Huu mfumo wa kulipia matibabu kwa kadi, hii imekaaje kwa wenye familia kubwa?

frank nyantu2

JF-Expert Member
Jun 26, 2016
298
162
MIX K’ndoni yaja na mfumo mpya hospitali na vituo vya afya vya serikali By Newsroom TZA
onJuly 18, 2016 COMMENTS

Baada ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi kukutana na waganga wafawidhi wa hospitali zilizoko ndani ya wilaya ya Kinondoni na kujadili changamoto mbalimbali zinazokabili hospitali za wilaya hiyo.

Leo July 18 2016 amekuja na taarifa njema ambapo ametambulisha mfumo mpya wa malipo ya afya kwa kutumia kadi katika hospitali na vituo vya afya vya serikali katika wilaya hiyo.

Kadi hiyo itakua inauzwa kwa sh 40,000 na itatumika kwa mwaka mzima kwa mtu mmoja, lengo la kuanzisha mfumo huu ni kudhibiti ufujaji wa fedha ambazo wafanyakazi ambao sio waadilifu walikuwa wanazifuja. Kadi hizo ambazo ziko chini ya manispaa na zinatarajiwa kuanza kutumika kuanzia July 25 2016.
 
Lakini insurance ni muhimu kuliko unavyodhani. Hata kama huumwi ovyo.

Ni kweli kabisa ila kinachokatisha tamaa ni pale unapoona huduma zinakuwa hafifu huku wanaoshikilia huo mfuko wakitajwa kuhonga mamilioni ya fedha kwa baadhi ya watu kwa maslahi binafsi, rejea ufujaji wa fedha wa ule mfuko wenye makao yake kule karibu na bandari
 
Back
Top Bottom