Kunguru anamsikitikia huyo kidege (kinda) kwa kuwa umauti 100% ndo umemfikia. Kunguru anasikitika kinafiki kwani hawezi kumwepushia Umauti japo uwezo anao. Kindege Atauawa na kuliwa ni chakula kwa kunguru. Hicho kindege hakijui wala hakitambui hatari iliyo mbele yake. Kipo kipo tu.
Ni kweli mkuu. Kuna shemeji yangu mmoja aliniambia ukiwa na matatizo ukajifungia ndani unaweza kufa ukidhani wewe ndiye mwenye matatizo makubwa pekee, lakini ukitoka na kusikiliza matatizo ya wengine utajiona kumbe uko kwenye hali nzuri.William Shakespeare aliwahi kusema kwamba "Nililia sana nilipokuwa sina Viatu lakini nilinyamaza baada ya kukuta Mtu hana Miguu"
Hivyo ndivyo ilivyo hata leo hii...Unaweza kumsimulia Mtu kitabu Kizima cha Matatizo yako halafu yeye akakupeleka kwenye Library(Maktaba) ya Matatizo yake....na huko ndipo unapokutana na Vitabu 6,278 halafu kitabu cha kwanza kufunua unakuta Matatizo yako wewe yameishia kwenye Dibaji tu (Fore words).
View attachment 3296518
Ni kweli kabisa 100%.Kuna watu wanapitia matatizo kwenye haya maisha wakikusimulia kuna unaweza jiona hauna shida kabisa.
Yep. Huenda uzi huu ukawa ni Tiba kwako. Usikae kimya ndani kwako i.e. usijifungie ndani, nenda huko usikie na kwa wenzio halafu pia usikie walifanyaje fanyaje kukabiliana na changamoto zilizowasibu.Najaribu kuupitia huu uzi kila wakati ili nielewe lakini nashindwa kwa hiki nachopitia.
Anyway nitavumilia na kujikaza.
Kuna jamaa yangu hali anayopitia kwasasa nikimfikiria naona mapito yangu hayakuwa kitu.Ni kweli kabisa 100%.
Hata wahenga walisema: "Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea"Kuna jamaa yangu hali anayopitia kwasasa nikimfikiria naona mapito yangu hayakuwa kitu.
Hakika mkuu kuna muda hatustahili kulalalama kabisa, kuna watu wanapitia magumu sana.Hata wahenga walisema: "Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea"