‘Hustle’ yako ya kwanza ulilipwa Shilingi ngapi?

‘Hustle’ yako ya kwanza ulilipwa Shilingi ngapi?

Duh nimeanzia mbali mzeebaba

Tangia kuokota scaper, kuuza chupa za bia, kufundisha tempo form 4 shule za kata mpaka kuwa injinia asee sio safari ndogo
 
1.Niko shule ya msingi std 3 au 4 naachiwa genge masaa mawili au matatu nalipwa kama sh. 200-300 na nshakula sana ma apple yale ya Tanga.

2. Nikabeba mchanga kitu kama 10,000
 
Kuuza magugu gugu moja shs 100 mwaka 1995 nilipata 50000 Kwa siku mbili bata lake sitalisahau
 
Milion 800 nikadhulumiwa zote.. hela za deal ya petrol..

Deal ya pili nilifoji doc nikapewa tender ya ujenzi wa daraja kama injinia kumbe nimeishia form 4 na ziro nzuri tu.. Nikapewa hela na gari na dereva wa kuniendesha nikapiga zangu Mil 50..

So katika M 800 ukapat M50??
 
HUSTLE yako ya Kwanza ulilipwa Pesa ngapi?? taja tuone vile wengi tumetoka mbali!
150,000 nilikua napiga tempo shule ya kata 2014 nilipomaliza form six.
Sasa hivi najitolea bure office moja nyeti.
 
Mimi nilianza na 150,000 kwa mwezi alafu pocket money napewa 4m kwa mwezi hii ilikua 2003
 
Milion 800 nikadhulumiwa zote.. hela za deal ya petrol..

Deal ya pili nilifoji doc nikapewa tender ya ujenzi wa daraja kama injinia kumbe nimeishia form 4 na ziro nzuri tu.. Nikapewa hela na gari na dereva wa kuniendesha nikapiga zangu Mil 50..
He.
 
Pesa yangu ya kwanza kukamata nilikuwa nachora picha za Nguo za kina Mama kisha naenda kuuza kwa Mafundi Nguo shilingi 20 nikiwa Darasa la pili.

Japo kipaji cha Uchoraji kilikufa kutokana na Miruzi kuwa mingi kila Mtu alikuwa ni mwenye mamlaka juu yako na Watu wapo zaidi ya 20.
 
Nilivyo ona boss anaminya mabovu wakati napiga kazi gereji ikanibidi nivizie magari ya wateja na kuanza kuuza diesel
 
Nilipata sh 1500 baada ya kuuza mchanga wa kujengea. Wakati wa mvua tulikuwa tunatoa mchanga kwenye mifereji. Ilikuwa 1996.
 
Back
Top Bottom