru.

huyu binti kingine nachowaza ni mtoto wa kitajiri. sasa nawaza nikimwoa yeye ni kama naenda kuongezea tu utajiri kwao na kwetu.ni bora nitamfute binti wa kitanzania maisha ya kawaida kama mtoto wa Bakhresa au Marehemu Mengi ndo nioe. ili nao wafadikie na utajiri wangu. sasa kwenda tena kuoa mtoto wa Bilionea wa Kiarabu huko Dubai... na huku TZ kuna familia ambazo ni kipato cha chini si ni kuwaongezea wenye nacho?

nikawa nawaza huku nitampata watu mtoto mzuri wa kiafrika ambaye ana akili na uelewa mkubwa?awe na figure nzuri na lugha at least azungumze min 5 kwa ufasaha? au awe tayari kwenda kusoma katika nchi tano tofaut tofaut. au hata akitaka aletewe watalaamu wa lugha waje mfundisha hapa hapa si mbaya.

nimewaza sana haya maisha..nikamwaza binti ambaye aligoma kula vyakula vingine akawa anakula tu cake na chocolate ili awakomoe wazazi wake. nikawa kwa masikitiko na share na mfanyakazi mmoja mrembo hapa ofisini nikashangaa anasema anatamani angekuwa yeye.... nilishtuka sana. yaani anatamani kam angekuwa anakula tu chocolate na cake akishushia ice cream siku zote? wakati mwenzake anafanya hivyo kuonesha ana huzuni na anataka kuwakomoa wazazi wake? anyway sijui watanzania wamekuaje kwa sasa.

wadau kama umewahi kukutana na mikasa kama hii yangu ulifanyaje? najua ningewaita washauri wangu but nimeona pia nijue maisha ya watu wa kipato chenu yakoje. kama mzazi anakulazimisha akununulie gari ambalo unajua utakuwa nalo nchini peke yako ungefanyaje? maana mimi nakwepa ile kujulikana kila wakati nilipo. pili anakushauri umwoe binti mrembo mtoto wa bilionea mwenzie na wewe hutaki unafanyaje? na kukutaka honey moon mkafanyie mwezini... haya yote yananipa hard time leo siku nzima sijawasiliana na mzee na simu zake sipokei. najua hachelewi kufunga safari kuja tanzania kujua naendeleaje. but nami nataka nimwoneshe tu kuwa sikubaliani naye katika hayo mambo.
Nimecheka kifala aisee
 
Kuna kitu wanaita daydreaming ila kuota sio kubaya ila kumbuka ukiwa unaona choo ndotoni huo ni mtego usikitumie. .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom