Huu mdororo wa uchumi wa dunia ni wa makusudi, kuna kitu kinatengenezwa

ndonger

JF-Expert Member
Jan 21, 2018
874
1,533
1. Walianza na kuidorora dunia kwa covid

2. Sasa ni Ukraine na Taiwan

Ukiangalia player mkuu hapa ni USA.

Huyu jamaa kuna jambo analitafuta si kawaida. Sasa ni dhahiri kuna mpango mkuu unaoendelea ambao sisi watu wa kawaida hatuelewi ila wakubwa wanaelewa.

Hii michezo USA ana uzoefu nayo miaka mingi sana.. hata Ukwasi wake ni kutokana na michezo kama hii

Keshafanya haya kwenye WW1 na WW2, keshafanya kwenye kunyongonyeza eastern hemisphere na middle east

Na kote huku anafanikiwa...

Lengo lake kwa muongo huu sjui ni nini ila kiukwel hali hii inadororesha sana uchumi wa nchi zetu hizi kapuku.

"Shaban kaoneka, shaban kaoneka, shaban kaoneka"

"Mandonga mtu kaazi naongea"
 
Nadhani Marekani imeona nafasi yake ya Usupa pawa iko hatarini kupotea.

Mbinu kama kuyawekea vikwazo vya kiuchumi mataifa yanayotaka kuipiku zimeonekana hazitoshi ikizifanya peke yake, kwa sasa wanatumia ule msemo wa Waswahili kwamba, “Ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya.”

Analichokoza taifa analoliwinda kwa namna ambayo ni lazima lijibu, likijibu linatangazwa duniani kwamba ni taifa lisilozingatia demokrasia, kwa hiyo linaingizwa kwenye vita na kuwekewa vikwazo na mataifa washirika.

Kikubwa ni acheze karata zake vizuri, washirika wake wakiona mbinu anazotumia zinawagharimu sana wataanza kumkataa.
 
Watafute Wasabato wakupe mchongo kamili wa kinacho endelea, mwaka 98 Kuna vitabu vyao nilisoma nikaona ni vya kusadikika ila sasa naanza kuona mambo niliyoyasoma mwaka 98 yanatokea live.

Nasubiri jambo moja ambalo vitabu hivyo viliandika kuwa ipo siku ambayo dini zote zitalazimishwa kuabudu siku moja yaani Jumapili.

Hili nalo likitokea naenda kubatizwa usabatoni.
 
Hilo ni lazima litokee mkuu kwa maana chochote kilichoandikwa kwenye BIBLIA ni lazima litimie
Hili nalo likitokea naenda kubatizwa usabatoni.
 
Maybe
FB_IMG_1659213015426.jpg
 
Back
Top Bottom